Baada ya South Africa kushinda Kesi Huko ICJ nchi za Kiarabu zaanza kujipendekeza kwa Palestine, zakutana UN kujadili Hukumu!

Algeria imeomba baraza la Usalama la UN likutane Jumatano kujadili Hukumu ya ICJ dhidi ya Israel

Nazo nchi zote za Kiarabu Huko UN zimekutana faragha kujadili na kuipongeza Palestine

Source Al jazeera news
Ile kesi imeamriwa kihuni!! Wasio na akili wanashangilia.

Kule Palestina Wananchi wanalalamika ICJ kushindwa kuamuru Cease Fire..... So wanaendelea kutandikwa kwa uangalifu tu!! 🤣🤣
 
Algeria imeomba baraza la Usalama la UN likutane Jumatano kujadili Hukumu ya ICJ dhidi ya Israel

Nazo nchi zote za Kiarabu Huko UN zimekutana faragha kujadili na kuipongeza Palestine

Source Al jazeera news

Kesi gani wameshinda?. Punguza kimbelembele. Unaijua maana ya provisional measures?
 
Algeria imeomba baraza la Usalama la UN likutane Jumatano kujadili Hukumu ya ICJ dhidi ya Israel

Nazo nchi zote za Kiarabu Huko UN zimekutana faragha kujadili na kuipongeza Palestine

Source Al jazeera news

John, hiyo habari ya kusema Afrika Kusini imeshinda kesi, umeiokota wapi? Afrika Kusini inawezaje kushinda kesi ambayo uchunguzi haujafanyika, wala kesi yenyewe ya msingi haijaanza kusikilizwa?

Afrika Kusini imepeleka tuhuma mahakamani. Halafu ikaweka ombi la dharula la kuitaka Mahakama itoa amri ya kusimamisha vita.

Israel ikapeleka pingamizi la awali la kudai tuhuma za Afrika Kusini hazina msingi, ikaomba mahakama itumbilie mbali madai ya Afrika Kusini.

Uamuzi wa Mahakama Kuhusiana na Maombi ya awali:

1) mahakama imekataa ombi la awali la Afrika Kusini la kuitaka mahakama itoe amri ya kusimamisha vita. Badala yake imetoa angalizo kwa Israel kuwa inapoendelea na vita yake dhidi Hamas, ichukue tahadhari na kujizuia kutenda makosa ambayo yataweza kutafsiriwa kuwa inafanya genocide. Na ikaikumbusha Israel mambo hayo ya kuzingatia.

2) Kuhusu ombi la Israel la kuitaka mahakama hiyo itupilie mbali kesi hiyo, mahakama imegoma, na kusema kuwa kuna baadhi ya mambo ambayo Afrika Kusini imesema kuwa Israel imeyatenda, kama yakithibitika, yanaweza kuangukia kwenye makosa ya uhalifu wa kivita.

Hii ina maana kuwa sahizi ndiyo uchunguzi utaanza ili kuthibitisha au kuyakataa madai ya Afrika Kusini. Na historia inaonesha kuwa kesi kama hizo, mpaka kufikia hukumu ya mwisho, huchukua si chini ya miaka 10.

Kwa hiyo sasa hivi vita itaendelea. Kusimamisha vita kupitia mahakama, imeshindikana.
 
Kwa hiyo sasa hivi vita itaendelea. Kusimamisha vita kupitoa mahakama, imeshindikana.
Netanyahu: Ushindi wa SA ni wa uonezi
 
Waarabu hawapendani

Kuna unafiki mkubwa, na kutoaminiani miongoni mwa Waarabu. Ndiyo maana misaada mikubwa ya kuwasaidia wapalestina huwa inatolewa na nchi za Ulaya, Marekani na Israel; siyo nchi za kiarabu. Misaada ya makombora kwa vikundi vyote vya kigaidi inatolewa na Iran.

Wakati hii vita inaendelea, kiuhalisia kuna mataifa ya kiarabu yanashangilia kwa siri.

Urafiki wa Israel na nchi za Saud Arabia, Misri na UAE, ni kwa sababu Israel ndiyo mbabe pekee anayeweza kumdhibiti adui yao mkuu, Iran. Nchi zote zenye Wasuni wengi au watawala ni Wasuni, hawaiaki kabisa Iran ambayo hutengeneza makundi ya kigaidi katika nchi zenye watawala wasuni ili waziangushe serikali zao. Na serikali za nchi hizo automatically huichukia Iran.
 
Baada ya taarifa hiyo ya mahakama, karibu wapalestina 200 wameuawa huko ghaza.
 
Back
Top Bottom