Baba Masaba: Mnaijeria aliyeoa wake 86 afariki akiwa na miaka 93

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
_93864207_ce77c8d0-34b3-44d2-b99a-fb252e3f6c29.jpg


Mhubiri wa zamani wa Kiislamu nchini Nigeria, ambaye alioa takribani wake 86 amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 93.

Mohammed Belo Abubakar, maarufu kama Baba Masaba, amefikwa na mauti akiwa nyumbani kwake siku ya Jumamosi kutokana na maradhi ambayo hata hivyo hayakubainishwa.

Watu wengi wamehudhuria msiba wake.

Gazeti la Daily Trust nchini Nigeria, limeripoti kwamba marehemu alikuwa na wake wanaofikia 86 mwaka 2008 - na umaarufu wake ulipozidi - idadi ikaongezeka na kufikia 130 wakati anafariki. Miongoni mwao wakiwa wajawazito.

Mnamo 2008, BBC iliripoti pia kuwa Bwana Abubakar alikuwa na watoto takribani 170 huku Daily Trust likieleza kwamba ameacha watoto 203.

Wakeze ambao BBC walizungumza nao mwaka huo (2008), walieleza kuwa walikutana na Bwana Abubakar walipoenda kwake kwa ajili ya maradhi, ambayo wanadai alikuwa akiyatibu.

''Mimi siwatafuti, wao ndio huja kwangu. Nafuata maagizo ya Mungu. Ameniagiza niwaoe nami natimiza hilo'', kauli ya Baba Masaba.

Ganiat Mohammed Bello, mwanamama aliyedumu ndoani na Baba Masaba kwa miaka 20, alipozungumza na BBC alisema kuwa walikutana kipindi akiwa anasoma sekondari, na ni mama yake ndiye aliyempeleka kwa ajili ya ushauri/matibabu fulani. Baadae akamposa.

"Nilikataa kata kata kuolewa na mwanaume mzee, lakini aliniambia kuwa hilo ni agizo la Mungu'', alisema Ganiat.

Madai hayo (kuwa ameagizwa na Mungu) yalikanushwa vikali na mamlaka za dini ya kiislamu nchini humo ambazo zilihusisha matendo ya familia ya Baba Masaba kuwa ni ya kishirikina.
 

Attachments

  • _93864207_ce77c8d0-34b3-44d2-b99a-fb252e3f6c29.jpg
    _93864207_ce77c8d0-34b3-44d2-b99a-fb252e3f6c29.jpg
    14.3 KB · Views: 44
More wives more holes...........................................................
 
Back
Top Bottom