Kumbukeni JK aliwahi kusema u-Rais wake hauna ubia na mtu yeyote! Labda alikuwa ana maana hiyo. Kwamba ni ubia wa kifamilia na maswahiba wachache! Jamani kinachonitisha sio hiyo staili ya kampeni, ila AHADI LUKUKI ANAZOTOA. Eti katika muda wa miaka mitano tu atajenga reli kutoka Dar hadi Mwanza....! Ile reli ya wakoloni kutoka Tanga hadi Arusha vipi imekufa? Ujenzi wa Reli wa miaka mitano tena kwa fedha za Serikali sijapata kuona katika nchi za Afrika! Tusubiri tuone. HILO ZIGO LA AHADI ZISIZOTEKELEZWA ATAACHIWA NANI NDANI YA CCM AHANGAIKE NALO? Maana kuna daraja la Kigamboni, meli mpya ziwa victoria, meli mpya ziwa nyasa, mabarabara ya lami mengi mpaka vijijini kama kule Lupembe, Njombe![/QUOTE
Kibeka Senzela, tafadhali kuwa kama "mbayuwayu" Sasa hivi muungwana anatafuta kura kwa wadanganyika ili abaki ikulu. Baada ya 2015 itakula kwetu. Hatakuwepo kwenye mchakato wa urais hivyo hakuna wa kumuliza mbona hatuoni Mv Bukoba mpya, mbona hakuna barabara ya lami au international airport pale Bukoba na Kigoma etc. Ahadi anazotoa ni danganya toto. There is neither an aorta or vein of truth in his many promises.