Baba Diamond aomba mwanae amkatie angalau bima ya afya

Kituko gani amefanya mama Chibu? Hayo ni malipo yake ya starehe alizo fanya akiwa kijana bila kujiwekea akiba uzeeni yaani mzee ana micheni shingoni kama mbwa ni wa kumuonea huruma kweli.
Unaweza kula starehe bila kuonekana kuwa against jamii inayokuzunguka. Huyo baba yake hana uzee wowote. Anaendekeza njaa tu, na hii ni baada ya kuona mafanikio.
 
Inawezekana sikatai, lkn pia ni lazima baba alikosea sehemu..kitu ambacho wengi hatujui tunajudge tu.
Huyo mzee aache kulalamika maana haisaidii, vyovyote vile ilivyo lkn Sasa anavuna alichopanda., Tunaona kwenye jamii inayotuzunguka jinsi ambavyo wababa wanasababisha mateso kwa familia zao na mwisho wa siku wanarudi kunyenyekea wakati tayari alishaumiza mioyo ya mke na watoto.
Mungu anisamehe lkn simuonei huruma. Ana watoto wengine why Kila Mara ni Diamond tu? Anachosha
Sidhani kama unatenda dhambi yoyote kutomuonea huruma. Hana ulemavu wowote ila anaendekeza njaa tu. Hayo mafanikio yasingekuwepo angefanya nini!
 
Akifanya mahojiano na gazeti mwananchi baba mzazi wa msanii diamond platnumz ambemuomba mwanae angalau amkatie bima ya afya kwani Hali yake kwa Sasa sio nzuri. Ilinichukua muda kumshawishi na baadaye kufanya mahojiano na Abdul Juma Isack ambaye ni baba wa msanii wa maarufu wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz. Ungeweza kukata tamaa ya kuendelea kumshawishi kwa sababu ana hoja nyingi na pengine nzito.

“Sioni mabadiliko kwangu,” anasema baba huyo mwenye umri wa miaka 52 wakati akieleza sababu za kukataa kufanya mahojiano. “Tangu nianze kuhojiwa, nilikuwa nikiamini kuwa ningeweza kubadili msimamo wa mwanangu anayetajwa kuwa msanii tajiri namba moja Tanzania. “Badala yake naonekana kama nalilia kusaidiwa na mtoto wangu. Pamoja na kuwa na mtoto maarufu ndani na nje ya nchi, maisha yangu ndio kama hivi unavyoyaona. Naishi Magomeni Kagera na nyumba yangu ya kawaida tu, ambayo naamini hata siku Diamond akikwama kimaisha atakuja kuishi kwa kuwa hapa ni kwao, japokuwa simuombei hilo.”

Abdul anasema kwa muda mrefu Diamond amekuwa hafanyi mawasiliano naye na hajui sababu . “Najiuliza ni nini kikubwa namna hiyo nilichomkosea?” anahoji baba huyo. “Ninatamani siku moja nikutanishwe katika mahojiano na Diamond na mama yake ili kila mmoja atoe alilonalo moyoni.“Huyu mtoto kanipa majina mengi kutokana na yanayoongelewa mtaani kwamba nilimtelekeza, wakati hakuna ukweli wowote. Mimi niliachana na mama yake wakati akiwa kidato cha kwanza.

Kwa umri hu alikuwa anajielewa na anajua sababu za kuachana kwetu. Kama kuna jingine wanalolijua wao kwamba nimewakosea, basi tuhojiwe hata mbele za watu ili lifahamike na kuyamaliza kuliko hiki wanachofanya kwangu. “Kasababisha kila kona ninayopita nanyooshewa vidole kuwa niliwatosa. Ifike mahali haya mambo tuyaweke sawa kwa kuwa naumia sana, hawajui tu. Si kwamba, labda ni kwa kutaka msaada wao, hapana. Bali kila mtu awe ameitakasa nafsi yake na kuondokana na vinyongo.”

Baba huyo wa Diamond anasema hata mawasiliano na mzazi mwenzake ni pale anapojisikia. “Tena wakati mwingine na maneno ya karaha, lakini ana afadhali kuliko mtoto ambaye mara ya mwisho tuliwasiliana akiwa na Wema Sepetu ambaye alikuwa akija naye hapa mara kwa mara kunisalimia,” anasema.

Kwa sasa maisha si mazuri. Abdul anajihusisha na biashara ya viatu. Huchukua viatu kwa malikauli katika soko la Karume na kuvipeleka kwa wateja wake mahali walipo. “Lakini maisha kwa sasa si mazuri kwa kuwa nasumbuliwa na tatizo la miguu. Inanifanya wakati mwingine nishindwe kutembea muda mrefu,” anasema mzazi huyo.“Kama unavyoniona miguu inaniuma na wakati mwingine nashindwa kuinuka hata kitandani.

“Naona ni wakati sasa na mimi kuwa na eneo la kufanya biashara hii, lakini ndio hivyo uwezo, walau ningekuwa na gari ningeweza kuzunguka nalo hata kwa kuendeshwa ili nisiwapoteze wateja wangu, lakini sina namna.” Anasema hata uwezi wa kugharimia matibabu, hana. “Labda ningekuwa na bima ya afya ingekuwa msaada kwangu lakini ndio hivyo sina,” anasema.
Apata msaada mtandaoni

Hata hivyo, msaada wake mkubwa uko kwa mtoto wake wa hiari anayeishi London, Uingereza anayeitwa Zubeda. Walijuana na mtoto huyo katika mitandao ya kijamii baada ya kuona mahojiano yake akielezea maisha anayoishi.


Mwananchi sourceView attachment 968793
Huyu dingi ...ashike mike aingie mtaani...aanze kuimba ....ashindane na mwanae.... atapata fedha....kiasi chake
 
Diamond hana wajibu wa kumtuza baba yake someni vitabu vya dini hata sheria. Mzee baba ndie alikuwa na wajibu wa kumtunza mtoto hakufanya hivyo. Nachokiona huyu mzee hana shida kama anavyodai bali ni mzee mpenda makuu, anataka gari atembelee wateja wake tena gari hilo anunuliwe na mtoto aliemtupa. Ajabu sana. Diamond rudisha roho sio kwa sababau unampenda huyo mzee bali kwa ajili ya jina lako huyu mzee anaweza kukutia nuksi na maneno yake.
 
Mzee anakosa 30,000 bima ya afya, anazingua bwana. Apige tu kimya aache kulalamika maana haisaidii
 
Hivi akifa hawatakwenda msibani?
Watakwenda Mkuu, gharama za msiba watazibeba....
Na Mama Domo atatoa na Machozi, akilia akisema Japo tulikua na utofauti Ila ni Mzazi mwenzangu Kafa!

Hela za Domo Sasa zinaliwa na Baba wa Kambo wa Domo, kwa kazi ya kusimamia Ukucha tu .......
Mwanamke ni Nyoko....!
 
Watakwenda Mkuu, gharama za msiba watazibeba....
Na Mama Domo atatoa na Machozi, akilia akisema Japo tulikua na utofauti Ila ni Mzazi mwenzangu Kafa!

Hela za Domo Sasa zinaliwa na Baba wa Kambo wa Domo, kwa kazi ya kusimamia Ukucha tu .......
Mwanamke ni Nyoko....!

Wanatia aibu sana hawa domo na mama yake
 
Hapo mama domo ndiyo kavuruga yote, ila tusubiri tuone mwisho, BABA NI BABA TU..Kama unazo saidia...
 
Kumbe huyu mzee ni miaka 52 tu, aache kulialia apambane. Jana nimesoma mahali mwenzake wa miaka 52 kasaini mkataba wa miaka 3 kuchezea timu ya daraja la kwanza huko Japan.
Wabongo kwa uvivu wetu tunapenda sana kutafuta excuses na kuwatupia watu lawama.
 
Kumbe huyu mzee ni miaka 52 tu, aache kulialia apambane. Jana nimesoma mahali mwenzake wa miaka 52 kasaini mkataba wa miaka 3 kuchezea timu ya daraja la kwanza huko Japan.
Wabongo kwa uvivu wetu tunapenda sana kutafuta excuses na kuwatupia watu lawama.
habari ya 2018 ana 55 sasa
 
Kama alivyokuwa mdogo angekua unamwambia apitie kijiweni kwake manzese aje achukue pesa ya kununulia mihogo shule wala asingemsahau
 
Siku huyu Baba akipoteza uhai Diamond ajiandae kuwa attacked sana, labda yeye amtangulie
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom