Baba Amuua Binti Yake Baada ya Kumpachika Mimba

Dr. Chapa Kiuno

JF-Expert Member
Sep 11, 2009
443
18
</SPAN>


Ana Matias ambaye aliuliwa na baba yake baada ya kupata mimba yake
Tuesday, October 13, 2009 1:41 AM
Baba mmoja wa nchini Marekani amepandishwa kizimbani baada ya kumuua binti yake mwenye umri wa miaka 14 baada ya kumpachika ujauzito.


Miguel Matias wa New York, Marekani alikiri mahakamani kumuua binti yake aliyekuwa na umri wa miaka 14 baada ya kumpachika mimba.

Mwili wa binti yake Ana Matias ulikutwa ukiwa umefichwa kwenye tanki la maji kwenye nyumba yao mwezi februari mwaka huu baada ya baba huyo kuamua kuwaambia ukweli polisi mauaji aliyoyafanya.

Awali Matias alikamatwa februari 28 mwaka jana baada ya kumuua binti yake kwa kumnyonga akidai alifanya hivyo baada ya kumkuta akiandika mambo ya ngono kwenye kompyuta yake.

Lakini iliwachukua polisi mwaka mzima kuweza kugundua ukweli kuwa binti huyo alikuwa na mimba ya wiki 12 aliyopachikwa na baba yake.

Matias alikuwa akijulikana kwa marafiki zake na ndugu zake kwa kupenda kuwanunulia zawadi watoto wake na kuwapeleka kwenye migahawa mbali mbali.

Kumbe Matias mwenye umri wa miaka 35 alikuwa na siri zake zingine akifanya mapenzi na binti yake kwa siri.

Baada ya kukiri kosa lake mahakamani, Matias alimuomba hakimu amtupe jela kati ya miaka 30 na 50.

"Nataka nifungwe jela kati ya miaka 30 na 50, nilimuua kwa kumnyonga kwa kutumia waya wa umeme", alisema Matias.

Kesi yake inaendelea na iwapo mahakama itamuona ana hatia, Matias huenda akahukumiwa kifungo cha kati ya miaka 25 jela na kifungo cha maisha.



Source: AP


 
Back
Top Bottom