Tundu Lissu, Mbowe, Maalim Seif, n.k. mmoja wao akirudi ccm basi Itakuwa ndiyo mwisho wangu mimi kupenda demokrasia, nitaachana kabisa na ushabiki wa kisiasa
For sure huyu jamaa Ana laana ya wanakigoma kwani Kuna baadhi ya wazee walimlaumu sana pale walipompigania kama kijana wao ili akawawakilishe lkn nipale tu alipoupata ubunge akahama mtaani akaenda kula maisha mjini na kuwatosa kabisa timu yake pamoja na dharau hapo sasa nao wakafanya kazi yao kuhakikisha hashindi hata kama kaamia Kwenye Chama cha role model wao... Kiujumla ni mlafi wa madaraka na kwa Mujibu wa lecturers wake, alikuwa mtu wa kubebwa lkn huwa anasahau alipotoka.
Laana ya usaliti inawatesa, tulisema na kuwatahadarisha hawa wanasiasa Vijana waliopata umaarufu mkubwa kuwa ktk mafanikio waliyokuwa wamepata walipaswa kutulia na kuwafanyia Wananchi waliyowakubali kazi, wao wakaanza kung'ang'ania madaraka... Langu jicho tutasikia mengi
Nilivyoona historia yake kwamba alianzia CCM then akaenda TLP then akaenda CHADEMA then NCCR then ACT then sasa. CCM wala sikushangaa.
Mtafuta maslahi huyu.
Tundu Lissu, Mbowe, Maalim Seif, n.k. mmoja wao akirudi ccm basi Itakuwa ndiyo mwisho wangu mimi kupenda demokrasia, nitaachana kabisa na ushabiki wa kisiasa
usikate tamaa hata kama wakirudi, demokrasi ni sawa na ushabiki kama wa simba, yanga, liverpool, arsenal, n.k. hata kama club itafungwa mabao mengi au kushindwa kutwaa kombe kwa miaka 50 watu wanabaki upande huohuo tu. Ninachoamini mimi wajinga wanazidi kupungua na warevu wanaongezeka kila siku nchini kutokana na matukio mbalimbali nchini na kimataifa.
...kila mtu anayo haki kamili ya kujiunga na chama cha siasa atakacho lakini ni kweli Machali anaipenda CCM au kuna kitu kilichomsukuma kurudi CCM? ni kitu gani hasa hicho?. Hakuna asiyebandikwa bei mgongoni!!