Baada ya Mwambe " kutulizwa" na Rais Magufuli sasa nitamchukulia Tundu Lissu fomu ya kugombea Uenyekiti wa Chadema

Tofautisha uenyekiti na urais.

Kwa CDM walimpatia Lowasa huku wakijua hawezi shinda urais wakati huohuo wakijua atapata kura nyingi kuliko mtu yeyote ndani ya CDM hivyo wapate viti maalum wengi.
Hao viti maalumu wanaisaidia nini?!
 
Mtu yeyote anayependa mambo ya kuhama vyama ni tapeli wa kisiasa mtu makini hawezi kuama chama kwa sababu ya cheo uwenyekiti apewe Lissu au Heche otherwise chama kitapotea.
Kweli kabisa Mkuu...... Hebu ona alichofanya Mwanbe Mbunge wa jimbo la Ndanda.......Alikuwa CCM akaenguliwa kwa kufahamu utendaji wake Mbovu..... Lakini lilipopita Winni la Kisulisuli la Chadema likamzoa na Sasa anaumbuka kwa Vitendo na matokeo yake anataka kuwaaminisha Viongozi wa juu ya kuwa alionewa Kumbe Aaaaaa wapiiiiiiii....... Kweli Dunia ya leo unawawekea wananchi Sinema ya uliyojirekodi na kuwaonyesha Watu kweli na wewe mwenyewe haupo Kama siyo Dharau ni nini...?
 
Mbowe kwanza jela inamuhusu, uenyekiti angalau mpeni Lissu alipigwa risasii 34 na bado yupo hai
 
Kiukweli kabla Rais Magufuli hajafanya ziara mikoa ya Lindi na Mtwara nilimuona mbunge wa Ndanda mh Cecil Mwambe kama kamanda anayeweza kumrithi mkongwe wa siasa za upinzani mh Mbowe.

Lakini baada ya Mwambe kuhojiwa na Rais Magufuli na kukiri kuwa alikuja Chadema kwa bahati mbaya baada ya kura zake kule CCM kwenye maoni kupewa mtu mwingine na yeye kupigwa chini, nimegundua Cecil kimwili yuko Chadema lakini kiroho yuko CCM hivyo hatatosha.

Hivyo basi wanaoniunga mkono naomba kwa pamoja tumchukulie fomu kamanda mwingine shupavu mwenye ujasiri uliotukuka ndugu yetu Tundu Antipas Lisu.

Sijajua fomu inauzwa bei gani lakini ninajitoa kwa gharama yoyote ili tupate kiongozi sahihi wa kumrithi kamanda Freeman.

Naomba kuwasilisha

Maendeleo hayana vyama!
Habari ya mujiini kwa sasa ni kukamatwa kwa ndege yetu kule Canada
 
Back
Top Bottom