Baada ya Rais Magufuli CCM haiwezi kusimama tena

Baada ya Rais Magufuli CCM haiwezi kusimama tena

Labda 2060 ndio wanaweza toka madarakani nayonilabda. chama kikuu chaupinzani kinaweka makapi yaCCM kugombea urais ni ndoto kuiondoa CCM kwa aina ii yaupinzani.
 
Siamini kama CCM ina vijana wenye mvuto kwa sasa.Siamini kama inaweza kuitisha Mkutano wa hiayi ikapata wasikilizaji wa maana.Nadhani chama kimechokwa maana hakuna jipya la kujivunia.Kama vile walivyoogopa kuwatangaza wagombea wao kupitia jina la chama ndivyo itakavyokuwa kipindi kijacho.
Wapinzani bado wanakubalika na kama uchaguzi huru na haki ukiitishwa huenda CCM ikageuka chama cha upinzani.Ukitaka kuhakikisha mikutano ya hadhara iitishwe halafu uone mwitikio.Kwa sasa watu wamechoka zaidi kuliko ilivyokuwa miaka miwili iliyopita.
kuelekea October 2015 yalisemwa mengi kuliko haya uliyoandika hapa, na kilichotokea ni kama ya Hilary Clinton na Trump.
 
Nduguzanguni, ukweli mchungu lakini ni lazima usemwe kwa uwazi kabisa.

JPM alikua ni mwanaCCM pekee ambaye kila Mtanzania alitegemea kupelekwa katika nchi ahadi baada ya kupewa dhamana ya kuliongoza taifa, pamoja na hayo mategemeo yote lakini hali imegeuka na watu wameonekana kukata tamaa kabisa, hawama hamu na utawala wake kabisa kwa sasa.

Pamoja na hayo yote ni ukweli usipingika kabisa jina ambalo likikua likivuma pasipo kujali itikadi ya mtu miaka ya nyuma lilikua jina la mzee wetu marehem SITTA(R.I.P), naye baada ya bunge maalumu la katiba jina likanywea kabisa likawa halisikiki tena. Mtu ambaye alionekana ni wa tofauti kabisa na wengine alikua ni mh JPM kutoka na utendaji wake serikalini kila awamu alipokua waziri. Hii na ndio maana alikua akikubalika sana na watu wote.

Rais JPM aliwakuna wengi kutokana na kuwajibika vizuri katika maeneo yake ya kazi, lakini mpaka sasa hakuna aliyevunja rekodi yake akiwa kama waziri, hakuna cha waziri wala Naibu waziri aliyefikia hata robo ya utendaji wake japo kiti cha Urais kinaonekana kua ni kitu kiingine kabisa kulinganisha na alikopita.

MwanaCCM kijana kwa sasa akiwa kama waziri au Naibu mwenye mapenzi na watanzania wote bila kubagua itikadi zao hajapatikana na hawezi kupatikana tena baada ya JPM, Wapo wanaojitutumua lakini wamejawa sifa,kuidai, mihemko,itikadi,kujikomba na kuijonesha kwa wananchi lakini naamini hakuna wa kumfikia JPM enzi hizo.Narudia kusema tena hakuna waziri wa kufanana nae, hakuna waziri ambaye anaweza kuleta ubunifu ndani ya wizara na watu wakaziona tofauti zaidi ya sifa tu.

Watu wanashindwa kuelewa kua awali JPM alipendwa sana kama mtu aliyeonekana kujali jamii zote, alikua ni mtu wa site muda wote,alikua ni waziri mbunifu kwa kila mahali alipopelekwa alionesha uhai wake ndani ya wizara.Alionesha kipaji kikubwa sana kwenye kuhifadhi takwimu za ripoti mbali mbali kichwani bila hata kukosea.

Cha ajabu ni kwamba JMP alikua ni Mbishi sana kwenye mambo ambayo alikua anaona hayana manufaa kwa umma, niliwahi kusikia alikua ni waziri ambaye alikua anao uwezo wa kumgomea hata bosi wake kipindi hicho akiona mambo yanayofanywa hayako sawa, JPM alikua hata akiigomea bajeti hata pale alipoona ni ndogo kwenye wizara yake,kuna siku wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu uliopita 2015 niliwahi kumsikia aliyekua Rais wakati huo Mh Jakaya Kikwete akisema kua "Magufuli ni mtu mbunifu sana,"
Je,Kwa sasa ni waziri gani mwenye Ubavu huo? Narudia kusema hakuna.

Kwahiyo naweza kuhitimisha kwa kusema akitoka JPM sasa, CCM haitokaa ipate tena wa aina yake. Sasa utakua ni wakati mwafaka wa kuangalia watu wa aina yake upande wa pili ambapo wanaonekana kua ni vijana wabushi,wenye kuhoji,wasioitikia tu.Watu aina ya Tundu Lissu,John Mnyika na John Heche na Godbless Lema mimi nawaona kama hazina kubwa sana kwa taifa na sioni tofauti kati na misimamo ya JPM enzi hizo, hawa jamaa siwafananishi na yeyote kule CCM hata kidogo.

Hatujinyongi hatunywi sumuu DP Mbele kwa mbele, hatujinyongi hatunywi sumuu DP mbele kwa mbelee, uhuuu mzukaa aaah napanda juu ya Meza, hatujinyongi hatunywi sumuu DP mbele kwa mbelee ash wajameni
 
Unajua mbowe hawakufikiri mbele kuna nn CCM wanaakili kuliko wao walimdhalilisha sana lowasa tena sana lkn mungu akawaonyesha kuwa huyo atakuja hukohuko na mtampamba lkn watanzania washawajua kuwa wako kipesa zaidi .... Tundu lisu hakulitambua hilo yeye alikuwa serious lkn wapigaji walimzunguuka.... Wamuulize john mnyika yuko wapi Leo hii kimyaa sana
 
yuko balozi MAHIGA

hata DOGO BASHE YUKO VIZURI

ila kuitoa ccm madarakani si kazi ndogo, labda wao na wenye nchi waamue, tena kwa mpango maalum

over
 
Back
Top Bottom