Baada ya Rais Magufuli CCM haiwezi kusimama tena

MAHANJU

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2014
Posts
5,255
Reaction score
8,027
Nduguzanguni, ukweli mchungu lakini ni lazima usemwe kwa uwazi kabisa.

JPM alikua ni mwanaCCM pekee ambaye kila Mtanzania alitegemea kupelekwa katika nchi ahadi baada ya kupewa dhamana ya kuliongoza taifa, pamoja na hayo mategemeo yote lakini hali imegeuka na watu wameonekana kukata tamaa kabisa, hawama hamu na utawala wake kabisa kwa sasa.

Pamoja na hayo yote ni ukweli usipingika kabisa jina ambalo likikua likivuma pasipo kujali itikadi ya mtu miaka ya nyuma lilikua jina la mzee wetu marehem SITTA(R.I.P), naye baada ya bunge maalumu la katiba jina likanywea kabisa likawa halisikiki tena. Mtu ambaye alionekana ni wa tofauti kabisa na wengine alikua ni mh JPM kutoka na utendaji wake serikalini kila awamu alipokua waziri. Hii na ndio maana alikua akikubalika sana na watu wote.

Rais JPM aliwakuna wengi kutokana na kuwajibika vizuri katika maeneo yake ya kazi, lakini mpaka sasa hakuna aliyevunja rekodi yake akiwa kama waziri, hakuna cha waziri wala Naibu waziri aliyefikia hata robo ya utendaji wake japo kiti cha Urais kinaonekana kua ni kitu kiingine kabisa kulinganisha na alikopita.

MwanaCCM kijana kwa sasa akiwa kama waziri au Naibu mwenye mapenzi na watanzania wote bila kubagua itikadi zao hajapatikana na hawezi kupatikana tena baada ya JPM, Wapo wanaojitutumua lakini wamejawa sifa,kuidai, mihemko,itikadi,kujikomba na kuijonesha kwa wananchi lakini naamini hakuna wa kumfikia JPM enzi hizo.Narudia kusema tena hakuna waziri wa kufanana nae, hakuna waziri ambaye anaweza kuleta ubunifu ndani ya wizara na watu wakaziona tofauti zaidi ya sifa tu.

Watu wanashindwa kuelewa kua awali JPM alipendwa sana kama mtu aliyeonekana kujali jamii zote, alikua ni mtu wa site muda wote,alikua ni waziri mbunifu kwa kila mahali alipopelekwa alionesha uhai wake ndani ya wizara.Alionesha kipaji kikubwa sana kwenye kuhifadhi takwimu za ripoti mbali mbali kichwani bila hata kukosea.

Cha ajabu ni kwamba JMP alikua ni Mbishi sana kwenye mambo ambayo alikua anaona hayana manufaa kwa umma, niliwahi kusikia alikua ni waziri ambaye alikua anao uwezo wa kumgomea hata bosi wake kipindi hicho akiona mambo yanayofanywa hayako sawa, JPM alikua hata akiigomea bajeti hata pale alipoona ni ndogo kwenye wizara yake,kuna siku wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu uliopita 2015 niliwahi kumsikia aliyekua Rais wakati huo Mh Jakaya Kikwete akisema kua "Magufuli ni mtu mbunifu sana,"
Je,Kwa sasa ni waziri gani mwenye Ubavu huo? Narudia kusema hakuna.

Kwahiyo naweza kuhitimisha kwa kusema akitoka JPM sasa, CCM haitokaa ipate tena wa aina yake. Sasa utakua ni wakati mwafaka wa kuangalia watu wa aina yake upande wa pili ambapo wanaonekana kua ni vijana wabushi,wenye kuhoji,wasioitikia tu.Watu aina ya Tundu Lissu,John Mnyika na John Heche na Godbless Lema mimi nawaona kama hazina kubwa sana kwa taifa na sioni tofauti kati na misimamo ya JPM enzi hizo, hawa jamaa siwafananishi na yeyote kule CCM hata kidogo.
 
CCM ina hazina kubwa sana, ccm hakijazuka tu, huwezi kuipima CcM na akina Lisu, Mnyika, Heche.

Itizame CCM tangu 1977 ilipozaliwa ilikuwa na akina Sita, Msekwa, Sapi Mkwawa, Moses Nnawiye, Makamba, Mwakanjuki, Karume, Mzindakaya, Natepe, Mkapa, Nyerere, Kawawa, etc ambao hawapo na bado ipo stable.

Wasiwasi wangu baada ya akina Mnyika, Mbowe, etc wakitoka nani atafuata? tangu 1992 vyama vingi kuingia bado viongozi wa vyama hivi bado wale wale Lipumba, Mbowe, Maalim Seifu, Baregu, Mbatia, Hashimu Rungwe, etc inawezekana kabisa baadaya ya 2020 hivi vyama vitakufa kabisa.
 
CCM ipo Madarakani kwasababu ya Dola na siyo vinginevyo, na hii ni hofu iliyojengwa makusudi kabisa kuwa upinzani ukikamata Mamlaka utakuja na utawala wake hivyo maafisa wengi wataondolewa, sumu hii imekuwa ikitafuna upinzani kwa muda mrefu sana.

ili kutoka kwenye kikwazo hicho lazima elimu ya uelewa itolewe kwa hawa ndugu zetu pia, kuwa hakuna chama kitakachokuja na maafisa wake badala yake ni kulifanya jeshi la police kuwa independent na kufanya kazi zake kwa weledi katika mazingira mazuri yanayofanana na hadhi yao kwenye jamii, kikwazo hiki ni kikubwa sana kutokana na mindset iliyojengwa kwa muda mrefu.
 
Hao wazee muda wao umeisha, wanaondoka na CCM yao. Hawa wa sasa maslahi mbele! Wa million 10 hawa?
 
CCM ipo Madarakani kwasababu ya Dola na siyo vinginevyo, na hii ni hofu iliyojengwa makusudi kabisa kuwa upinzani ukikamata Mamlaka utakuja na utawala wake hivyo maafisa wengi wataondolewa, sumu hii imekuwa ikitafuna upinzani kwa muda mrefu sana.

ili kutoka kwenye kikwazo hicho lazima elimu ya uelewa itolewe kwa hawa ndugu zetu pia, kuwa hakuna chama kitakachokuja na maafisa wake badala yake ni kulifanya jeshi la police kuwa independent na kufanya kazi zake kwa weledi katika mazingira mazuri yanayofanana na hadhi yao kwenye jamii, kikwazo hiki ni kikubwa sana kutokana na mindset iliyojengwa kwa muda mrefu.
Kichekesho kipo hivi, wakati wa uchaguzi wa 2015 - babu Duni alihama chama kwa ajili ya madaraka, na wengine wengi tu, matokeo yake baada tu ya uchaguzi kila mtu alianza kurudi alikotoka.

Hili suala ni la kiusalama sana, kuongoza nchi hakuhitaji majaribio, wapinzani bado wanahitaji kukomaa.

Mara 1000 hicho kikwazo kiendelee kuwepo.
 
Naomba msisahau na hili pia kuwa.
Tangia Tanganyika na hatimae ikaja Tanzania tumekuwa tukitekeleza ilani ya ccm.Hatujawahi kutekeleza ilani ya Tanzania,sasa kuna kila sababu kuanza kutoa elimu ya uraia ili watanzania wadai kutekelezwa kwa ilani ya nchi yao.Chama kama chama kimeshindwa.over
 
CCM ina hazina kubwa sana, ccm hakijazuka tu, huwezi kuipima CcM na akina Lisu, Mnyika, Heche.

Itizame CCM tangu 1977 ilipozaliwa ilikuwa na akina Sita, Msekwa, Sapi Mkwawa, Moses Nnawiye, Makamba, Mwakanjuki, Karume, Mzindakaya, Natepe, Mkapa, Nyerere, Kawawa, etc ambao hawapo na bado ipo stable.

Wasiwasi wangu baada ya akina Mnyika, Mbowe, etc wakitoka nani atafuata? tangu 1992 vyama vingi kuingia bado viongozi wa vyama hivi bado wale wale Lipumba, Mbowe, Maalim Seifu, Baregu, Mbatia, Hashimu Rungwe, etc inawezekana kabisa baadaya ya 2020 hivi vyama vitakufa kabisa.

ccm hazina yake ni dola. Kila wakati wa uchaguzi, hata wa meya tu askari wanajipanga na selaha mzito zito kuliko vikosi vya marekani huko Afghanistan.
 
Kitakachoua kabisa hiki chama changu pendwa cha Mapinduzi ni mambo matatu:
1. Rushwa na kukumbatia rushwa,
2. Uoga na unafiki wa wanachama wake,
3. Sera za ovyo, za uongo na zisizotekelezeka (Nyingine zilianza kutekelezwa miaka 50 iliyopita lakini hazijawahi kuonyesha mafanikio yoyote).

Msema kweli ni Mpenzi wa Mungu.
 
Katumwa na akili yake we unatakaje? Mkiambiwa ukweli eti katumwa acha msuba wewe
 
Tatizo sio CCM, tatizo ni kupata mbadala wa CCM. !
 
Hizo sifa ulizompa wala hastahili na watanzania wengi mlidanganyika na sifa za aina hii.Huyu bwana ukimchunguza vizuri huwezi na wala usingempa kura yako.

Watanzania ni wavivu wa kusoma na kutafuta habari ndio maana huwa wanadanganywa na wanasiasa.
 
CCM ina hazina kubwa sana, ccm hakijazuka tu, huwezi kuipima CcM na akina Lisu, Mnyika, Heche.

Itizame CCM tangu 1977 ilipozaliwa ilikuwa na akina Sita, Msekwa, Sapi Mkwawa, Moses Nnawiye, Makamba, Mwakanjuki, Karume, Mzindakaya, Natepe, Mkapa, Nyerere, Kawawa, etc ambao hawapo na bado ipo stable.

Wasiwasi wangu baada ya akina Mnyika, Mbowe, etc wakitoka nani atafuata? tangu 1992 vyama vingi kuingia bado viongozi wa vyama hivi bado wale wale Lipumba, Mbowe, Maalim Seifu, Baregu, Mbatia, Hashimu Rungwe, etc inawezekana kabisa baadaya ya 2020 hivi vyama vitakufa kabisa.

Siamini kama CCM ina vijana wenye mvuto kwa sasa.Siamini kama inaweza kuitisha Mkutano wa hiayi ikapata wasikilizaji wa maana.Nadhani chama kimechokwa maana hakuna jipya la kujivunia.Kama vile walivyoogopa kuwatangaza wagombea wao kupitia jina la chama ndivyo itakavyokuwa kipindi kijacho.
Wapinzani bado wanakubalika na kama uchaguzi huru na haki ukiitishwa huenda CCM ikageuka chama cha upinzani.Ukitaka kuhakikisha mikutano ya hadhara iitishwe halafu uone mwitikio.Kwa sasa watu wamechoka zaidi kuliko ilivyokuwa miaka miwili iliyopita.
 
Back
Top Bottom