Baba na mwanaye waoa mabinti mapacha

As long as hawali mmoja hakuna shida hapo. Mbona mengi kaoa mwanae na hakuna nongwa
 
Wala Mimi sipo na Bashite nimeleta habari kama nilivyoipata
 
Kama hao wahusika ni waislam bhasi uislam unasema hiviiiii...

(23) An-Nisaa

Mmeharimishiwa mama zenu, na binti zenu, na dada zenu, na shangazi zenu, na khaalati zenu, na binti wa ndugu mume, na binti wa dada, na mama zenu walio kunyonyesheni, na dada zenu kwa kunyonya, na mama wa wake zenu, na watoto wenu wa kambo walio katika ulinzi wenu walio zaliwa na wake zenu mlio waingilia. Ikiwa hamkuwaingilia basi hapana lawama juu yenu. (Pia mmeharimishwa) wake wa watoto wenu walio toka katika migongo yenu. Na kuwaoa pamoja dada wawili isipo kuwa yale yaliyo kwisha pita. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe Mwenye kurehemu.

(24) An-Nisaa

NA WANAWAKE wenye waume, isipo kuwa walio milikiwa na mikono yenu ya kulia. Ndiyo Sharia ya Mwenyezi Mungu juu yenu. Na mmehalilishiwa wasio kuwa hao, mtafute kwa mali yenu kwa kuowa pasina kuzini. Kama mnavyo starehe nao, basi wapeni mahari yao kwa kuwa ni waajibu. Wala hapana lawama juu yenu kwa mtakacho kubaliana baada ya kutimiza waajibu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua na Mwenye hikima.

MyComment: Hakuna uharamu hapo juu yao kwa mujibu aayaat hizi na ndizo guidelines za kuoana
 
Asante kwa ilmu hii adhimu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…