Baba na mama wana mgogoro mkubwa nisimame upande upi?

Baba na mama wana mgogoro mkubwa nisimame upande upi?

panama city

New Member
Joined
May 12, 2015
Posts
1
Reaction score
0
Waheshimiwa,

Mimi ni baba wa watoto wawili ni mfanyakazi na nimeoa pia. Mzee wangu pamoja na utu uzima alionao aliingia kwenye penzi zito na secretary wake maana ana kampuni yake binafsi inahusika na consultation ya accounts, auditing, risk na tax. Baada ya kuanza mapenzi na huyo secretary wake akahama nyumbani na kumwacha mama peke yake akaenda kuishi kwa secretary nyumba ambayo yeye baba ndio aliijenga.

Amekaa na huyo secretary kwa miaka 2 na kitu. Baba ni mgonjwa wa Kisukari sasa yule binti akamshauri baba atahiriwe Mimi binafsi sikua najua baba hajatahiriwa. Wakaenda pamoja hospital kwa zoezi hilo, sijui kwanini mzee hakuwaambia hospital kwamba anaumwa Kisukari. Baada ya kutahiriwa kile kidonda kimeshindwa kupona kabisa, sasa ni miezi sita na kimekua life threatening. Hivi sasa amelazwa anauguzwa na yule secretary na kidonda kinazidi kuoza ndugu wana JF ukikiona hicho kidonda uume umeliwa kabisa chochote kinaweza kutokea.

Mama aliniita mimi na wenzangu na kutuweka kikao, maana mimi naishi kwangu wenzangu wanne bado wapo nyumbani
Akatuambia, nawapa onyo nyinyi wote yoyote atakae kanyaga kwenda hospitali kumuona mzee basi atakoma kuwa mtoto wangu, akasema kwa kuwa mzee aliitelekeza familia na kutokomea kwa huyo malaya na tulimuonya sana hakusikia hivyo muacheni afie huko na hata akifa azike huyo malaya peke. Sasa mimi nimekua nikienda hospital kwa kulazimisha hivyo hivyo, sasa naonekana msaliti, wadogo zangu wametii agizo la mama hivyo hawafiki kabisa.

Ndugu wa baba wanalaumu sana kuwa mama na ndugu wengine wapo wapi mimi nashindwa cha kuwajibu. Wazee wa ukoo wamemwita mama na kumuonya kuwa lolote likitokea asije akadai mali au mirathi, wakamuonya atakosa yeye na watoto anaowakataza kwenda kumuona na kuwa pamoja na mzee. Mama akawajibu kuwa yeye haitaji mirathi huyo malaya achukue tu kwa kweli hali ni mbaya na ni aibu kwa familia yaani tunaenda mimi na mke wangu tu hospital baba huuliza wenzio wako wapi mimi nashindwa cha kumjibu. Wakuu hali ni kama hiyo, ofisi ya mzee imefungwa hali si hali.

Naombeni mawazo yenu
 
So sad sijamalizia kusoma sina hata ushauri
 
aiss...nachoweza ni kukutia nguvu tu!endelea kwenda hosp na kumtia faraja baba...kama ni mtu wa maombi mkumbuke mzee katika maombi yako...mambo mengine yatajulikana namna na kuyashughurikia kadri yatakavyokuwa yakitokea.
 
Ndugu yangu ulichofanya ndio uamuzi sahihi.

Kwa sasa hayo magomvi ya Mzee na Mama achana nayo na usimsikilize sana Mama juu ya hili, kwa sasa muuguze na umwangalie Mzee wako utakavyoweza.Sie sote hufanya makosa.

Na watoto waliomsikiliza Mama juu ya hilo nasikitika kusema kuwa ni wapumbavu na hawana akili, tusikilize wazee kwa masuala mazuri na ya kujenga; huu ni ugonjwa na as long ni Baba yenu na hakuwatupa, aliwatunza, basi mna wajibu wa kumfariji na kumwangalia.

Kuna wimbo uwa naupenda "Bwana kama wewe ungetazama makosa yetu, nani angesimama?"
 
duh hakuna jinsi hata baba akiwa malaya ni baba yenu tu.. shauri ndugu zako muende kumwangalia huwezi jua mama alikosea wapi mapaka baba akahama home?

mkuu wanawake tunaendeshwa na hisia mama ni mwanamke .. sisitiza ndugu zako wakamwone baba yenu.....

je huyo baba alikuwa anawasaidia kimasomo ?
 
Duh poleni sana,maamuzi anayochukua mama yanatokana na hasira,mzee tayari ni mgonjwa kumtenga haisaidii wewe kama mtoto wake mtu mzima mwenye ufaham unapaswa ujue nini chakufanya.Hata kama wazazi wenu wana ugomvi yeye atabaki kuwa babaako nakushauri umsaidie mzee wako.Mama mpe muda apoe coz anaugulia maumivu ya usaliti.
 
Umeamua vema kuwa muwazi na kutofuata ushauri wa mama. Endelea kumtunza Baba yako. Washauri na wadogo zako waachane na msimamo wao, baba yenu anahitaji faraja yenu zaidi.
 
Kiukweli hadi mama kasema haitaji mali za mumewe inaonesha ni kiasi gani ameumia na msimamo wake ni wa kweli...cha kushauri jarbu kuongezea na mzee pia amuombe msamaha mkewe ata kam hawatarudiana ila wawe na mawasiliano ili mzee aweze pata faraja ya wanawe
 
Wewe ndio Mwanamume Komaa hivyo hivyo.
Sijajua ni kwanini Mama anashindwa kurudisha Moyo nyuma kwani si lazima wakashirikiane Kitanda hata kumuuguza sio vibaya
Washauri wadogo zako kuwa yule ni baba yao kma hawamtambui wamuulize mama yao Baba yao ni yupi ili wawe wanamjulia hali.

Kwa huyo secretary si mlaumu kwani naonesha Ukorofi wa mama yenu ndio uliomsababisha hata Baba ahame nyumba
Ni Familia nyingi Baba na Mama wakishaanza kufikia 65' yrs kina Mama huzeeka na kuwa na vuhasurahasira na kusitisha huduma zote hiyo husanbabisha Wanaume wengi kufa kwa kutengwa au Kero na gubu
 
Ndugu yangu ulichofanya ndio uamuzi sahihi.

Kwa sasa hayo magomvi ya Mzee na Mama achana nayo na usimsikilize sana Mama juu ya hili, kwa sasa muuguze na umwangalie Mzee wako utakavyoweza.Sie sote hufanya makosa.

Na watoto waliomsikiliza Mama juu ya hilo nasikitika kusema kuwa ni wapumbavu na hawana akili, tusikilize wazee kwa masuala mazuri na ya kujenga; huu ni ugonjwa na as long ni Baba yenu na hakuwatupa, aliwatunza, basi mna wajibu wa kumfariji na kumwangalia.

Kuna wimbo uwa naupenda "Bwana kama wewe ungetazama makosa yetu, nani angesimama?"
wewe kama mwanaume, utajisikiaje katika maisha yako ukiwa umekosea halafu watoto uliowazaa wasije kukuona hospital? wewe nenda hospital, mamako hata akikupa laana laana isiyo na sababu huwa haifanyi kazi. wewe mwambie mama mimi sitaingilia ugomvi wenu, na ninawapenda wote hata baba nampenda na nitasikitika kumpoteza. usimtose dingi aisee.
 
Kutokuelewana kwao hakuwazuii kutambua kuwa huyu ni mama na yule ni baba, mama anawatumia kama fimbo ya kumchapia baba, wakati sio sahihi!
Mwana komaa na Mshua, umefanya uamuzi sahihi. Hakuna laana toka kwa mama itakayokufika kwa hayo ufanyayo. Mungu akupe nguvu.
 
Komaa na mzee wewe pia umeoa unajua matatizo katika ndoa yapo tens ndo pakujifunzia wewe ndo unatakiwa kuwa MTU Wa karibu Wa baba yako huo ulioonyesha uanaume washauri na ndugu zako Wa kiume waliobakia
 
we endelea kwenda bana hayo matatizo tunayo wengi bora wewe baba kaiacha nyumba sie alifukuzwa akaletwa mwingine mungu katusaidia tumemjengea yake mama alikuwa anasema hivyohivyo lakin tumemuelewesha kwenye shida aaah! sasa wanawasiliana
 
mtoto mwerevu ni fahari ya baba yake ila mtoto mpumbavu ni aibu kwa mama yake
 
mkuu wengi wamekupa ushauri wa maana hata mimi NAKUSHAURI ENDELEA KUMUUUZA BABA UGONVI WAKE NA MAMA YAKO HAUKUHUSU. tafadhali ukiweza wakonvice hata wadogo zako na mama pia.
 
Nani kakuambia ww msuruhishi uwaache washauriwe na wengine.

Wewe endelea kumjulia hali kwa kuwa ni mzazi wako.
 
Mama yenu ana matatizo kumukichwa, kuna viashiria kuwa ndiye chanzo cha mgogoro kwenye ndoa yake. Angependa kuona kila anayemchukia basi dunia nzima imchukie.

Mhudumieni Baba yenu kwa maana yeye ndio nyinyi, mna haki ya kuionyesha dunia kuwa ndani yenu kuna chembehai nyiiiiiiingi za upendo, mkiwa karibu na baba yenu mtakuwa mmeipambana dhambi ya "visasi"

Mungu anaweza kukutendeeni muujiza.
 
Ujue mama anashindwa kutofautisha kua nyie yule ni baba yenu wakati yeye ni mme wake, mnakila haki yakwenda kumuona mzee wenu hata kama mama anamuona hafai ila anabaki kua baba yenu,,ao wadogo zako wasipoangalia watapata laana coz yule ni baba yao,,,mama pia mumshawishi abadil au alegeze misimamo
 
Back
Top Bottom