Baada ya Zitto sasa ni Kikwete

Kuna kila dalili kwamba Mh. Lema ataomba Rais wetu mpendwa Mheshimiwa Dr. Jakaya Kikwete ampe majina ya wauza unga baada ya kusita kuyataja. Dr. Kikwete muda mrefu sana alisema tayari ana majina ya wauza unga mfukoni, lakini hadi leo hajawahi kuthubutu kuyataja.
Tunavyoona ni kwamba Mheshimiwa Rais hayupo tayari kuaibika kama alivyoaibika rafiki yake kipenzi Zitto Kabwe. Rais hatakuwa tayari kuaibishwa na AG mbele ya bunge pindi AG atakapokuwa anamjibu Mh. Lema. Ninavyofikiri na ndivyo itakavyokuwa ni kwamba AG atakuwa tayari kumjibu Mh. Lema kwamba rais yupo tayari kumkabidhi Kamanda Lema majina ya wauza unga ayataje.

Kama itakuwa hivyo basi, namuomba Mh. Lema atakapopokea list ya wauza unga, aikague list kwanza kuhakikisha jina la yule aliyekamatwa Hong Kong yupo kwenye list.
 
Sizani kama hawana hayo majina wanayo ila wanaogopana kutajana majina kikwete we sindo mwenye nchi sasa unaogapa nnn basi pengine unawafaam unaogopa kuwataja wasije wakakuaibisha nawe hebu taja hayo majina nnn
 
Nakumbuka mwaka 2006 akiwa Sumbawanga Kikwete alisema anawajua wauza unga,huu ni wakati sasa wa kumpatia Lema hayo majina ayataje hadharani.
 
Hivi majina yakijulikana nini huwa kinafuata?. Mwakyembe alitaja wahusika wa Richmond, Slaa alitaja wahusika kwenye List of Shame..... hata hao wenye Fedha chafu Uswis wakitajwa inakuaje?

au adhabu ya Fisadi Bongo ni kutajwa hadharani?
 
mybe na yye mwnywe msambazi mkuu hz safari za nje kila wakat zimezid kwa kwel so akitoa list yeye mwenyewe atatajwa na wale waliomo kwnye list
 


Ama kweli ndugu unachekesha, hilo hatauliza wala la ujambazi hawezi uliza, kwani litamdhuru yeye na wenzake wengi, hivyo ndivyo vitega uchumi wake na wafadhili wake.
 
Rais Kikwete ni msikivu licha ya udhaifu wake kiuongozi, bila shaka ni wakati sasa wa mh Lema kuomba hayo majina yawekwe hadharani.

​Njoo nyumbani kwangu Leo usiku nikupe hayo majina.
 
Naunga mkono kabisa asipowataja ana ushirika nao. Mwenye suruali ni lazima mikono yote miwili ijue kilichoko ndani ya mifuko yake maana suruali ni yake hivyo hata usalama wanajua
 

Mkuu sijakuelewa Lema alimuomba zitto majina gan hayo je ni yale zitto aliapa hana?
 
Ninyi sasa mnataka kumuuwa Rais kwa presha! Really, do you want it?
 
Nchi ya waoga ukiongozwa na waoga wenyewe, hakuna kitu chenye nguvu kama pesa ktk Nchi masikiniiii kama hii yenu japokuwa kwa mtizamo ni Nchi Tajiri
 
Naamini mh Rais wetu mpendwa Kikwete na serekali yake sikivu itasikiliza ombi hili la wananchi la kumkabidhi majina ya wauza ngwende mh Godbless Lema ili ayataje nje na ndani ya bunge ili hii ngonjera ya majina tunayo sasa ifikie tamati, na kuwataja watu wanaovuruga uchumi wa nchi hii hakuhitaji kinga ya kibunge wala kibali cha spika. Mh Rais naamini atafanya hivyo haraka kwa mamlaka aliyopewa na katiba yetu pendwa inayobadilishwa.
 
Lema ni kama nani mpaka kutaka kupatiwa majina yeye si karagosi tu na hanjifu ya wakubwa wa CHADEMA kujifutia mikono,Hata akipewa ili iweje.
 
Mnataka mkulu ataje majina ya vijana wake????????
 


Mbona unatokwa povu mkuu?
 

Naona unataka vita na Prince maana nasikia jina lake linaongoza kwenye hiyo list of Sembe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…