Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,498
- 113,597
Wanabodi,
Mara baada ya kifo cha Mwangosi nilipandisha uzi huu humu jf
Waziri Nchimbi na IGP Mwema, Mnasubiri Nini Kujiuzulu? kwenye hitimisho langu nilisema h
" Kama ni kweli polisi mfyatuaji risasi atapandishwa kizimbani, then RPC wake nae ndie amtangulie, huku waziri Nchimbi na IGP Mwema, wao bado wanasubiri nini kuwajibika?.
Hata hivyo, damu ya mtu, haiwezi kupotea bure!, sio damu tuu ya Mwangosi, bali damu za wote zilizo mwagika bila hatia, kwa mujibu wa sheria kubwa kabisa iitwayo The Law of Karma, damu zote hizo lazima zitafidiwa kwa damu au kwa adhabu kubwa zaidi ya damu!. Tatizo la fidia, inaweza kuwa kubwa kuliko tukio lenyewe au hata kuwakumba na wasio husika ili kuisafisha roho ya marehemu!". Mwisho wa kunukuu!
Hiki kilichotokea sasa kwa mawaziri kuwajibika ni utekelezaji tuu wa "karma" na kilichotokea juzi kwenye oparation tokomeza sio kipya nchini mwetu, wale wenye kumbukumbu, mwaka 1976, kulitokea operation kama hiyo Mkoani Mwanza na Shinyanga hali ilikuwa kama ifuatavyo.
Kulitokea mauaji ya vikomgwe huko Mwanza na Shinyanga kwa tuhuma za ushirikina. Watuhumiwa wawili, walifariki mkoani Mwanza. Mwaka huo 76 mimi nilikuwa nasoma darasa la kwanza pale Nyakahoja!.
Watuhumiwa wawili wa mauaji ya vikongwe, Bw. Masanja Kahula Mazengenuka na Isaack Mwana Mkoboko, walipoteza maisha kwenye mahojiano. Waziri wa mambo ya Ndani wakati huo Ali Hassan Mwinyi alijiuzulu, Waziri wa Usalama wa Taifa, Peter Siyovelwa nae aliwajibika!, mkuu wa Polisi, Pundugu alistaafishwa kwa manufaa ya umma. Mkuu wa Usalama wa Taifa, Mzena alistaafishwa kwa manufaa ya umma. Wakati huo, Peter Kisumo ndiye alikuwa mkuu wa mkoa wa Mwanza, naye pia aliwajibika!. Watekelezaji ni RPC wa Mwanza, Cassian Mkwawa, RSO wa Mwanza, Andrew M na DSO, Jemes Ihuya! walishitakiwa katika ile kesi maarufu ya Mauaji Mwanza.
Wakuu hao watatu wa polisi walikuwa wakiishi nyumba tatu zilizofuatana zikiwa pale Isamilo ya chini ikianza ya Ihuya, ikafuatia ya Andew M na ya mwisho ni ya Mkwawa!. Nyumba ya nne ilikuwa ni Daktari Mkuu wa Mkoa, Dr. Dahoma ambaye yeye alihusishwa kutoa post morterm report fake, ili aligeuzwa PW, hivyo kutoshitakiwa. Just imagine hali ilikuwaje mtaani wakati vigogo wanne wanene wa serikali wanaokaa mtaa wote wanashitakiwa kwa kosa la mauaji!.
Kesi iliendeshwa, aliyekutwa na hatia alihukumiwa, Mshtakiwa mmoja Andrew M, hakukutwa na hatia. aliachiwa huru, ila wakuu wote waliwajibishwa!.
Hiki kilichotokea kwenye operation tokomeza, hakina tofauti na operation ile, Kama waziri wa Mambo ya Ndani amejiuzulu, IGP Saidi Mwema anasubiri nini?!. Kama Waziri wa Ulinzi Amejiuzilu, CDF Mwamunyange anasubiri nini?!. Waziri wa TISS na Mkurugenzi Mkuu wa Tiss nao wanasubiri nini?. Tunasubiri kuona wahusika wakipandishwa mahakamani kama ile ya 1976!.
Naomba kuwasilisha.
Pasco.