Baba legeza tumeshanyooka

Nyankuru Wankuru

JF-Expert Member
Joined
Apr 22, 2018
Posts
1,199
Reaction score
1,349
Yaani hakuna watu walioonyooka kama watumishi wa umma ,haijalishi mkuu wa idara, afisa, mhudumu wa ofisi ,waziri, RAS, ma ded wote nidhamu imerejea.

Hapa ni kazi tuuuuu

Kunywa kunywa hovyo machai, makahawa maoficn kumepungua. Labda mawaziri, rc, RAS na makatibu wakuu na wengine hao wanaishia kupiga miayo.

Extra duties kuzipata siku hizi ni kazi kazi.

Kujiandikia ma perdiem ya uongo uongo wamekoma, hapa pccb, kule tiss , wanyooshe babaaa.

Mkuu ninachokuomba, kuna wanaojiita wakuu, kila mwezi wao wananunuliwa magazeti na wanapewa hela za mawasiliano , naomba uzipige marufuku.

Utakuta maafisa wasiopewa pesa za mawasiliano ndio huumia kwa kutumia pesa zao ku ratibu kazi toka ngazi mbali mbali,huku wakuu wa idara wamekaa tu ikizingatia wana pewa pesa za mawasiliano.

Kwenye chai mida ya breakfast, watu huenda kunywa chai na kurudi fasta kuhudumia wananchi.

Ila bado kuna wengine wakienda kunywa chai hufanya maeneo hayo vijiwe vya kupiga stories kama vijiwe vya kahawa.

Siku hizi vikao vya bajeti ndio wezi na wadokozi huzifumania huko

Baba hongera sanaa, kwa kazi nzuri
 
Dah mlitesa mno na safari zenu za nje eti training mara India, England Holland, mtu akirudi mwisho wa mwezi ana 20M kila mwezi imagine mtu anasafiri mara mbili hata tatu. Wakati ukuta km mlihonga nyumba ndogo hamkuwekeza imekula kwenu! Subirini jiwe atoke. Na atakayekuja mumloge ndo aruhusu khaaa mlitutesa
 
Sasa ukisikia roho mbaya ndio hii...

Ivi unaakili kweli wewe?

Per diem na extra duty ziko kisheria, okey wasipewe, je unadhan mtu atafanya kazi kwa motisha? Na asipofanya kazi kwa motisha unadhani unamkomoa yeye au mwananchi kama wewe?

Tumia kichwa kufikiri sio kuvalia wigi, sawa?
 
Mpaka akili zikae sawa, si bado tunajifanya kujiuguza wehu.

Hii ngoma tutasimulia watoto wetu na wajukuu.
 
Akikujibu usisahau kunitag
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…