Baada ya mwalimu Nyerere, Tundu Lissu ndie mwanasiasa mwenye influence kubwa kwa sasa

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,014
144,371
Huu ndio ukweli japo ni mchungu kwa jamaa zetu wa upande wa pili.

Msimamo wake,kutoyumba,ujasiri wake,kusema ukweli pasipo kujali jina wa cheo cha mtu, kutokuwa na kashifa, ufahamu na uelewa mkubwa wa mambo kuhusu siasa na uongozi,n.k, ni miongoni mwa sifa zinazomtofautisha na wanasiasa wengi sana wa leo hii.

Lissu ana kipaji kikubwa cha siasa na uongozi kuliko mwanasiasa mwingine yoyote yule.

Lissu,kama ilivyokuwa kwa Baba wa Taifa, ana uwezo wa kuwakemea watawala bila kumung'unya maneno jambo ambalo wanasiasa wengi leo hii limewashinda.

Lissu,kama ilivyokuwa kwa Baba wa Taifa,ameonyesha uwezo mkubwa wa kuona mbali kwani mengi aliyokuwa akionya leo hii yanatimia japo ni vigumu kwa baadhi ya watu kukiri ukweli huu.

Lissu,kama ilivuokuwa kwa Baba wa Taifa,ameonyesha uwezo mkubwa wa ku-capture attention ya watu anapohutubia wananchi au kuongea na media kuliko mwanasiasa mwingine yoyote yule.

Kama ambabyo Mandelea aliwakosesha usingizi Makaburu,leo hii Lissu anawakosesha usingizi kina fulani na pengine wanatamani hata afukuzwe nchini na angekuwa na asili ya watu wa mataifa mengine,bila shaka leo tungesikia nae si raia wa nchi hii na uzuri hataki mikoani ya pembezoni.

Lissu leo hii akiwa na mkutano na waandishi au akihutubia live, Lumbumba na hata Magogoni shughuli nzima za siku zitasimama kutaka kumsikiliza Lissu ataongea nini.

Leo hii ukiwapa assiģnment wanafunzi wa sekondari au chuo ya kuandika maelezo juu ya mwanasiasa mahiri/machachari,wanafunzi wengi watamtaja Lissu kwasababu watakuwa na hoja nyingi na pia mifano mingi ya kutetea chaguo lao.

Tutausema ukweli huu angali yu hai na si vinginevyo.
 
Salary Slip,

Na kwa nyongeza, serikali imetikisika na kutaharuki zaidi maana mtetezi wetu wa kweli na kaka wa taifa Mh. Tundu Lissu kuelekea Brussels Belgium /Luxembourg kulipo na makao makuu ya Jumuiya ya Ulaya / EU na bunge la ulaya siyo habari nzuri kabisa kwa wana-Lumumba na serikali yao ya CCM.

Habari za ukandamizaji, vitisho, kujaribu kumaliza maisha ya walio na fikra tofauti na utawala huu wa awamu hii zitatinga ktk kamati, bunge na makao makuu ya jumuiya ya ulaya /EU.

Na jumuiya hii ya ulaya hufanya kazi na maazimio kwa umoja wao ikiwemo kusitisha misaada, mikopo, kutenga nchi, vikwazo vya viza kwa viongozi kuingia EU na kuwekea vikwazo vya kiuchumi kwa tawala gandamizi zisizofuata demokrasia, katiba na uhuru wa raia kujumuika/kupashana habari.

Tutegemee kutakuwepo ktk siku chache zijazo, matamko yasiyo ya kawaida kutoka serikalini kuhusu maendeleo-chanya ya uchunguzi wa waliohusika na jaribo la kuondoa uhai wa mwanasiasa mashuhuri maana mbinyo-wa kidiplomasi/ kisiasa kimataifa unainyemelea serikali ya awamu hii kwa mara ya mwanzo.

Utawala wa awamu hii ulizoea ku- "deal" na vuguvugu la kiupinzani wa ndani ya nchi, swali kuu ni je wataweza kuhimili dhoruba ya kimataifa kidiplomasia na kisiasa? Na wale waliohusika na mipango-ya-kimla kupanga, kufadhili na kutekeleza vitendo viovu, je watatolewa kama kafara kunusuru sura, haiba na sifa ucharwa za viongozi wa CCM.

Yetu macho yapo hapa Jamiiforums kutizama kwa makini kila mpepesuko, kujikwaa, mtikisiko, kuanguka na hatimaye kuchanganyikiwa kwa wadhalimu hawa.
 
huo nyi uchochezii

Bashite ndiye mwenye ushawishi baada ya Nyenyere...

kumbuka alimfukuzisha kazi Nnape,halafu tena wale watumishi wasio na vyeti 12,856...(yeye akabaki)

halafu,wale wacongo wabakaji alihusika wao kuwa uraiani

na kama hutaki 'mwezi wowote lulu naye atakuwa huru' dad's coming!
 
Huy
Huu ndio ukweli japo ni mchungu kwa jamaa zetu wa upande wa pili.

Msimamo wake,kutoyumba,ujasiri wake,kusema ukweli pasipo kujali jina wa cheo cha mtu, kutokuwa na kashifa, ufahamu na uelewa mkubwa wa mambo kuhusu siasa na uongozi,n.k, ni miongoni mwa sifa zinazomtofautisha na wanasiasa wengi sana wa leo hii.

Lissu ana kipaji kikubwa cha siasa na uongozi kuliko mwanasiasa mwingine yoyote yule.

Lissu,kama ilivyokuwa kwa Baba wa Taifa, ana uwezo wa kuwakemea watawala bila kumung'unya maneno jambo ambalo wanasiasa wengi leo hii limewashinda.

Lissu,kama ilivyokuwa kwa Baba wa Taifa,ameonyesha uwezo mkubwa wa kuona mbali kwani mengi aliyokuwa akionya leo hii yanatimia japo ni vigumu kwa baadhi ya watu kukiri ukweli huu.

Lissu,kama ilivuokuwa kwa Baba wa Taifa,ameonyesha uwezo mkubwa wa ku-capture attention ya watu anapohutubia wananchi au kuongea na media kuliko mwanasiasa mwingine yoyote yule.

Kama ambabyo Mandelea aliwakosesha usingizi Makaburu,leo hii Lissu anawakosesha usingizi kina fulani na pengine wanatamani hata afukuzwe nchini na angekuwa na asili ya watu wa mataifa mengine,bila shaka leo tungesikia nae si raia wa nchi hii na uzuri hataki mikoani ya pembezoni.

Lissu leo hii akiwa na mkutano na waandishi au akihutubia live, Lumbumba na hata Magogoni shughuli nzima za siku zitasimama kutaka kumsikiliza Lissu ataongea nini.

Tutausema ukweli huu angali yu hai na si vinginevyo.
Jamaa yetu yeye na siasa za kishamba kwa kweli kwa sasa hatuna kiongozi mwenye maono chanya kwa ustawi wa nchi yetu,kiongozi anayeweza kuwaunganisha watanzania
 
Nauliza kwa maana ya kuuliza
Nani anapenda kuelezwa ukweli
Nani anapenda kuwekwa kona
Nani anapenda kupewa za uso
Kuambiwa ukweli ni uchochezi

Kila mtu apenda kusifiwa ujinga
Mgongo wa chupa kupaka futa
Kusifiwa hata kwa yasiyokuwepo
Ndipo bichwa hufura kwa furaha
Huona ndiye mpakwa mafuta
Mwokozi wa wakazi wa kitale
Ingaa ni nyoka mwenye pakanga
Achomaye kama fir@ na kibiriti

Yangu Macho na Masikio tu
Kuusikiza ukweli wake Tundu
 
...Tutegemee kutakuwepo ktk siku chache zijazo, matamko yasiyo ya kawaida kutoka serikalini kuhusu maendeleo-chanya ya uchunguzi wa waliohusika na jaribo la kuondoa uhai wa mwanasiasa mashuhuri maana mbinyo-wa kisiasa kimataifa unainyemelea serikali ya awamu hii kwa mara ya mwanzo.
Ndoto za mchana hizi.
 
Back
Top Bottom