Baada ya TLS hawa nao wafuate.....

UNDENIABLE

JF-Expert Member
Feb 26, 2013
2,326
1,314
TLS tayari. Hao ni mawakili. Lakini Tanzania imebarikiwa kila aina ya taaluma.

Sasa nadhani ni muda muafaka kabisa taaluma zingine zianze kufuata nyayo za TLS. Kuna wahasibu/wakaguzi, kuna madaktari, kuna mainjinia, kuna walimu kwa ujumla wao, kuna maIT kwa mapana yao, na kadhalika.

Kwa muda sasa kuna malalamiko makubwa kuwa wasomi hawaisaidii nchi hii ipasavyo. Sababu inayotolewa ni kuwa serikali haizingatii ushauri wa kitaalamu (wasomi) toka kwa wasomi wake.

Wengine wanaenda mbali zaidi na kusema. Usomi wa wasomi wa Tanzania ni wa past papers tu. Yaani kusoma Q and A mwanzo mwisho then unatusua pepa. Kwa hio ni suaa la copy and paste tu. Hakuna original thinking ability katika elimu ya watanzania. Wanazidi kusema kuwa hata mwalimu naye anatoa maswali kwa ku copy na ku paste. Wengi wao hawatungi maswali yao 'original' bali wana edit tu maswali yaliyowahi kuulizwa. Na hivyo kufanya elimu ya bongo kuwa less competitive.

Sasa. Let's crack the code. Jumuiya zingine za kitaaluma zifuate mwenendo wa TLS ili tutengeneze balance ya kitaaluma katika nchi yetu. Imagine, huku TLS, kule Mainjinia, kule wahasibu, nk. What a combination katika kusemea masuala ya Tanzania.

Nasema hivi kwa sababu am sure TLS itaanza kusikika vema Tanzania ikiwa chini TL. Nakumbuka hata wakati wa mchakato wa katiba mpya walikuwa kimya kama vile wamenyeshewa na mvua. Sasa nadhani wataanza kuamka rasmi.

Nawatakia kila la kheri!
 
Back
Top Bottom