Baada ya Mh Kikwete kusherehekea vifoo vya Mawaziri walio Bwagwa nje , Sasa Asubiri Chake 2015

abdulahsaf

JF-Expert Member
Aug 31, 2010
858
130
Millya Apokelewa Rasmi CHADEMA
Mkutano mkubwa wa CHADEMA jana Arusha viwanja vya NMC walpowapokea rasmi wanachama wapya waliotoka CCM.
Picha kwa hisani ya Jamiiforums
 
Huyu kikwete amezoea kwenda nje then akirudi anangalia CD ZA KANUMBA, ATAPATA WAPI MDA WA KUSOMA KATIBA YA NCHI..USANII M2UPU NA HUYU MWENZAKE KAPINDA
 
Nakweli ye anazani anayotoa kafara wenzake tena wamemsaidia sana anadhani dhambi hiyo yeye haita mkuta hapa duniani bana.;.......inasikitisha kumtoa nundu na kumwacha kombani...unatoa msafoi unaweka fisadi.
 
2015 kikwete atakua amemaliza muda wake kwa mujibu wa katiba yetu sasa iko kifo chake kinatoka wapi?ungenambia kabla ya muda huo hpo ningekuhoji zaidi
 
Hakuna Shaka kuwa Uchaguzi mkuu wa 2015 utakuwa mzito kwa upande wa Chama tawala Ccm kwa vile ushindi wao mara nyingi hutokana na kutumia ukungu wa kizaa ili kujipatia ushindi wa kimabavu kwa kutumia vibaya vyombo vya Dola.


Lakini mwaka huu wa 2015 mambo yatakuwa mazito kwa upande wao wachambuzi wengi wanasema hivyo, kwanza ni kutokana na Chama cha wananchi Chadema kuonekana na kukubalika kuwa ni chama cha wananchi kweli na kuwa karibu mno na wananchi.


Swala jengine ni kujaribu kufichuwa uoza na marazi mingi ya ufisadi wa mabilioni yalio ikimba Tanzania chini ya utawala wa Chama cha Ccm na viongozi wake kujilimbikizia mabilion na rasilimali za mabilion huku Watanzania wengi wakichindwa kupata mloo moja kwa siku.


Hii imewa sababisha Watanzania wengi kutokuwa na imani na ccm kutokana na kufuga majambazi wakutisha(Wabadhilifu wa mali za Umma) ndani ya chama, Watanzania wamesoma mengi kwa Chadema na hivi sasa wanajaribu kufuta ukungu wa macho na kuto kuwa blind dena wakudanganywa kwa T-SHART na Kanga za kisudu kila kipindi cha Uchaguzi.


Hivi sasa ni wakati wa rasilimali za Watanzania kutumiwa na Watanzania wote wakila Tabaka sio viongozi fulani tu wa chama huku Watanzania wengi waki umbuka kwa joto la jiwe (Maisha magumu).


Hakuna sababu ya Watanzania (Tanzania kwa Ujumla) kutiwa katika kundi la nchi omba omba na maskini zakutupa haliyakuwa Tanzania ni Tajiri na ina rasilimali nyingi zakujivunia? lakini rasilimali hizo hufaidisha Vigogo tu kwa kujilimbikizia Mali huku walio wengi wakifaa njaa.


Tanzania sio nchi maskini lakini mfumo ulopo ndio unaifanya nchi iwe maskini na watu wake, tuangalie viongozi wetu jinsi walivyo jilimbikizia mamali na jinsi wanavyo vuruga pesa za Umma kiholela? kiongozi moja tu wa Serekali anaweza kuwa na Nyumba sita magari kumi na miradi kibao ya mamilion.



Jee ukiangalia takumu ya Mshahara wake utaona nusu ya mali zake amezipata kwa kupora pesa ya Umma ili kujilimbikizia mali na mafilia yake, kuiba kwa mamilioni Tanzania sio Zambi lakini kuiba kuku mitani ndio Zambi.


Mh Kikwete hivi juzi kapanguwa Baraza la Mawaziri na wale 8 kati yao 6 ndio walio tupwa nje kwa kosa la ubadhilimu wa pesa za uma mamilionea?, sasa Watanzania tuangalie baada ya kutupwa nje hao mawaziri sita ,jee hatuwa ya pili itafuata nini?.


Ikiwa hukumu yao ndo imepita kwa kutupwa njee, basi hii itakuwa Kikwete anacheza na akili ya Watanzania , maana haingii akilini mtu kuondoka na mamilioni kitu ambacho kinaisababicha madeni Tanzania inayo daiwa na IMF kicha walipo kodi kila mtanzania kulipa deni hilo? hii itakuwa sio haki.


Hivi sasa Tanzania inadaiwa madeni akubwa makubwa na kila mtanzania akiambiwa alipe basi tutachukuwa muda kuyamaliza, sasa leo umdu anaondoka na pesa za umma na malipo yanakuwa ya Watanzania wote hii sio haki na itakuwa Kikwete hajafanya kitu mbele ya Watanzania.

Ili ili kikwete ajisafishe mbele ya Watanzania nilazima Hawa watu wapandishwe kizimbani ili iwe mfano kwa wengine na kuisaficha Tanzania na Ufisadi wakutisha, imekuwa upole wake ni fursa za Mafisadi kufanya watakamo na kuwa kama ndio mfumo wa maisha kwa viongozi kuiba pesa za umma?.

Hii ife mara moja tukikubali kuendelea hii itakuwa ndio kama calture ya Viongozi.
 
Sio hivyo tu ni ukweli usiopingika haya anayafanya si kwa mapenzi yake bali ni kutokana na hali tete inayosababishwa na upinzani.Ndani ya CCM wachafu ni wengi mno kinachofanyika mambo yanapoharibika ndipo kale kamchezo cha kutoangaliana usoni hufanyika, hata hawa hanaofia haka kamchezo wanaondoka kuinusuru CCM dhidi ya ANGUKO kwa wananchi.Cha kushangaza wanalificha anguko hili kwa watanzania wasiokuwa na elimu,wenye elimu tunayafahamu yote kuwa MWISHO wa CCM umefika hata wale walikuwa wakiamini kuwa watatalawa milele katika nchi za Afrika sasa hawapo:Ben Ali (Tunisia)Gadaffi(Libya)Mubarak(Misri) na zaidi Malawi ambako demokrasia ya kweli imefanyika.
 
hadi mwili unasisimka!
 

Attachments

  • umati-mboye.jpg
    umati-mboye.jpg
    24.3 KB · Views: 46
Kaka Abdulahsaf unayoyaongea ni kweli kabisa suala la kuwapeleka Mahakamani Mawaziri kwa Kikwete ni SUMU,sumu ambayo si hawezi kuionja Mheshimiwa huyu bali karibu viongozi wote wa nchi hii.Shida inakuja hapa:
  1. Viongozi waliopo Serikalini wengi wao wameingia kutokana na urafiki miongoni mwao hususani kwa Rais
  2. Pesa nyingi zinazotumiwa kwa rushwa,hongo, kitu kidigo kuanzia kura za maoni mpaka uchaguzi mkuu kuwaweka viongozi hasa Rais zinatolewa na watu ambao baada ya kuingia madarakani hupewa nafasi mbalimbali kama kulipa fadhila za kujitolea kwao.
  3. Viongozi wengi waliopo madarakani ni WACHAFU ndio maana inakuwa vigumu kuchukua hatua kwani huwezi kumpandisha kizimbani kwa wizi wa mabilion ilhali yeye mwenyewe anayempeleka mahakamani amenufaika katika wizi wa Mtuhumiwa licha ya hivyo yawezekana Mtuhumiwa anafahamu wizi mwingi tu ambao umefanywa na huyu tunayesema awapeleke wenzake mahakamani
  4. Hakuna kipengele kilicho wazi katika katiba kinachoagiza kiongozi wa umma anapokumbwa na kashfa ya kuliingizia Taifa hasara kwa yeye mwenyewe kuiba au kusaini mkataba ambao hauna manufaa kwa Taifa apelekwe mahakamani.
  5. Suala la amani linaloimbwa na viongozi hawa hasa Mkuu kwamba endapo atachukua hatua dhidi yao amani haitakuwepo.Ukweli ni kwamba Tanzania hakuna AMANI.Amani iko wapi iwapo viongozi wanalalia manoti ilhali wananchi hawana uhakika wa japo mlo mmoja ambao nao sio mlo kamili,amani iko wapi iwapo suala la mikopo kwa wanafunzi wa vyuo ni tatizo mikopo ambayo serikali haitoi bure kwa mtoto wa muuza vitumbua bali itamdai mtoto huyu amalizapo masomo yake wakati watoto wao wanasoma nje ya nchi kwa pesa za walalahoi zilizoibwa na wakubwa hawa,amani iko wapi wakati shule hazina hata chaki za kufundishia ilhali kuna pesa zinazoibwa kwenye wizara mbalimbali kwa kuwalipa wafanyakazi hewa,Amani iko wapi wakati mwananchi anapigwa risasi na kuuwawa kwa kudai haki yake kwa serikali.
  6. HAKUNA MAREFU YASIYOKUWA NA MWISHO NA MWISHO WA MWONGO NI FEDHEHA.HATUTA NYAMAZA TUTAYASEMEA HAYA KWASABABU TANZANIA NI YETU NA HAKUNA ATAKAYEKUFA AKAENDA KUZIKWA NJE YA NCHI WOTE TUTAZIKWA HAPAHAPA TANZANIA HIVYO LAZIMA TUITETEE NCHI YETU.
 
Sio hivyo tu ni ukweli usiopingika haya anayafanya si kwa mapenzi yake bali ni kutokana na hali tete inayosababishwa na upinzani.Ndani ya CCM wachafu ni wengi mno kinachofanyika mambo yanapoharibika ndipo kale kamchezo cha kutoangaliana usoni hufanyika, hata hawa hanaofia haka kamchezo wanaondoka kuinusuru CCM dhidi ya ANGUKO kwa wananchi.Cha kushangaza wanalificha anguko hili kwa watanzania wasiokuwa na elimu,wenye elimu tunayafahamu yote kuwa MWISHO wa CCM umefika hata wale walikuwa wakiamini kuwa watatalawa milele katika nchi za Afrika sasa hawapo:Ben Ali (Tunisia)Gadaffi(Libya)Mubarak(Misri) na zaidi Malawi ambako demokrasia ya kweli imefanyika.
 
Back
Top Bottom