BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,769
- 288,283
WAGOMBEA MTUKEMEE
Katika hali ya kawaida, Vijana huwazika wazee. Katika hali isiyo ya kawaida, wazee huwazika Vijana.
Katika hali ya kawaida, Viongozi wa dini huwakemea Wana siasa. Katika hali isiyo ya kawaida, Wana siasa huwakemea Viongozi wa dini.
Tuna hali isiyo ya kawaida katika taifa letu. Wanasiasa na Viongozi wa serikali wanapaswa kutukemea Viongozi wa dini.
Sheria na katiba ya nchi vinaruhusu kufanya Uchaguzi kila baada ya miaka mitano. Viongozi waliopo wawe wazuri au wabaya, sharti uchaguzi ufanyike kila baada ya miaka 5.
KWA hiyo, Si sahihi kuwaona watanzania wenzako watakaochagua upande huu au ule kuwa ni wasaliti au wazalendo zaidi. Sisi Viongozi wa dini tusijipe haki zaidi ya kuhukumu nani msaliti na nani mzalendo kwa kutumia kipimo kimoja tu - cha kupigia kura upande fulani.
Tunaowaita wasaliti ndio wamejaa mahekaluni mwetu sambamba na wazalendo. Kinachoonekana wazi lakini ni vigumu kukisema wazi ni kuwa sisi Viongozi wa dini tumewasaliti waumini wetu kwa kusema kwetu au kukaa kimya kwetu. Tumemsaliti Mungu wetu kwa kusema kwetu au kukaa kimya kwetu. Tumeamua kuwatumikia wanasiasa na vyama vyao, tukawaacha watu na Mungu wao. Kamwe uamuzi wa siri au wa wazi wa waumini kupiga kura kumkubali huyu au yule kusitafsiriwe kuwa USALITI au UZALENDO. Ni utekelezaji wa takwa la kikatiba.
Kuna nyakati Mungu huifanya mioyo yetu kuwa migumu ili ukuu wake uweze kudhihirishwa kwa hakika. Ilikuwa hivyo kwa Farao, yaweza kuwa hivyo kwetu Viongozi wa dini. Na tukemewe na ambao tungewakemea. Chumvi imekwisha kuharibika.