Baada ya Road licence SUMATRA nako kuangaliwe

mycall

JF-Expert Member
Dec 17, 2014
849
500
Huwa sioni sababu ya Sumatra kushughurika na ukaguzi wa vyombo vya usafiri wa nchi kavu, wakati kazi hiyohiyo inafanywa na Polisi wa usalama barabarani/Trafiki. Huku ni kuwaongezea gharama wamiliki wa magari bila sababu.
Kwanini SUMATRA wasi deal na vyombo vya majini pamoja na magari ya Abiria tu na Magari ya mizigo yakaachiwa Trafiki na Wakara wa vipimo na Mizani?
Hiyo ada ya kila mwaka ya Sumatra kwa magari ya mizigo kwa mini isifutwe, Mimi huwa sioni kabisa umhimu wake, nikuongezeana gharama bila sababu.Gari huendelea kudaiwa hata kama limesimama ! kama ivyokuwa Load licence. Ukichelewa kulipa fine ni sh. 250000 wakati ada halisi ni chini ya sh. 100000.
Hebu tujadiri hili jamani.

cc. Bashe
Msukuma
Msigwa
Lissu
Serukamba
 

kinjumbi one

JF-Expert Member
May 27, 2015
1,645
2,000
Sasa hao wa magari ya abiria wao huwa awakaguliwi na traffic? Au wao ndo hupenda kuongezewa gharama? Hoja yako ni ya msingi ila umeiwasilisha ki ubinafsi zaidi. Sumatra washughurikie vyombo vya majini tu. Huku nchi kavu traffic, veco, mizani wanatosha. Hakuna haja ya kuongezeana ukali wa maisha bila sababu.
 

Joseverest

Verified Member
Sep 25, 2013
42,857
2,000
Ndiyo ifutwe upande wa vyombo vya nchi kavu, maana hata yenyewe ada hudaiwa hata kama chombo kimesimama, the same as Load licence fee.
sasa taasisi ipi itasimamia usafiri wa ardhini na majini?
 

mycall

JF-Expert Member
Dec 17, 2014
849
500
sasa taasisi ipi itasimamia usafiri wa ardhini na majini?
Nimesema upande wa nchi kavu wasihusike kwa kuwa kuna Trafiki na wakara wa vipimo na mizani. Kwa maana hiyo ada hiyo isitozwe. Wabaki na vyombo vya majini tu.
 

imhotep

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
22,573
2,000
SUMATRA wasi deal na vyombo vya majini pamoja na magari ya Abiria tu na Magari ya mizigo yakaachiwa
Kwanza fanya uchunguzi kijana/msichana.kabla ya..ooh hivi...oh vilee..hata magari ya mizigo pia yanalipa SUMATRA.
 

mycall

JF-Expert Member
Dec 17, 2014
849
500
Kwanza fanya uchunguzi kijana/msichana.kabla ya..ooh hivi...oh vilee..hata magari ya mizigo pia yanalipa SUMATRA.
Magari ya mizigo yanalipa na Mimi mmoja wa wamiriki wa vyombo hivyo. Tena ukichelewa tarehe ya kulipa fine ni sh. 250000. Nenda Dodoma kwenye mzani wa NARA kuna beria,kila siku Sumatra wapo wanakaguwa na kutoza magari yaendayo mikoa ya kati na kanda ya ziwa
 

bigcell

JF-Expert Member
Oct 6, 2010
220
225
Hiyo itakuwa badae ngoja kwanza tumalizie huu mwezi tusidaiwe tena Road Licence then tujadili Sumatra Sawa! Sawa?!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom