Treni ya kwanza ya Abiria yawasili Arusha baada ya miaka 30

Kweli Tanzania tumepata Raisi haya mambo ukiyatazama unaweza kuhisi ni ndoto lakini ndio hivyo yanatokea.

Ashukuriwe Mungu, wabarikiwe wote waliochangia JPM kuwa Raisi wa hii jamuhuri, hakika Mungu hawatupi waja wake. Tulifunga na kuomba kwa ajili ya kupata Raisi mzalendo na haya ndio matokeo yake, viva JPM.
 
Pongezi kwa mjerumani kwa kuona mbali. Walianza kuijenga mwaka 1893 mpaka 1912 ilianza kazi. Hawa wajerumani wangebaki sijui tungekuwa na maendeleo kiasi gani ila cha moto tungekipata.
Pongezi kwa kufufua reli hiyo.

nimesikitika sana kuona mwana jf una comment hivi,
mjerumani hakujenga hiyo reli ili bibi yako asafiri mkuu, hiyo ilikuwa ni kwa ajili ya kurahisisha wizi wake wa natural resources zetu, mjerumani alijenga reli hiyo kwa faida zake binafsi
fuatilia historia hizi reli zilitumika kuiba dhahabu kutoka kwenye makoloni

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Dah! Hata mimi nimesikitika kwa nilichoandika. Ila ndio hivyo reli ya mwaka 1893 ndio tunaikarabati leo mwaka 2020. Kwa hiyo pongezi ziende moja kwa moja kwa serikali ya awamu ya tano kwa kukarabati reli ya Arusha. Hongera sana TRC.

(Natumaini masikitiko yako yamepungua)
 
nimesikitika sana kuona mwana jf una comment hivi,
mjerumani hakujenga hiyo reli ili bibi yako asafiri mkuu, hiyo ilikuwa ni kwa ajili ya kurahisisha wizi wake wa natural resources zetu, mjerumani alijenga reli hiyo kwa faida zake binafsi
fuatilia historia hizi reli zilitumika kuiba dhahabu kutoka kwenye makoloni

Sent from my iPhone using JamiiForums
Kwa hiyo bila wao tungekuwa na reli sasa? Lazima ukubali kuwa ukoloni ulileta faida pia
 
nimesikitika sana kuona mwana jf una comment hivi,
mjerumani hakujenga hiyo reli ili bibi yako asafiri mkuu, hiyo ilikuwa ni kwa ajili ya kurahisisha wizi wake wa natural resources zetu, mjerumani alijenga reli hiyo kwa faida zake binafsi
fuatilia historia hizi reli zilitumika kuiba dhahabu kutoka kwenye makoloni

Sent from my iPhone using JamiiForums
Hao makamanda wakishavaa magwanda yao ni vigumu sana kuwaelewa.
 
Sikujua kwamba kuna watu wa hali ya chini wanaofaidika na usafiri wa treni hususan third class.
Mpaka nilipoona wajomba wa Kigoma wanavyo changamkia treni. Kwao muda sio issue na hata buffet car hawana habari nayo.
 
Mimi ni miongoni mwa abiria wa mwishomwisho waliowahi kutumia usafiri huo wa treni kutoka Moshi kwenda Arusha miaka takriban 35 iliyopita. Tulikua tukipita nyika zenye nyasi fupi za ki savannah katika miji/stesheni za Boma, Kikuletwa, Kia na Arusha yenyewe

Sijawahi kuelewa kwanini reli hii ilikufa/iliuliwa!!! Juhudi zozote za kuifufua na kisha kuiboresha hakika ni za kuungwa mkono na wapenda maendeleo wote
 
Baada ya miaka 30 hatimaye treni imekanyaga ardhi ya Jiji la Arusha.

Nategemea kumpeleka mwanangu akaipande na kuiona treni ili azielewe katuni zake kivitendo.

1582782068184.png
 
Back
Top Bottom