Baada ya Serukamba kumkaba Mwakyembe, sasa ni Lowasa vs Membe....... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Baada ya Serukamba kumkaba Mwakyembe, sasa ni Lowasa vs Membe.......

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwana Mpotevu, Jun 6, 2012.

 1. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #1
  Jun 6, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,295
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180

  Waandishi Wetu

  KAMATI ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama imembana Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe ikimtaka aeleze ni kwa nini vitabu vya bajeti ya wizara hiyo vimechelewa kufikia wajumbe wa kamati hiyo.

  Hatua ya kamati hiyo inayoongozwa na Mbunge wa Monduli (CCM), Edward Lowassa imekuja siku chache baada ya baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Miundombinu kuikataa Bajeti ya Wizara ya Uchukuzi, ikihoji sababu za bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka 2011/12 kutekelezwa kwa kiwango cha asilimia 40.

  Juzi jioni, taarifa zilizopatikana kutoka kwenye kikao cha kamati hiyo ya mambo ya nje zilisema wajumbe walichukizwa na hatua ya wizara hiyo kuchelewa kuwapatia vitabu kwa mujibu wa taratibu.Taarifa hizo zilisema, Lowassa alihoji sababu za msingi za wao kuchelewa kupata vitabu hivyo siku mbili kabla na badala yake kuvipata siku ya mkutano.

  Mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo aliliambia gazeti hili kwamba wajumbe waligomea bajeti hiyo kutokana na kuchukizwa na kitendo hicho cha kucheleweshwa kwa vitabu na kutokuonyesha madeni ya wizara.

  Pia wajumbe hao walichukizwa na hatua ya ujumbe huo wa wizara hiyo kuchelewa kufika katika kikao hicho.

  Hata hivyo, Lowassa alipotakiwa kutoa ufafanuzi juu ya suala hilo alikataa na kumtaka mwandishi athibitishe taarifa hizo kwa mtu aliyezitoa... “Siwezi kusema lolote kuhusu hilo na wala mimi sijui. Mwulize aliyekupa taarifa, yeye ana maelezo zaidi lakini siyo mimi.”

  Chanzo hicho cha habari kilisema kamati hiyo pia ilihoji kuhusu uwasilishaji wa michango ya wanachama wa mifuko ya hifadhi ya jamii, ikiwemo NSSF.

  Hata hivyo, baadaye kamati ilipitisha bajeti hiyo ya Sh80 bilioni na kumtaka Waziri Membe na ujumbe wake kuwasilisha mapema vitabu vyao katika siku zijazo ili wajumbe waweze kuhoji utekelezaji wa mikakati ya Serikali.

  Source: Mwananchi (Leo)

  MY TAKE: Bila ubishi, kambi ya EL ambayo inaongoza kamati ina malengo ya kuwafanyia kweli wale wote ambao ni wapinzani wao kisiasa. Bado Sitta zamu yake inakuja.
   
 2. Viol

  Viol JF-Expert Member

  #2
  Jun 6, 2012
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 18,982
  Likes Received: 1,087
  Trophy Points: 280
  magazeti yanakuza tu taarifa,hiyo ishu itaisha tu kinafki
   
 3. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #3
  Jun 6, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,197
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Mbona unasema wameigomea Huku wameipitisha?
   
 4. N

  Njoka Ereguu JF-Expert Member

  #4
  Jun 6, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 822
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 35
  Taarifa hii kama haiendani na hitimisho, taarifa inasema kamati iligomea bajeti kwa kuwa vitabu vilichelewa na kwenye hitimisho kamati ilipitisha bajeti ya Bil. 80.

  Mwandishi kama vile alikosa cha kuandika au alienda kwenye hicho kikao akalala hivyo hakusikia kilichoendelea kutoka mwanzo hadi mwishi (alisikia ufunguzi wa kikao na kufungwa kwa kikao tu nadhani).
   
 5. TUNTEMEKE

  TUNTEMEKE JF-Expert Member

  #5
  Jun 6, 2012
  Joined: Jun 15, 2009
  Messages: 4,582
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Ni kweli mwanzo mwingine na hitimisho jingine Kabisa

  Ni hivi,wamerudishwa mpaka j4 ijayo hakuna kilichoongelewa juzi.

  Randama Yao imechelewa,hawajaonyesha madeni wanayodaiwa na utekelezaji wa bajeti 2011/2012 hawajaonyesha.

  Hivyo waliambiwa wakajipange upya na Membe alikubali
   
 6. kookolikoo

  kookolikoo JF-Expert Member

  #6
  Jun 6, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 2,537
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  afadhali angesema 'nusura waigomee!'
   
 7. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #7
  Jun 6, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,798
  Likes Received: 3,883
  Trophy Points: 280
  hii thread ulikuwa ni udaku tu wala usitilie maanani!1
   
 8. Vin Diesel

  Vin Diesel JF Gold Member

  #8
  Jun 6, 2012
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 8,403
  Likes Received: 737
  Trophy Points: 280
  Mwananchi wameanza kuandika ki-udaku udaku......
   
 9. Yummy

  Yummy JF-Expert Member

  #9
  Jun 6, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 1,801
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hivi ni gazeti gani la kuaminika siku hizi???
   
 10. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #10
  Jun 6, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  kiswahili kinaonekana kuanza kuwa na matatizo hivi kukataliwa na kukubali ni maneno sawa? jamaa kiswahili kinapoteza mvuto wake kabisa
   
 11. TaiJike

  TaiJike JF-Expert Member

  #11
  Jun 6, 2012
  Joined: Dec 14, 2011
  Messages: 1,475
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 160
  Tatizo la waandishi wetu wa siku hawaandiki habari za kiuchunguzi wanasubiri taarifa kwa simu na kisha kuchapa. kaaaaazzzi kweli.
   
 12. r

  ralphjn Senior Member

  #12
  Jun 6, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 169
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mwanahalisi na Raia mwema.

   
 13. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #13
  Jun 6, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,375
  Likes Received: 19,621
  Trophy Points: 280
  vitabu kuchelewa nayo imeshakuwa hoja? duh kweli visasi havina macho
   
 14. Yummy

  Yummy JF-Expert Member

  #14
  Jun 6, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 1,801
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Tena kubwa ya kujadilika......yaaani we acha tuuu
   
 15. andishile

  andishile JF-Expert Member

  #15
  Jun 6, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 1,430
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  habari imekuzwa,mbona sioni cha ajabu hapo,kama walichelewesha vitabu na wakaulizwa sababu,hakuna ubaya.mbona watu mnataka kukuza makundi ya viongozi bila sababu?
   
 16. m

  mlagha Member

  #16
  Jun 6, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Unajua sasa nimeona huyu Waziri Membe anawindwa kwa udi na Uvumba kwa sababu suala la vitabu kucheleweshwa limewekwa kama vile Wizara ndo ilichelewa kuwapelekea vitabu. Wakati watu wa Bunge wanasema vitabu vilifika Ijumaa ambayo ni three days before Monday. Siyo jukumu la Wizara kuwagawiya Wabunge bali ofisi za Bunge.


  Jambo lingine ni kama alivyosema TAIJike na Santivuga Mwananchi imeondoka kkatika magazeti ya kuaminika. Istoshe Mwananchi wana kesi nyingine ya kumwandika Membe vibaya huko nyumba kwa hiyo wangependa kila taarifa mbaya kwa membe iandikwe. Lakini wangetafuta taarifa kuliko kuandika madudu ya kusema kamati imekataa kupitisha bajeti ya Mambo ya Nje. Alafu mwisho anasema bajeti ilipita. uhariri gani huo.
   
Loading...