Baada ya Msiba wa wanafunzi kule Arusha waandishi wengi watarudi kwenye habari za kiki

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,533
22,279
Baada ya Msiba wa wanafunzi waandishi wengi watarudi kwenye habari za kiki lakini tungekua na waandishi makini wangefanya research ya vyazo vya ajali..
Kuna maswali mengi sana ambayo mpaka watanzania wanasubiri majibu ya kina kuhusu ajali hiyo.
Jana RPC wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha akiongea na waandishi wa habari alisema.
"Siku ya tukio walikuwepo abiria 38 kwenye gari katika uchunguzi baada ya kubaini hilo tumeshachukua hatua kwa mtu aliyewezesha gari hilo kupakia hao watu, tumeshamkamata mmiliki wa gari ambaye ndiye mwenye shule hii, sasa hivi tunaendelea na uchunguzi na utakapokamilika atafikishwa mahakamani" alisema RPC wa Arusha

Kwa mujibu wa Mkumbo anasema gari hiyo ilikuwa na kibali cha kubeba watu 30 lakini gari hiyo siku ya ajali ilikuwa na watu zaidi ya 30.
Maswali ya kujiuliza kutoka Arusha mpaka Karatu ambapo ajali imetokea hapakuwa na ukaguzi wowote ?Je vyombo vya usalama wapi? Vyombo vya Usalama kama walikuwepo kwa nini waliruhusu vipi gari kupakia abiria zaidi ya 30?
 
Back
Top Bottom