Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,286
- 10,831
JESHI la Polisi wilayani Chato mkoani Geita, limemfikisha mahakamani Kazimili Dotto, akituhumiwa kumbaka na kumlawiti mtoto wake wa kambo, ambaye ni mwanafunzi wa darasa la pili.
Mshtakiwa huyo ambaye ni mkazi wa Kijiji na Kata ya Makurugusi wilayani hapa, anadaiwa kumbaka na kumlawiti mtoto wa mkewe na kutishia kumuua kwa kisu iwapo angesema kutendwa ukatili huo.
Katika Mahakama ya Wilaya ya Chato, Mwendesha Mashitaka wa Polisi, Mauzi Lyawatwa, alidai mshitakiwa anakabiliwa na kosa la ubakaji ambalo ni kinyume cha kifungu cha 130(1)(2)(e) na 131(1) cha Sheria ya Makosa ya Jinai.
Alidai kuwa Februali 17 mwaka huu, majira ya mchana, mshitakiwa akiwa nyumbani kwake, alimwita mtoto huyo na kumwomba amletee maji ya kunywa ndani ya chumba anacholala na mkewe kabla ya kumbaka na kumlawiti.
Alidai kuwa baada ya mtoto huyo (jina tunalihifadhi) kufikisha maji, alikamatwa kwa nguvu na kutupiwa kitandani na baba yake kisha kumvua nguo za ndani na kuanza kumbaka na kumlawiti.
Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa wakati hayo yakifanyika, mama wa mtoto alikuwa shambani na aliporejea, alisukuma mlango wa chumba chake uliokuwa umeegeshwa, kisha kumfumania mumewe akiwa kifuani kwa mtoto wao huku wote wakiwa hawana nguo.
Alidai kuwa baada ya kuona hali hiyo, aliamua kupiga yowe kuomba msaada na majirani walipofika, waliamua kuita askari wa Jeshi la Polisi, ambao walifika na kumweka mshitakiwa chini ya ulinzi.
Baada ya kutolewa maelezo hayo na Upande wa Jamhuri, mshitakiwa alikana kuhusika na mashtaka yanayomkabili.
Hakimu Mkazi Mfawidhi Odira Amworo, aliahirisha kesi hiyo hadi Februali 24 mwaka huu.
Chanzo: Nipashe