Baadhi ya Wawakilishi wa CCM ZNZ wapinga uchaguzi wa marudio

Baraghash

JF-Expert Member
Dec 18, 2012
2,713
1,789
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimeingia tena katika mvutano na wanachama wake waliokabidhiwa vyeti vya ushindi wa uwakilishi na udiwani katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 25 mwaka jana, kwa kushikilia kuwa hawataki uchaguzi wa marudio, anaandika Jabir Idrissa.

Baadhi ya wawakilishi wamesema hawaoni sababu ya msingi ya chama kujiingiza katika uchaguzi mwingine wakati wanachama wake walishatangazwa washindi baada ya kuchaguliwa na wananchi.

“Kwa mfano mimi binafsi nimetangazwa mshindi wa kiti cha uwakilishi jimboni kwangu. Nina cheti nilichokabidhiwa na msimamizi wa uchaguzi wa jimbo, sasa inaingia akilini kweli kuniingiza kwenye uchaguzi mwingine?”

Mwakilishi huyo ambaye kwa sababu za kuhofia kuchukuliwa hatua za kinidhamu na chama hataki kutajwa kwa jina, amesema kuna shida ndani ya akili za viongozi wa CCM ambazo zinasababisha kuingiza nchi kwenye mgogoro mkubwa wa kikatiba na kisiasa.

“Huwezi kuamini viongozi wetu wanashikilia uchaguzi wa marudio ilhali wanajua kwamba hakuna haki ya kuwaingiza wananchi kwenye uchaguzi mwingine kwa kuwa uliofanyika Oktoba na kupatikana washindi haukuwa na matatizo,” amesema.

Alipoulizwa kama wana mshikamano katika msimamo wake kwa maana ya wawakilishi wenzake wanafikira kama yeye, mwakilishi huyo amesema “sote tunazungumzia suala hili tangu siku zile za mwanzo baada ya uchaguzi kufutwa, lakini tatizo ni viongozi wetu wachache wa juu kufikiria zaidi maslahi binafsi kuliko ya nchi.”

Mwakilishi huyo wa moja ya majimbo ya Wilaya ya Mjini, anapozungumza hayo, kunakuja taarifa kutoka ndani ya CCM kuwa hata baadhi ya wajumbe wa Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya Taifa Zanzibar hawaafiki uchaguzi wa marudio.

“Nakwambia tunapinga suala hili lakini wachache wanalishikilia kama vile lina maana yoyote kwa maslahi ya nchi na watu wake. Wapo viongozi wakubwa wanadhani wana haki ya kuungwa mkono kwa kila wanachokiamini wao, kumbe wanachokipigania ni maslahi binafsi ndani ya utashi wa kujenga siasa za chuki nchini. Tufike mahali mtindo huu ukome ili kuipa nchi nafasi ya kusonga mbele kama wenzetu,” amesema.

Kwa mujibu wa taarifa, kamati maalum ilifanya kikao katikati ya wiki iliyopita mjini Zanzibar na kujadili uchaguzi wa marudio lakini idadi kubwa ya wajumbe walipinga uchaguzi huo.

Taarifa zinasema wajumbe 35 walipiga kura ya kukataa uchaguzi wa marudio, tisa waliridhia na wengine walikataa hata kupiga kura.

“Baadhi ya wajumbe waliamua kutoka nje ya ukumbi kwa kuchukizwa na chagizo za viongozi wakubwa wachache kulazimisha uchaguzi wa marudio,” amesema mwanamama kutoka Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Pamoja na CCM kushikilia kuendeshwa uchaguzi wa marudio Machi 20, bado wanavutana kwa kila kukicha kuendeleza vikao vya mikakati wakati dunia nzima inaishangaa Zanzibar kwa kujiingiza katika utaratibu wa kukandamiza maamuzi ya wananchi waliochagua kwa utulivu mpaka Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) kutangaza matokeo ya majimbo 31 ya urais na kukamilisha kazi ya kuhakiki kura za majimbo tisa mengine.

chanzo: zanzinet
 
Kama walishinda kwa mizengwe mizengwe wajiandae kutumbuliwa. Uchaguzi uko pale pale.
 
ISIS na Al Shabaab wamejitega vizuri kabisa kuchukua vijana watakaokimbia machafuko na kuwatumia kuja kujitoa muhanga siku za mbeleni. Zanzibar hautakuwa salama, bara haitakuwa salama na dunia haitwakuwa salama. Kisa ni ukurunziza wa Ally Mohamed Shein kugoma kuachia madaraka baada ya kushindwa uchaguzi
 
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimeingia tena katika mvutano na wanachama wake waliokabidhiwa vyeti vya ushindi wa uwakilishi na udiwani katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 25 mwaka jana, kwa kushikilia kuwa hawataki uchaguzi wa marudio, anaandika Jabir Idrissa.

Baadhi ya wawakilishi wamesema hawaoni sababu ya msingi ya chama kujiingiza katika uchaguzi mwingine wakati wanachama wake walishatangazwa washindi baada ya kuchaguliwa na wananchi.

“Kwa mfano mimi binafsi nimetangazwa mshindi wa kiti cha uwakilishi jimboni kwangu. Nina cheti nilichokabidhiwa na msimamizi wa uchaguzi wa jimbo, sasa inaingia akilini kweli kuniingiza kwenye uchaguzi mwingine?”

Mwakilishi huyo ambaye kwa sababu za kuhofia kuchukuliwa hatua za kinidhamu na chama hataki kutajwa kwa jina, amesema kuna shida ndani ya akili za viongozi wa CCM ambazo zinasababisha kuingiza nchi kwenye mgogoro mkubwa wa kikatiba na kisiasa.

“Huwezi kuamini viongozi wetu wanashikilia uchaguzi wa marudio ilhali wanajua kwamba hakuna haki ya kuwaingiza wananchi kwenye uchaguzi mwingine kwa kuwa uliofanyika Oktoba na kupatikana washindi haukuwa na matatizo,” amesema.

Alipoulizwa kama wana mshikamano katika msimamo wake kwa maana ya wawakilishi wenzake wanafikira kama yeye, mwakilishi huyo amesema “sote tunazungumzia suala hili tangu siku zile za mwanzo baada ya uchaguzi kufutwa, lakini tatizo ni viongozi wetu wachache wa juu kufikiria zaidi maslahi binafsi kuliko ya nchi.”

Mwakilishi huyo wa moja ya majimbo ya Wilaya ya Mjini, anapozungumza hayo, kunakuja taarifa kutoka ndani ya CCM kuwa hata baadhi ya wajumbe wa Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya Taifa Zanzibar hawaafiki uchaguzi wa marudio.

“Nakwambia tunapinga suala hili lakini wachache wanalishikilia kama vile lina maana yoyote kwa maslahi ya nchi na watu wake. Wapo viongozi wakubwa wanadhani wana haki ya kuungwa mkono kwa kila wanachokiamini wao, kumbe wanachokipigania ni maslahi binafsi ndani ya utashi wa kujenga siasa za chuki nchini. Tufike mahali mtindo huu ukome ili kuipa nchi nafasi ya kusonga mbele kama wenzetu,” amesema.

Kwa mujibu wa taarifa, kamati maalum ilifanya kikao katikati ya wiki iliyopita mjini Zanzibar na kujadili uchaguzi wa marudio lakini idadi kubwa ya wajumbe walipinga uchaguzi huo.

Taarifa zinasema wajumbe 35 walipiga kura ya kukataa uchaguzi wa marudio, tisa waliridhia na wengine walikataa hata kupiga kura.

“Baadhi ya wajumbe waliamua kutoka nje ya ukumbi kwa kuchukizwa na chagizo za viongozi wakubwa wachache kulazimisha uchaguzi wa marudio,” amesema mwanamama kutoka Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Pamoja na CCM kushikilia kuendeshwa uchaguzi wa marudio Machi 20, bado wanavutana kwa kila kukicha kuendeleza vikao vya mikakati wakati dunia nzima inaishangaa Zanzibar kwa kujiingiza katika utaratibu wa kukandamiza maamuzi ya wananchi waliochagua kwa utulivu mpaka Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) kutangaza matokeo ya majimbo 31 ya urais na kukamilisha kazi ya kuhakiki kura za majimbo tisa mengine.

chanzo: zanzinet
Hizi hekaya za kusadikika ni sawa na kujidanganya kwamba usiku hauchi kamwe...!mtu anatunga kujifurahisha...hao ccm ambao wanagombea bila upinzani wana wasiwasi gani?..
 
Kwani hujui kuwa Zanzibarnet ni mtandao wa kipropaganda unaomilikiwa na CUF? Ni kama hapa kwetu Mwanahalisiforum
 
Kama hata wa ccm wameanza kususia huu uchaguzi itakuwa safi safi, maana huu upuuzi ukishiriki lazima nawe utakuwa mpuuzi tu, kama una akili timamu lazima ukae pembeni.
 
Haki ya mtu inaweza kuchezewa ila hutoweza kuiondoa. Haki hata kama haitotolewa kutokana na mifumo mibovu tuliyonayo, kweli hiyo hubaki milele.

Leo baadhi ya viongozi na CCM wanaojifanya miungu watu, na wenye kuwapangia na kutoa haki wakijiona ndiyo mwenye mamlaka, wanajidanganya bure.

Haki ya mtu ni hasili ya mtu katika kweli. Udanganyifu wanaofanya ili waendelea kuwa madarakani milele wakati wao kama wanadamu hawana huo umilele, ni ndoto za ajabu kutokea katika ulimwengu huu.

Sina shaka yoyote ile, ilicha ya vimbwanga vya wana CCM kila kukicha. Mungu aweza kuruhuru ovu, ili kutokana na ovu hilo, jema liibuke na watu wajifunze. Ila kamwe Mungu hawezi kuwa sehemu ya Uovu.

Kama kila kitu kina sababu yake, basi hata hili la mkwamo wa siasa Zanzibar litakuwa somo la kujifunza.
 
Huo mkwamo wa kisiasa uliotokea Zanzibar kutokana tu na wahafidhina wachache ndani ya CCM ambao wanaamini kuwa ni wao pekee waliopewa 'hati miliki' na Mwenyezi Mungu kuvitawala visiwa hivyo hadi mwisho wa dunia, hakika inaelekea Mungu ameamua kuingilia kati kwa kufanya hata wenyewe CCM wameanza kugawanyika baada ya kuona kama wataendelea kufumbia macho uovu huo wa viongozi wenzao wachache ndani ya chama chao inaweza kuja kusababisha kuitumbukiza nchi yetu kwenye machafuko makubwa.
 
Kwa sasa kuna hekaya nyingi sana za kuwaaminisha Watanzania wasahau dhuluma walizofanyiwa. Kusahau ni sehemu ya maumbile ya mwanadamu. Ila kumsahaulisha mtu kwa kumpora haki yake si jambo la kibinadamu. Sote kwa hasili yetu tumehesabiwa haki hiyo na yule aliyetuumba.

Mfano lisilo haki halitegemei ufahamu wa pekee kuelewa. Leo hii nenda kamzabe mtoto mchanga bila kosa na uone atakavyolia kwa uchungu na kusononeka.

Kama hakuna mtetezi wa kweli na haki, mwenye haki, yaani Mungu, huisimamia haki hiyo kwa wale waja wake walio onewa. Kama watawala wetu wana uwezo wa kujadili uhai wao na Mungu, wafanye na hilo.

Kama uwezo huo hawana, ni wakati wa kuwa na hofu ya Mungu na kutenda haki. La sivyo wanajidanganya bure. Viongozi hawa tunakutana na Misikitini siku za Ijumaa na Makanisani siku za jumamosi na jumapili. Swali ni hili; wanamwabudu Mungu gani???
 
Najuwa Maalim Seif yuko tayari kuapa huku akishika kitabu kitakatifu Quruan kwamba yeye ni mshindi halali.Swali ni Je Hajj Jecha yuko tayari.....???kama ndiyo atoke hadharani aseme halafu kiapo kifanyike kibanda maiti na mambo yaishe.
 
Tangu hawa jamaa washindwe kuonyesha kile wanachosimamia Bunge la Katiba, wala hawaaminiki kabisa.
 
Back
Top Bottom