Baada ya matokeo ya Igunga, CUF itoe tamko rasmi kwa wanachama wake

Baada ya matokeo ya Igunga, CUF itoe tamko rasmi kwa wanachama wake

TATIZO limetokea WALIFUNGA NDOA YA MKEKA NA CCM BILA KUALIKA WANACHAMA WA BARA KULA UBWECHE.
 
Umeandika hii article bila ya uchambuzi wa ukweli. CUF ina mafanikio zaidi ktk vyama vya upinzani. Angalia Wabunge waliokuwa nao, na sasa hivi wanayr Makamu wa Rais.

Sasa huoni kama hiyo ni progress?
Aaaaaaah mr right this time you sholud call yourself mr wrong...
 
Cuf, ilipojitangaza kipindi kile kuwa ni ngangari kilionyesha ni chama mbadala kinachoweza kusimamia utajiri wetu, kumbe walikuwa ngangari kwa tamaa, haikuwa na haja ya kukubali ndoa na ccm kisa watapata nafasi ya pili, matokeo ni kusababisha baraza kubwa la mawaziri na gharama kubwa katika uendeshaji wa zanzibar. Wale waliopigwa january 27 2001, wale wananchi walioandamana ili kutafuta haki na usawa damu iliyomwagika ni kwaajili ya seif apate umakamu na baadhi wapate uwaziri.

Hiki sio chama na hii yote ni kutokana na chama kuwa na sura ya kumuangalia mtu mmoja kwa matumaini, seif alisha sema kama ccm watanipa uenyekiti wa chama nipo tayari kurudi !, sasa prof lipumba anachokifanya cuf sikielewi anatakiwa asome alama za nyakati other wise atafulia kama mrema ila chdema tuna watu makini wengi na wenye uwezo zaidi na wanakubalika na wananchi wengi. Yaani 2015 ni raaaaaha
 
Hatuhitaji tamko la CUF, kwani kwaniaba yao, wananchi wa tanzania kupitia wapiga kura wa Igunga wametoa TAMKO! Inatosha wao(CUF) kuchukua hatua na kufanya maamuzi
 
na hili suala la kutekeleza sera za ccm vicwan ndani ya suk then wakfka bara wao ni wapinzani wa sera za ccm itawagharim mno leo na cku zijazo..
 
Jamani kuna vitu ambavyo havitaki kuumiza kichwa saana CUF ni ccm2 au b then wale siyo wapinzani wa ccm.
 
Umeandika hii article bila ya uchambuzi wa ukweli. CUF ina mafanikio zaidi ktk vyama vya upinzani. Angalia Wabunge waliokuwa nao, na sasa hivi wanayr Makamu wa Rais.

Sasa huoni kama hiyo ni progress?MOBILE!
 
Anguko la CUF lilianza huku bara hata kabla ya ndoa yao huko visiwani na CCM. Tatizo kubwa ni kwa vigogo waanzilishi ambao wengi wanatokea Pemba na Unguja kushindwa wavutia wanasiasa wenye ushawishi na ubunifu toka upande wa bara. Tuseme kwamba chama kilibakia kama kampuni ya Seif Sharif Hamad na wenzake wachache. Licha ya Lipumba kuwa mwenyekiti,lakini ni Seif aliyebakia na uongozi na sauti ya mwisho ndani ya CUF.
 
Please update us. Mi niko kenya na sina tv set nilipo. I am so dying to celebrate Igunga's revolution.
 
kosa la cuf ni kuungana na ccm. Wameponzwa, kama ilifikia hatua ya kuambatana na magamba mpaka kwenye banda la kuku, wananchi walikuwa wanawachora tu.
 
Tatizo la CUF sio udini bali uwezo mdogo wa viongozi wao kukijenga chama. Angalia ccm walipowapakazia kuwa ni chama cha kiislamu akina lipumba badala ya kukataa hiyo propaganda wakaikumbatia wakidhani kuwa waislam wote sasa wataiunga mkono. Ukilinganisha na CHADEMA baada ya kupakaziwa kuwa ni cha kikristo, Chadema imekanusha na kulaani kwa maneno na vitendo. Kitu kingine Chadema imebadili sura ya wenyeviti mara kadha wakati CUF Lipumba antaka kuifanya kuwa kampuni lake. Pili chadema wanaonyesha wana strategists waliosmart sana.
 
wa2 wa Igunga wameshatoa tamko kwa niaba ya waTZ...
CUF inabidi wajipange upya...
 
0. Kwa sheria ya Uchaguzi, wasimamizi na mawakala wa uchaguzi wanaruhusiwa kupiga kura kwenye vituo walivyopangiwa kuvisimamia, lakini cha kushangaza zaidi ya vituo 30 chama cha CUF hakijapata kura hata moja, hii inamaana hata mawakala wao wameipigia kura CCM, hapa tunajifunza nini, ona kilio cha Mtatiro hapo chini, hivi inamaana hajui ni kitu gani kinaendelea CUF, au anatufanya malimbukeni, asanteni CUF kwa ushirikiano wenu.


1. Waliingia mufaka na chama tawala nakupoteza muonekano wa kiupinzani hadi kufikia hatua ya kuitwa Chama B, kwa kweli sasa hivi umaarufu wao umeshuka sana hasa Tanzania bara.

2. Wamekuwa wakikishambulia sana chama cha upinzani cha CDM kama vile wao siyo upinzani

3. Hata baada ya kuona kuwa nafasi yao ya kufanya vizuri igunga ilikuwa ni ndogo sana lakini hawakutaka kuwapa nafasi wenzao wa CDM walioonekana kuwa na ushawishi kuliko wao kana walivyofanya NCCR

4. Walidai kuwa walikuwa na mtaji wa kura zaidi ya elfu kumi, 10,000 katika jimbo la igunga kitu ambacho hawakutilia maanani ni kuwa kati ya kura hizo 10,000 ni za watu wasiokuwa na mapenzi na chama tawala na si kuwa watu hao ni CUF

5. Walipokuwa Igunga waliwapiga vijembe na kuwashambulia wapinzani wenzao hadi hatua ya kukunjana mashati kati ya mgombea wao na wanachama wa CDM



Lazima nikiri kuwa washindani wetu wakubwa CCM na CHADEMA wametushinda katika uchaguzi mdogo wa Igunga.

Kwa matokeo ambayo nimeyashayapokea kutoka kwenye asilimia 88 ya vituo kwa ujumla tumefanya vibaya sana. Japokuwa tumekuwa na mgombea mzuri sana na tumemnadi kwa kutumia uwezo wetu wote ambao kwa hakika kila mtu ameuona, lakini matokeo hatuwezi kuyageuza.

Ninachojifunza zaidi ni kuwa wapiga kura wengi ndani ya Tanzania bado wanaamini zaidi propaganda kuliko hali halisi ya mazingira yanayowakabili na hii ikizidi kushabikiwa ndivyo ambavyo wananchi watakosa fursa bora siku za mbele.
Ikiwa hali hii itaendelea hivi ina maana bado nchi ina safari ndefu ya kufikia demokrasia ya kweli na maendeleo yatakayoonekana kwa macho.

Katika uchaguzi huu wa Igunga CUF tumepambana na changamoto kubwa ya kujibu propaganda zilezile kuwa eti "Sisi ni CCM B", kila tulikoenda tumekutana na kikwazo hiki, tumejaribu kwa dhati kuwaelimisha wananchi bila mafanikio na muda umekuwa ukikimbia kuliko upepo.

Hata hivyo bado naamini kuwa tutapata fursa kubwa ya kuwaelimisha wananchi siku za usoni. Mimi na wenzangu hatutakata tamaa kwani MAFANIKIO KATIKA NYANJA YA SIASA huhitaji mioyo migumu.

Natambua kuwa uongozi ni dhamana nzito inayohitaji kujipanga zaidi na zaidi, Na CUF itazidi kujipanga zaidi na zaidi na kila tutakapoanguka tutanyanyuka na kuanza safari, hakika TUTAFIKA.

Chama changu kinakabiliwa na changamoto kubwa sana mbele ya safari na kwa hakika inahitaji tuzidi kujipanga na kujiimarisha. Kama chama hatutajilaumu kamwe, tumeonesha uwezo mkubwa na kufanya kampeni sahihi tukiwa na mgombea wa kiwango kizuri kwa mpiga kura yeyote anayehitaji kiongozi. Lakini kusimamisha mgombea mzuri na kufanya kampeni nzuri wakati mwingine siyo sababu ya kufanya vizuri. Maamuzi ya nani awe mbunge, ni mzuri au mbaya, anafaa au hafai yako kwa wananchi.

Wananchi wa Igunga tunawashukuru kwa namna walivyotuunga mkono na tunawaomba wawe kitu kimoja katika kuiendeleza Igunga yao kwani mshindi akishatangazwa yeye ni mbunge wa wananchi wote. Vyama vyetu hivi vipo ili kuisaidia jamii kupata kiongozi mzuri tu, nasi kama chama tumetimiza wajibu wetu.

Mimi kama kiongozi wa ngazi ya juu wa CUF - Tanzania Bara(Bila kujali nimekuwa kiongozi wa ngazi ya juu miezi minne tu iliyopita tu) nabeba dhamana kwa matokeo yote tuliyopita, najitwika mzigo wa kusimama imara kuiimarisha CUF. Sitatoka CUF na kukimbilia kwenye vyama vyenye nguvu Tanzania bara kama CHADEMA n.k. eti kwa sababu tu CUF imefanya vibaya kwenye uchaguzi. Ninaamini katika CUF na nitaisaidia Tanzania yangu nikiwa CUF, ninaamini siku moja wakati CUF imeimarika nitatajwa kati ya watu ambao hawakukata tamaa na hawakuyumbishwa na magumu yaliyowakabili na walisimama kidete kwenda mbele.

Tunawashukuru wale wote waliotuunga mkono katika uchaguzi huu na wale wanaotuunga mkono siku zote na wale watakaotuunga mkono siku zijazo. Kwa hakika wote tunawashukuru sana na CUF itasimama imara.

Mungu awabariki sana.

"HAKI SAWA KWA WOTE"

Julius Mtatiro,
Naibu Katibu Mkuu,
Chama Cha Wananchi - CUF,
Tanzania Bara,
02 Oktoba 2011,
Igunga - Tabora.
 
Kwa mwenye akili timamu yeyote, alikuwa anajau kuwa CUF haiwezi kushinda kwa njia yeyote Tabora, wanyeji wa mkoa huu ni welewa na welevu saana, hawawezi kupigia kura chama kinachofadhiliwa na nchi jirani Zanzibar.

Matokeo ya Igunga ni barua tosha kwa CUF, hatuwataki bara
 
Kuna jamaa yangu mmoja anafanyia kazi Igunga vijijini na alikuwa CUF damu (na alikuwa akijinadi kama mwanamageuzi) alinipigia simu kunieleza kwa uchungu mkubwa kwamba yeye na wenzake karibu wote kwenye eneo wanaloishi waliamua kujiunga na CHADEMA baada ya kuwasikiliza CDM wakifafanua sera zao na kushuhudia kwa masikio na macho yao CUF wakiungana na CCM kuwaponda CHADEMA. Anasema walibaini kuwa CUF si chama cha upinzani na kuthibitisha tuhuma za chama hicho kuwa kibaraka wa CCM.
CUF na vyama vingine vya upinzani viwe makini kujibainisha na hoja za CCM haswa kwa wakati huu ambapo CCM wamepoteza kabisa jina na mvuto.
 
Chama cha Wananchi CUF, kinawiwa na wanachama wake tamko mahsusi kuwa ni nini hatma yake kwa sasa. Uchaguzi wa Igunga unafanyika katika mkoa ambao anatokea mwenyekiti wa chama, pamoja na mbunge wake wa viti maalumu. Kwa nguvu waliyoiweka CUF ikiwemo kumleta makamu wa raisi wa SMZ, wabunge, viongozi waandamizi na bila kusahau kutumia helicopter, naamini matokeo ya leo is the best thay can expect kwa uchaguzi wowote utakaofanyika Tanzania bara.

Vipo vyama vilivyowahi kuvuma na kuporomoka kikiwemo NCCR-mageuzi. Tofauti na CUF, sababu za kuporomoka kwa vyama hivi ilikuwa wazi, hususani migogoro ya uongozi na ukata. Ila kwa CUF, sababu ya kuporomoka kwake haiko wazi; uongozi ni ule ule, ruzuku imeongezeka, tena wamepewa na sehemu ya serikali kule Zanzibar. Tulitegemea CUF kionyeshe kuaminika zaidi na wananchi, hivyo kiwe chama kikuu cha upinzani!!!

Sio siri, ni halali yao wanachama na wapenzi wote wa CUF kupata maelezo ya kina, ni kwa nini chama hakifanyi vizuri...

Kwa heshima na taadhima, namwomba ndugu Julius Mtatiro pia atoe maoni yake juu ya matokeo ya Igunga, na juu ya mustakabali wake kisiasa. (Ingekuwa heri leo asikie sauti ya wananchi, asifanye mgumu moyo wake).
Mkuu kweli wewe kiboko, I like your strategy.
Yaani kelele zooote zile za CDM inashinda na leo matokeo umeyajua na sasa unajaribu kudivert kushindwa kwa CDM kwa kuhoji kushindwa kwa CUF na blah blah nyiingi.

CDM na CUF vipo sawasawa kwa maana ya sura ya muungano,
CDM hawana hata jimbo moja Zanzibar na wanakubalika zaidi bara
CUF hawakubaliki zaidi bara kama wanavyokubalika zanzibar
The good things kwa CDM ni kwamba upande wanaokubalika wao kuna wapigakura wengi kuliko upande wanao kubalika CUF

Katika kata 22 CDM wameambulia kata 3 tu, najua ni rahisi sana kwa CDM kujitetea wameibiwa kura ila kwa CUF watoe maelezo kwanini wameshindwa
Thats so fun..............
 
ilianza na busanda,halafu hapa igunga,kwa chama kama CUF inahitakiwa wakae chini na kujiuliza nani kawaloga,kupata kura moja vituoni au sifuri na sijaona wapi wamepata kura zaidi ya kumi wakati mwaka jana walikuwa no 2 baada ya ccm inatisha hali hii.katika mikutano walikuwa wanajaza watu,mashine kama jussa,mtatiro,maharagande,mketo nk zote zimeshindwa tena baada ya busanda,na hata hapa.kipi kimeikummba CUF marehemu?
 
Cuf na Mtatiro watengue ndoa yao na Magamba ndo waanze kukijenga chama,Tuliwashangaa sana kuona wanawashambulia sana wapinzani wenzao baadala ya chama tawala,Mimi nadhani ni wafuasi wazuri wa Magamba,
 
Umeandika hii article bila ya uchambuzi wa ukweli. CUF ina mafanikio zaidi ktk vyama vya upinzani. Angalia Wabunge waliokuwa nao, na sasa hivi wanayr Makamu wa Rais.

Sasa huoni kama hiyo ni progress?


we ndo umetoa comment bila kutafakari.ni progress ipi cuf yameifanya bara km co kuporomoka kisiasa.nachowashauri cuf wang'oe nanga bara wabaki zanzbar huku hawapawez
 
Back
Top Bottom