Baada ya Mkandawille kijana mwingine nae aacha chuo Udaktari kufundisha tuition advance

ze jj

JF-Expert Member
Aug 20, 2012
494
590
Wadau kwa mliosoma advance combination za science naamini huyu Mkandawille mnamfahamu. Historia yake inasemekana alikuwa akisoma MD Muhimbili akaacha ili afundishe chemistry adv tuition. Kiukweli ana wezo mkubwa sana kiasi kwamba alipendwa sana na wanafunzi.

Sasa kuna kijana mwingine maarufu sana Kanda ya Ziwa (Mwanza) anaitwa Dr. Jose. Naye kafata nyayo zake, ameacha MD Bugando third year mwaka jana na anafundisha advanced Biology.

Ni maarufu kiasi kwamba anakuwa na wanafunzi mpaka mia tatu.

Wadau hii imekaaje? Kwanini hawa wanaoacha MD wakifundisha wanapendwa na wanafunzi? Kiukweli wanapiga pesa kuliko graduate wa MD.
 
They are using the title Dr. kufanya biashara ya tuition,other wise hakuna cha ziada.

Juhudi zake na uadilifu wake ndio unaomfanya awe maarufu kiasi hicho,la sivyo asinge ambulia kitu.
 
Ni vilazaaa, tu hao.
Kwa mfano , Kwa nini wasihitimu masomo (MD) badala ya kufanya hiyo kazi ya utabibu wakaenda kuendelea na kufundisha hizo tuition ?

Kwa nini wameacha masomo/ ameacha masomo?

Kwa nini wote wafundishe tuition baada ya kuacha chuo?

Au unawashauri na kuwarubuni vijana waache masomo ya MD wakafundishe tuition,?

Mleta mada acha ushabiki uchwara unapoleta mada.

Kwa kifupi wewe mleta mada nakuona unachowaza na kwa hiyo wewe ni mchochezi sana.
 
mbona umepanic sana!!!!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom