Baada ya Virungu, Serikali kuwalipa fidia wanafunzi UDOM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Baada ya Virungu, Serikali kuwalipa fidia wanafunzi UDOM

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Mr. Zero, Dec 23, 2010.

 1. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #1
  Dec 23, 2010
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,506
  Likes Received: 2,748
  Trophy Points: 280
  Serikali yasalimu masharti Udom Send to a friend Wednesday, 22 December 2010 19:49 0diggsdigg


  [​IMG] Waziri wa Mambo ya Ndani, Shamsi Vuai Nahodha.

  Habel Chidawali na Masoud Masasi, Dodoma
  HATIMAYE Serikali imesalimu amri kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom), baada ya kuridhia madai yao na kukubali kulipa gharama za uharibifu wa mali zao zilizotokana na vurugu kati yao na polisi.

  Hatua hiyo imefikiwa baada ya mawaziri wawili; Shukuru Kawambwa wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi na Waziri wa Mambo ya Ndani, Shamsi Vuai Nahodha kufika chuoni hapo juzi mchana kwa ndege ya kukodi kwa ajili ya kusuluhisha mgogoro huo uliodumu kwa siku mbili.

  Mawaziri hao wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma , Dk James Msekela na maafisa wengine wa Serikali mkoani Dodoma, walifika Udom saa 9 alasiri na kwenda moja kwa moja katika ukumbi kwa ajili ya kikao hicho kilichomalizika saa 8:00 usiku wa kuamkia jana.

  Wakati mawaziri hao wakifika chuoni hapo kwa msafara, viongozi wa serikali ya wanafunzi waliwasili kwa basi dogo wakitokea polisi walikokuwa wamewekwa rumande na baadaye kumlaki kiongozi wa Kitivo cha Sayansi ya Jamii aliyekuwa kinara wa mgomo huo, Leonard Singo.

  Baadaye Singo alikutana kwa faragha na Rais wa serikali ya wanachuo wa chuo hicho, Saimon Baisi na kuteta jambo kabla hawajaingia kwenye ukumbi wa mkutano.

  Baada ya kikao hicho kumalizika, Dk Kawambwa alienda kuzungumza na wanachuo na kuwaeleza kuwa Serikali imesikia kilio chao na sasa inaenda kuyafanyia kazi madai yao.

  Dk Kawambwa alizungumza na wanachuo hao saa 12:00 asubuhi wakati anajiandaa kwenda Uwanja wa Ndege Dodoma kwa ajili ya safari ya kurejea jijini Dar es Salaam.

  "Serikali imekubali matatizo yenu baada ya kuyaona kuwa ni ya msingi kwani hakuna watu wanaosoma bila kwenda field (mazoezi kwa vitendo)," alisema Dk Kawambwa na kuongeza:

  "Tunaorodhesha majina yenu ili wanafunzi wa mwaka wa pili waende field mapema iwezekanavyo na wale wa mwaka wa tatu waende kabla ya kumaliza chuo."

  Awali Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Idris Kikula alieleza kuwa Serikali inakwenda kutengeneza bajeti ya kuwalipa wanafunzi hao baada ya kuorodhesha majina yao na kuwasilishwa Tume ya Vyuo Vikuu na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu.

  Profesa Kikula aliwasihi wanafunzi hao kurejea madarasani ili waendelee na masomo kwa kuwa mgomo huo sasa umekwisha.

  Alisema kilichotokea hata chuo hicho kikashindwa kuwapeleka kwenye mafunzo kwa vitendo baadhi ya wanafunzi hao ni ufinyu wa bajeti ya serikali.

  Kabla kulitokea hali ya kutoelewana baada ya wanachuo hao kumkataa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Msekela katika mazungumzo hayo kwa madai kuwa yeye ni moja ya chanzo cha vurugu zilizotokea juzi.

  Baisi ambaye juzi alitangaza mgomo wa wanafunzi wote jana endapo Serikali isingekubali kuyatekeleza madai hayo alithibitisha kumalizika kwa mgomo huo.

  Hata hivyo, kiongozi huyo wa serikali ya wanafunzi alitahadharisha kuwa wanafunzi hao wamekubali kusitisha mgomo ili kuipa muda Serikali kutekeleza madai hayo, lakini hawatasita kuuitisha tena kama kauli hiyo ya Serikali ni danganya toto.

  “Tumeingia madarasani baada ya kuambiwa kuwa mambo yetu yanashughulikiwa. Kimsingi tulikubaliana na mawaziri hao waende kwa Waziri Mkuu na baada ya siku tatu watuletee majibu ya kutosha lini tutaanza mafunzo hayo kwa vitendo. Nasema wasipofanya hivyo bado tutaingia katika mgomo, tena mkubwa,” alisema Baisi.

  Juzi wanachuo wapatao 500 wa Kitivo cha Sayansi walifanya maandamano ambayo yalisababisha polisi kutumia nguvu ya kuwatawanya kwa mabomu ya machozi hali iliyosababisha baadhi yao kuumizwa na kukimbizwa katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma kwa matibabu.

  Lakini jana Waziri Kawambwa alisema pamoja na kutekeleza madai hayo, Serikali pia italipa gharama za mali za wanafunzi hao zilizopotea au kuharibika katika vurugu hizo.

  Wanafunzi wengi wamekuwa wakieleza kuwa wamepoteza simu na kompyuta ndogo (laptop).
   
 2. b

  bojuka Senior Member

  #2
  Dec 23, 2010
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 128
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  serikali ya jkndivyo inavyotaka haiendi haki isukumwe.
   
 3. PayGod

  PayGod JF-Expert Member

  #3
  Dec 23, 2010
  Joined: Mar 4, 2008
  Messages: 1,255
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Hili la kulipa mali za wanafunzi zilizoharibika kama DANGANYA TOTO VILE?, sijuhi kama litatekelezwa?
   
 4. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #4
  Dec 23, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,196
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Gharama ya ndege ya kukodi na marupurupu ya safari ya mawaziri wawili na msafara wao, gharama ya kuandaa operesheni ya FFU, mabomu ya machozi, fuel allowances (for the hopeless police) ni kiasi gani? Na wanfunzi walikuwa wanadai kiasi gani unawezakuta kiasi cha madai ya wanafunzi ni kido kuliko hela ilitumika kusuluhisha mgogoro huo.

  Watanzania hatuna mfano duniani.
   
 5. B

  Baba Tina Senior Member

  #5
  Dec 23, 2010
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 131
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  sio tu kilipa fidia tunataka polisi waliohusika kupora vifaa hivyo washughulikiwe ipasavyo. Hongereni wana UDOM huo uwe ni mwanzo tu sasa mmeanza kurejesha imani kwa jamii ya watanzania.
   
 6. Obuntu

  Obuntu JF-Expert Member

  #6
  Dec 23, 2010
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 512
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Siyo mali zilizoibiwa tu, hata fedha ya PT itatoka baada ya Miezi 6!
   
 7. STEIN

  STEIN JF-Expert Member

  #7
  Dec 23, 2010
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 1,764
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Si mara ya kwanza kwa serikali kukubali kuwalipa Wanafunzi maana Dar ni karibu miaka yote hajatia guu waziri yeyote wa JK, Lakini UDOM mawaziri wawili na fidia za Simu na Laptop, Ama kweli UDOM ni chuo cha CCM nimeamini.

  Hivi CCM iko makini kweli mbona sijasikia wakitoa tamko kuhusu mbunge lema kupigwa na polisi pamoja na wananchi wengine. Lakini kwa udom wako fasta.


  Peoples Power
   
 8. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #8
  Dec 23, 2010
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Huu ni uthibitisho kwamba UDOM ni chuo cha CCM.
  Tusubiri kutoka chuo cha ARDHI tuone.
   
 9. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #9
  Dec 23, 2010
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145


  Polisi wanapogeuka mgambo wa jiji la dsm dhidi ya wamachinga!!
   
 10. Kagemro

  Kagemro JF-Expert Member

  #10
  Dec 23, 2010
  Joined: Jan 11, 2010
  Messages: 465
  Likes Received: 50
  Trophy Points: 45
  Mkuu nakubaliana na hili.
   
 11. papason

  papason JF-Expert Member

  #11
  Dec 23, 2010
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 2,317
  Likes Received: 634
  Trophy Points: 280
  Hi kali ya funga mwaka sijawai kuisikia
   
 12. Mzalendo Mkuu

  Mzalendo Mkuu JF-Expert Member

  #12
  Dec 23, 2010
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 738
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Wakati wa uchaguzi UDOM walijipambanua kama WASIO NA UGOMVI na Serikali licha ya serikali kuwa na matatizo na vyuo vingine ikiwemo babalao UDSM. Mwanafunzi wa chuo unapaswa kuwa BUNGE LA WANA TAALUM (Professional's Parliament) maana theories za jinsi ya kutawala na kuongoza wananchi na nchi zinakuwa bado ziko hot. Pongeza serikali inafanya vema, lakini pia kemea inapofanya vibaya. :embarrassed:
   
 13. Mtego wa Noti

  Mtego wa Noti JF-Expert Member

  #13
  Dec 23, 2010
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 2,231
  Likes Received: 136
  Trophy Points: 160
  si walimchangia milion moja kikwete akachukue form ya kugombea urais? ngoja viwatokee puani sasa...
   
 14. Mzalendo Mkuu

  Mzalendo Mkuu JF-Expert Member

  #14
  Dec 23, 2010
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 738
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Sicheki!
   
 15. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #15
  Dec 23, 2010
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 589
  Trophy Points: 280
  kwahiyo watu kulipwa fidia imekukera eeh!
  Hao ardhi na wenyewe wakionesha msimamo kama vijana wa dom mambo yatawanyookea.
   
 16. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #16
  Dec 23, 2010
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 589
  Trophy Points: 280
  hauna lingine la kuandika inapoongelewa udom zaidi ya hilo.
   
 17. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #17
  Dec 23, 2010
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Political analysts wazuri wanajua kuwa CCM kwa muda mrefu imeshindwa kuwavutia wasomi ama kujiunga na chama hicho ama kuwapigia kura. Matokeo yake wamejikuta wanashbikiwa zaidi na watu wasiokuwa na elimu na baadaye kujiingiza kwenye uongozi wa juu wa chama na kuteuliwa kuwa viongozi serikalini. Hawa maamuma waliojazana katika ngazi zote za uongozi wa CCM ndiyo kikwazo kikubwa kwa nchi kupiga hatua ya kimaendeleo kutokana na mtazamo wao finyu wa kibinafsi na kujipendekeza kwa masilahi binafsi.

  Kitendo cha polisi kuwapiga mabomu wananchi na hasa wasomi wa vyuo vikuu siyo tu kinachochea chuki binafsi dhidi ya CCM na serikali yake bali pia kinaongeza uwezekano wa wasomi kutafuta vyama makini na kuvitumia kuipinga CCM within badala ya kujiunga na CCM. Hali hii haitishii tu usalama wa CCM kama chama in the future bali pia usalama na ustawi wa Taifa kutokana na viongozi maamuna ndani ya CCM kujiona miungu watu na wao pekee ndiyo wenye uwezo wa kutawala, ikifika mahali na Polisi, jeshi wakianza kuchukia matendo ya hawa maamuma wa CCM kuwatumia kwa masilahi yao binafsi badala ya yale ya Taifa basi tutakuwa katika wakati mgumu kama nchi.

  Kitendo cha kukubali madai ya wanafunzi na kuwalipa fidia huenda ni mpango maalum wa wasomi wachache ndani ya CCM kuvutia vijana wengi wasomi kujiunga na kuipenda CCM, kitu ambacho kitatishia ustawi wa viongozi maamuma ndani ya chama hicho. CCM inahitaji mapinduzi makubwa ya mfumo wake ndani na mfumo mzima wa jinsi kinavyoongoza nchi. Ni wakati sasa wa kuacha kuogopana na kuambiana ukweli kwa masilahi ya Taifa. Kuna watu bado wana imani na CCM si kwa sababu ni chama makini bali bado kina watu ambao kama watapewa nafasi watakibadili chama katika muundo wake wa sasa wa kimasilahi binafsi zaidi ya yale ya nchi. Ila kitendo cha kuwaridhia wanafunzi madai yao bado hizi zote ni mbio za sakafuni kama CCM haitaweka misingi mizuri ya uchumi na kuwawezesha wasomi hawahawa kujiajiri ama kuajiriwa badaa ya kumaliza masomo yao.
   
 18. Mla Mbivu

  Mla Mbivu JF-Expert Member

  #18
  Dec 23, 2010
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 221
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35

  Kama CCM inamiliki UDOM basi CCM wako juu ile mbaya, wakati CHADEMA hata ofisi ya chama ni kibanda.. What is the sense??
  Nawachukia mnaosema UDOM ni chuo cha CCM maana mnaipaisha hiyo CCM yenu balaaa, maana kile chuo ukubwa wake na buildings zilizopo ni UDSM mara 7.
   
 19. sbilingi

  sbilingi Senior Member

  #19
  Dec 23, 2010
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 144
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  yakujitakia mwenyewe, tamko la nini?????????
   
 20. sbilingi

  sbilingi Senior Member

  #20
  Dec 23, 2010
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 144
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  imeshindwa kuwavutia wakristo wanaochipukia na wachaga kujiunga na chama si wasomi bwana...
   
Loading...