Baada ya mapenzi

Nyani Ngabu

Platinum Member
Joined
May 15, 2006
Posts
97,076
Reaction score
136,490
Binadamu bana!

Watu wakiwa kwenye lindi la mapenzi huwa wanaonana wazuri sana.

Unakuta labda mdada anamsifia sana jamaa alivyo mzuri.

Anakuwa na majigambo ya hapa na pale. Kwamba hataki wadada wenzie waone hata picha zake kisa anahofia kuibiwa kwa sababu jamaa ni 'mzuri', kwa mujibu wake.

Sasa penzi likishachuja na wahusika kumwagana, ghafla yule alokuwa mzuri eti anageuka kuwa mbaya.

Utasikia 'oh mtu mwenyewe kwanza mbaya', 'mtu mwenyewe wala sio mzuri', mtu mwenyewe ana kibamia, mtu mwenyewe ana matege, mtu mwenyewe hivi, mtu mwenyewe vile.

Hilo limenipelekea niwaze hivi ni maneno yepi ambayo ndo huwa ya kweli?

Ya wakati penzi limekolea au ya wakati penzi linapochuja?

Pia kauli kama hizo ni moja ya uthibitisho kuwa mapenzi bila uongo uongo nayo hayataenda vizuri.

Wakati mwingine labda huwa inambidi mtu amdanganye mwenzake walau kidogo tu ili mapenzi yao yaweze kwenda bila mushkili.

Wadau nyie mnalizungumziaje hilo suala?

Mshawahi kuwa 'wazuri' pindi penzi limekolea lakini mkaja kuwa 'wabaya' baada penzi kuchuja au kuisha?
 
Inategemea ntu na ntu.
Mie kuna ntu nilimwacha lakini siachi kumsifia jamaa ni handsome kweli na yuko vizuri kwa game lakini kitu kidogo tu tulishindwana na ni rafiki yangu bado tunajadili Mambo kadhaa ya maisha ingawa kila mmoja alisha move on
 
Wanasemaga.."mapenzi ni upofu"

Chongo utaaita kengeza...

Kiuhalisia ukimpenda mtu kwa dhati na ukakolea haswa huwezi kuona kasoro yeyote kwake...

Hata ukishuhudia 'baya'lolote kwake akili yako itakuambia kuwa ni zuri.

Do not underestimate "the power"of love.
 

Huo upofu hupona baada ya kuachana au?

Maana watu wakishaachana ndo utasikia kila lililo baya la mtu.
 
Huo upofu hupona baada ya kuachana au?

Maana watu wakishaachana ndo utasikia kila lililo baya la mtu.
Na'am,ndio maana likatumiwa neno "mapenzi",hayo mapenzi au mahaba yanayokuwa yamezijaza nyoyo za wapendanao ndiyo yanayotia upofu,na pengine na ukiziwi kabisa,'cause mtu akipenda bhana,unaambiwa 'pale hasikii wala haoni'...
Na pindi yakiondoka basi upofu nao unaondoka mtu anaanza kuona bayana yale yaliyokuwa yamefichwa na mapenzi. Hapo ndo unaanza kuona yale mapungufu yaliyokuwa yamefunikwa na mapenzi...
 
baada ya kuachana wengi huona kuwa wenza wao walikuwa wabaya kuna m1 aliwahi kusema humu ndanh eti simtaki yule bata mweusi khaaaa! really??!
 
Binafsi nafikiri ni kwamba kwa wanawake wengi huwa hawaoni kasoro za mwanaume au anaona ila anapotezea kwa makusudi ikiwa huyo mwanaume ana pesa na anamwezesha kwa mengi.

Kwa sisi wanaume mara nyingine unaweza kumpenda binti kwa muonekano au kigezo flan mfano mwenye "CHURA" la ukweli au mwenye sura nzuri kisha unamtumia kwa muda flan halafu unakuta anayemzidi viwango.

Sasa hapo kuna Wanaume wenye tabia ya kuwaponda hao maduu au wengine kukaa kimya tu.

Hatahivyo, hii tabia ipo zaidi kwa wanawake na sio tabia nzuri kiukweli.
 
Nikuruhusu emotions zikuendeshee tu.

Haha..kuna binti mmoja tulimwagana. Alikuwa kaweka kichwani phone number yangu basi hasira zikimpanda ananirukia hewani ananitukaaaana akimaliza anakata simu analala

I never reacted or kumjibu matusi yake. Leo hii kawa rafiki yangu na misamahaa kibao.
 
Kweli kabisa!

Ila sio kila mapungufu huongelewa mengine tunapaswa kuyamezea tu!maana aibu itakukuta na wewe pia mpondaji!
 
Duuuhhhh, kazi kweli kweli.

Kumuongea vibaya au kwa mabaya mpenzi wako wa zamani ni sawa na kujivua nguo. Wahenga walisema "ndege wafananao huruka pamoja".

Kama huyo aliekuwa mpenzi wako ni "kichaa" Basi hata wewe ni "kichaa " pia sema chako hakijakolea vizuri.
 
Upendo hauhesabu mabaya, Upendo hufukia ubaya wote wa mtu.
Ukimpenda mtu na ukadhamiria haswa kumpenda kamwe hutoona wala kuhesabu ubaya wake.
Wahenga wanaposema amri kuu ni upendo maana yake ktk upendo ugomvi na aina yoyte ya chuki na kadhia haviwezi tamalaki.
Ila kinyume chake ndio kuanza kuhesabiana madhaifu baada ya upendo na mapenzi kuisha.
 
Kaka ktika hao wawil atakae ongea sana ndo ameumia zaid anapo sema ww n mbaya ujue huko ni kutapa tapa tu....na anajarib sana kusema na akili yake ikuone mbaya lakn akil ya kwanza iliyo sema ww n handsome ndo jib kabisaaa.....mengn ni kuhangaika tu....ndo mana utakuta anajiuliza kila mahali ili kusaidiana na akil za wengn uonekan mbaya....wat watasema jamaa kakosea tu ila sio mbya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…