BAADA YA MIEZI 8 MWOCHWARI , LEO NDO MAZISHI YAKE

KUDOLE CHA MWISHO

JF-Expert Member
Joined
Aug 13, 2017
Posts
407
Reaction score
898
Mwili wa Frank Kipange (22) umechukuliwa katika Hospitali ya Rufaa Mbeya leo tayari kwa mazishi baada ya kukaa mochwari kwa miezi 8.

Awali ndugu wa marehemu walikataa kumzika wakitaka uchunguzi wa chanzo cha kifo chake, huku wao wakidai alifia mikononi mwa polisi.

Frank alifariki dunia Juni 24, 2018, na ndugu zake walifungua shauri katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya, ambapo mahakama hiyo ilitupilia mbali keshi hiyo na kuamuru azikwe.

Hata hivyo wanafamilia walikata rufaa katika Mahakama ya Rufaa, lakini nayo ikaitupilia mbali kesi hiyo kwa madai ya kutofuata taratibu wakati wa ufunguaji kesi.

Hospitali ya Rufaa Mbeya imewasamehe ndugu hao gharama za kuutunza mwili huo, wakiwataka watumia fedha hizo kwa ajili ya mazishi. (22) umechukuliwa katika Hospitali ya Rufaa Mbeya leo tayari kwa mazishi baada ya kukaa mochwari kwa miezi 8.

Awali ndugu wa marehemu walikataa kumzika wakitaka uchunguzi wa chanzo cha kifo chake, huku wao wakidai alifia mikononi mwa polisi.

Frank alifariki dunia Juni 24, 2018, na ndugu zake walifungua shauri katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya, ambapo mahakama hiyo ilitupilia mbali keshi hiyo na kuamuru azikwe.

Hata hivyo wanafamilia walikata rufaa katika Mahakama ya Rufaa, lakini nayo ikaitupilia mbali kesi hiyo kwa madai ya kutofuata taratibu wakati wa ufunguaji kesi.

Hospitali ya Rufaa Mbeya imewasamehe ndugu hao gharama za kuutunza mwili huo, wakiwataka watumia fedha hizo kwa ajili ya mazishi.
FB_IMG_1556872511294.jpeg
 
Mleta mada ongeza umakini kidogo.

Sasa kutoka juni 2018 mpaka unayoisema leo May 2019 ni miezi 8?

Frank amezikwa baada ya kukaa mochwari miezi nane yaani alizikwa Mwez February mwaka huu.
 
Anataka aonekane yeye ndio mleta taarifa wa kwanza hapa wakati tayari taarifa zipo siku nyingi hume..asuburi wadau watakuja hadi na ushahidi
 
Back
Top Bottom