Baada ya ushuhuda wa Diamond, jamaa yangu aapa kumkataza mkewe kwenda gym!

ichenjezya

JF-Expert Member
Sep 26, 2013
1,010
1,119
Habari wadau!

Baada ya kusikiliza mazungumzo aliyofanya msanii Diamond Platnum jana pale Wasafi Fm,na kufunguka kuwa mpenzi wake wa zamani Zari aliwahi ku cheat na Trainer wake, jamaa yangu flani anayekaa maeneo ya Mikocheni hapa mjini kanipigia simu leo kaniambia usiku wa jana amekosa kabisa usingizi maana mkewe nae ndio waleeee dizaini ya kina Zari uzungu mwingi kuwa na Trainer.

Ila tofauti yake mke wake yeye huwa anaenda gym kabisa nje ya nyumbani kwao na huko gym mkewe ana huyo trainer wake na mara si moja mkewe ameshawahi kumtaja kuwa trainer anampigia simu kuuliza mbona leo amechelewa mazoezi?

Mke wa jamaa si haba ukimuona mashalaah! Last time nilikuwa kwenye gari nikamuona anapiga zoezi la kukimbia ile njia ya kutoka Mlimani City kupitia chuo kwakweli moyo ulinishituka kuona mke wa jamaa yangu anakimbia huku akiacha mushikeli kwa wanaume mafisi wa maeneo yale.

Nilimpigiaga simu jamaa yangu nikasema nimemuona mtu kama shemeji maeneo ya Survey hapa anapiga zoezi akasema yes ni mwenyewe ilikua awe gym ila leo umeme umekatika kwahiyo ameamua apashe kidogo.

Basi ndio hivyo jamaa yangu analalamika sana anasema Diamond kamfungua akili, hawa ma trainer hawa sio wa kuwamini sana. Maana hii si mara ya kwanza kusikia mambo hizi, niliwahi sikia tena kuna jamaa alikuwa anamshutumu mkewe kuliwa na dereva aliyekuwa anamfundisha kuendesha gari.

Wanawake sijui huwa wanakosea wapi jamani. Basi ndio hivyo jamaa amesema yupo tayari kumkataza wife kwenda gym kuanzia leo!
 
list ni ndefu mkuu: ma-trainer,boss wake kazini, staff mwenzake, jamaa kwenye group lao la Kipaimara, muuza bucha, jamaa anayepaka rangi kucha, bodaboda, shamba boy, nk,nk. sasa kama unataka kufa kwa presha na vidonda vya tumbo jifanye unaweza kufuatilia
 
Ila Domo ka seng*,watu tushasahau ka walishadet ndo anakuja kuzungumza now.wakati mwenzie mambo ya ndoa yameiva.....

Roho mbaya hii
 
Kuna mazingira ukimweka karibu mwanamke lazima uumle tu, hata kama anamisimamo kama alshabab.....

Wengine hujikuta tayar washaliwa, na hakuwa na lengo la ku-cheat....

Juzi nilokuja Dar, kuna mke wa mtu nilikuja mpa mafunzo flani..,
Nilimkuta mwenyewe nyumbani, mumewe yuko kazini....

Ndani ya masaa mawili, mtu macho yamelegea, haelewi wala hasikii nachomfundisha.....
 
Mke wa jamaa si haba ukimuona mashalaah! Last time nilikuwa kwenye gari nikamuona anapiga zoezi la kukimbia ile njia ya kutoka Mlimani City kupitia chuo kwakweli moyo ulinishituka kuona mke wa jamaa yangu anakimbia huku akiacha mushikeli kwa wanaume mafisi wa maeneo yale.

Nilimpigiaga simu jamaa yangu nikasema nimemuona mtu kama shemeji maeneo ya Survey hapa anapiga zoezi akasema yes ni mwenyewe ilikua awe gym ila leo umeme umekatika kwahiyo ameamua apashe kidogo.

wewe na jamaa yako wote ni watoto!
 
Back
Top Bottom