Niko hapa Star
Park mji kasoro bahari (ingawa kulikuwa na matarajio ya Mzee Hashimu Rungwe kupitisha bahari ikielekea Dodoma lakini ndiyo hivyo tena...). Sasa jirani na meza 2 moja iko kulia na imejaa jamaa wanafurahia ushindi wa sunami... Nyingine iko kushoto ya jamaa wanaosononeka na kushindwa uchaguzi. Wote wanapiga maji vibaya wengine huku wakicheza, wengine huku wananungunika. Hata hivyo hawa walioshindwa inaonekana wako vyema kifedha kwani vinywaji vimejaa plus mbuzi choma, ndizi, mara kongoro mara mkia etc... Wenzao upande wa pili meza imeanza kuwa na chupa tupu na huduma imedorora. Jamaa mmoja wa meza iliyodorora akaona isiwe tabu akaja meza ya pili (naona wanajuana) kimbembe jamaa kuomba kinywaji jamaa akamnongoneza mhudumu, daah jamaa si akaletewa chupa kubwa ya maji ya Uhai??