Baba Nakupenda

Ni kama msosi mezani tu, kinachokupa shibe ni ugali ila kinachodetermine kufurahia chakula ni mboga au viambata vingine vidogo vidogo.

Kwenye majukumu ya familia (zilizo nyingi) ni baba ndo awajibike, baba utalipa ADA za wanao kisha mama atawaita jikoni (mafichoni) na kuwashikisha kiasi kidogo cha ziada kwa siri (kwa sharti la kutomwambia mzee)..... hiki kiasi cha ziada ndo hubeba furaha ya mtoto kuliko ada ambayo ni JUKUMU lako.

Usile Mbegu.
 
Duh, samahani kwa kuuliza, baba yako alisema hivyo kweli?
Yaani alikosa kabisa sababu nyingine ya kujitetea?
Hivyo katika maisha yangu sijawahi ita neno BABA na wala sijui umuhimu wake kwani mama hajawahi olewa tena wala sijawahi kumuona mwanaume ndani ya nyumba yetu tofauti na ndugu tu wa upande wa mama yaani wajomba
Na mm nimebaki peke angu kwa mama kwani hakuwahi zaa tena

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mungu akafanyike Faraja kwako
 
Mungu akafanyike Faraja kwako
 
Watu wenye matatizo km yako hata kauli zenu huwa zinafanana utadhani huwa mnaambizana. Pole sana mkuu. Lkn me nataka nikuambie na kukupa ushauri ambao si lazima uuchukue. Pamoja na kwamba sijapata maelezo ya upande wa Baba yako lkn ukweli hicho unachosema kuhusu weakness za Baba yako ni 15%tu.

Hizo sababu zingine unazotoa unatuonyesha tu kwa hisia kuwa Baba yako alikuwa mbaya sana..na kwa bahati mbaya sana mpaka leo unaamini hivyo na unaposema jambo hilo kwa watu na wakakuonea huruma ww ndo unapata nafuu.

Hasira zako zote zinatokana na sumu aliyokulisha mama yako ambaye ndo alikulea na kwa sababu mlikuwa na shida sana wakati huo,ile sumu iliyokuwa inapandwa na mama yako ilikuwa rahisi tu kukuingia na kusema kweli imekuumiza mno!

Me nakuhakikishia mama yako pamoja na kukulea,lkn ndo alikuwa mbaya sana aliyesababisha hadi Baba yako awatelekeze. Me nakushauri ufanye jambo moja kubwa sana,msamehe Baba yako na muoneshe upendo utakuja kusikia vitu ambavyo hukutarajia kuhusu mama yako. Wanaume huwa ni wastaarabu sana huwa wanajizuia mambo mengi sana kuyasema kwa watoto wao.

Usiangalie sana mafanikio uliyoyapata,hayo mafanikio yamepatikana kutokana na hilo tukio. Pengine ungekuwa unapata kila kitu kwa Baba na mama ungebweteka na usingefika hapo ulipo leo. Hayo mapungufu ya wazazi wako ndo yaliyokujenga na kukupa hasira ya kupambana. Natamani kuandika sana,lkn Acha niishie hapa. Lkn unahitaji ushauri mkuu,hicho kitu kitakutesa maisha yako yote. Na kimsingi ww ndo unaumia kuliko hata Baba yako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Alinichukia kwa dhati kabisa tena bila hiyana, aliapa hatakaa apokee msaada wangu hata kama ndio tone la mwisho la misaada. Yaani aliapa kwa kila njia. LAKINI huwezi amini. Alinifia mikononi, alikaa kwangu 17 yrs. Tena nikampenda kupita.
Ndiyo kishatangulia mbele ya haki lakini nasema; BABA NAKUPENDA. Sioni cha kinitenga na mzazi wangu kwani, nadhani kuna siku aliwahigi kunipa zawadi yoyote hata kama ilikuwa haki yangu.
Ni chizi tu ambaye hampendi BABAKE.
 
Pole ndugu japo nimejikuta natamani kujua umri wako, unaongea kwa hisia kali na umeanza vizuri ila huku mbele ni kama umeipoka siredi hii na deeply personal information.

Kutokuona njemba inatokea ndani kwenu ni heshima anayolinda mama yako, jiandae vema uje kuwa baba kwa wanao.... utajua umuhimu wa baba.

Usile Mbegu.
 
Kwanza naomba nikuhakikishie kua mama yangu hakuwahi kuniambia kua baba kamtenda ubaya au baba mbaya na alikua ananambia baba kasafiri kawnda kunitafutia viatu akieudi atanileta nivae maana nilikua sina natembea peku
Mtu wa kwanza kunieleza ukweli wa nini kilitokea ni mdogo wake baba ambae alikua wa mwisho wao
Aliniambia kisa chote ndio nikaanza kumuliza mam na mpaka leo mama hajawahi kuniambia kua baba mbaya wala nisimpende ila hua ananambia MUOMBEE REHEMA MAANA HAKUNA MKAMILIFU

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Una uhakika ndio baba mzazi?
 
Nimekuelewa zaidi ya sana.. Ni watu wachache wanaoumizwa na wakaweza kubakia na mioyo ya kawaida, cha msingi umemtendea wema mzee wako na Mungu atakulipa..
Kuhusu kuzaliwa peke yako isiwe tabu, Ukipata familia yako ndio watakuwa ndugu zako na ukibahatika kupata marafiki wema, utapata dada na kaka wa kweli.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ila mafaza huwa wanazingua sana...
Halafu inabidi muelewe, mtoto haangalii kiwango unachompa bali ile effort na upendo ulioutumia kumpa.. Unakuta mzee anakesha Bar na marafiki kula bata, mnaskia story tu watu wanavyomsifia anavyojua kuchafua meza na kuhonga watoto wazuri bila hesabu, ila ada na pay ya shule unakuta anakupa nusu mara matumizi mengine anayatoa na pesa ya kujikimu anakupa ile ambayo haiwezi kukusaidia sana..

Ukirudi kwa mama awe anacheza upatu au anafanya kazi ambazo unajua ni kazi kupata pesa ila anaamua kukupa pesa ndogo katika macho ya mzee ila mtoto unafeel jinsi alivyojinyima na kuiumiza bajeti yake.. Hapa ni level ya upendo inayopimwa kwa SACRIFISE

Mzee ukishazeeka, wale marafiki na vimada vinatoweka.. wale wapambe wanatoweka na hapo ndo unaanza kuforce kurudi katika maisha ya watu uliowaeka kando "WATOTO" ili upate faraja.. ukiona hawana time sana unaanza kutafuta sababu za kuhalalisha matendo yako... KUBALI ULIKOSEA USAMEHEWE FULL STOP........

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nani kama Mama!
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Samehe mkuu ubaki na amani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimekusoma kama vile naangalia filam. Mi nakupa hongela kwa kumfanyia mzee kulingana na aliyoyafanya
 
Mimi kitendo tu cha mzee wangu kumpanda mother nikazaliwa kinatosha kumshukuru ayo mambo mengine ni matokeo tu.Inawezekana siku hiyo mzee anataka vyombo mother alikua anazingua au mother ndo alikua tayar mzee anazingua ila yote kwa yote niwashukuru tu kwakutimiza majukumu yao yakunifyatua,mambo ya malezi hapa kila mmoja ana historia yake kwasababu dunia ina mengi.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…