G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,555
- 35,880
Niweke kumbukumbu sawa, nilishaamua kuhusu ubunge na udiwani.
Haya ninayasema kwa dhati kabisa baada ya kusikiliza hotuba ya Slaa na kupitia chunguzi mbalimbali!
Mnamo siku ya jumanne Slaa alitoa hotuba yake iliyojaa tuhuma mbalimbali dhidi ya Gwajima, Maaskofu 30 wa kanisa katoliki, Lowassa, Masha na Sumaye.
Niliitafakari sana hotuba ile na baada ya kushindwa kupata uhakika nikaingia kwenye vyombo vyangu vya uchunguzi vilivyo ndani ya familia mpya ya Slaa kupata uhakika!
Kuna swali moja ambalo mimi nilijiuliza siku ileile na baadaye nimemsikia Tundu Lissu kwenye redio moja ya kimataifa akiuliza swali hilohilo "Kwanini sasa? " "Why now? "
Naomba nithibitishe kuwa mtu wa kwanza kabisa ndani ya Chadema kuwasiliana na Lowassa ni Slaa! Yeye ndiye aliyepanga mipango yote wakishirikiana na Gwajima.
Slaa aliendelea kuwa karibu na Gwajima huku akimshawishi awe karibu sana na Lowassa kumshawishi kwa hali na mali ahamie Chadema endapo ATAKATWA!
Asipokatwa itakuwaje?
Baadhi yetu tulijua na tulikuwa na uhakika kuwa ni lazima Lowassa akatwe! Alikatwa kabla hajachukua fomu CCM, alikatwa kabla ya kutangaza nia ya urais ndani ya CCM. Hivyo hilo tulikuwa na uhakika nalo!
Mbowe alijulishwa baadaye sana kuhusu ujio wa Lowassa. Asishutumiwe kuwa aliiuza Chadema kwa Lowassa! Tena niwahakikishie kuwa Mbowe alishtuka sana kusikia maneno ya kumkaribisha Lowassa yakitoka kinywani mwa Slaa!
Nini tatizo?
Slaa alikosea sana kufanya mambo haya bila kumshirikisha Josephine (mwenza wake) katika hatua za awali kabisa! Josephine alikuja kukasirika sana baada ya kuona picha (nasisitiza tena kuona picha) za Lowassa akiwa na viongozi wa Chadema akiwepo Slaa!
Josephine baada ya hilo akakengeuka na ikawa ni jino kwa jino kati yake na Slaa. Akaanza mipango.
Kuna thread moja niliileta humu nikiwatuhuma mke wa kigogo mmoja wa Chadema pamoja na kigogo mmoja wa CUF wakitumiwa na CCM kuhujumu UKAWA! Hiyo mipango niliipata kutoka kwa mtu wa karibu wa Sofia Simba na bahati mbaya sana ile thread mods waliichomoa ndani ya sekunde 30. Ilikuwa siku ambayo Magufuli alienda kuchukua fomu tume ya uchaguzi.
CCM walifanikisha mipango yao dhidi ya watu hao wawili kwa unafuu sana! Hawakuamini! Sasa ikabaki kwa Slaa (hilo jukumu aliachiwa mwenza)
Baada ya hapo nilichokishuhudia ni kama hivyo! Nilijua kuwa Slaa angeachana na siasa lakini sikufahamu kama ameongea vile! Hilo ndilo hasa dhumuni langu!
Kwanini sasa? Kwanini isiwe ndani ya kamati kuu ameyasema haya ili waamue kama kweli Slaa anakipenda chama alichokitolea jasho na damu? Kwanini baada ya Chadema kukamilisha taratibu zote za tume? Ila wakati tukijiuliza hayo tuweke kumbukumbu sawa kuwa engineer wa kumleta Lowassa Chadema alikuwa Slaa! Kwanini sasa? Kwanini isiwe ndani ya vikao vya chama kama alitaka kukinusuru chama? Maana tuhuma zote alizotoa zilikuwa ni za zamani sana kabla Lowassa hajaanza hata harakati za urais, hivyo alikuwa na ushahidi wa kutosha kabisa kuupeleka ndani ya vikao vya chama! Kwanini sasa?
Pia tuelewe kuwa kwenye hotuba ya Slaa alijichanganya sana! Kuna sehemu anasema wazi kuwa alikuwa na ushahidi wa kutosha kuwa Lowassa siyo msafi. Hapohapo anasema kuwa alitaka kwanza Lowassa aeleze ukweli wote kuhusu Richmond ndipo apokelewe Chadema! Utamtakaje mtu ajisafishe kwanza huku ukiwa na ushahidi wa waziwazi kuwa ni mchafu? Hiyo ni hadaa!
Pia zipo sehemu kwenye hotuba yake alionyesha chuki za waziwazi! Mimi nikajiuliza tena, uswahiba uliotukuka kati ya Gwajima na Slaa ulikufa lini? Hawa watu walikuwa marafiki hadi mambo ya familia walikuwa wakishirikishana!
Nini tatizo?
Ni nguvu ya mwenza! Slaa alitekwa na mwenza. Mwenza alifanya mipango hiyo chini ya miongozo maalum kutoka ndani ya 'system'
Slaa kwa sasa ni mtumishi halali wa CCM! Na ataifanya kazi hiyo hadi October 24!
Mimi G Sam nimetafakari sana kuhusu Lowassa! Kama kweli angekuwa mtu hatari hivi kama tunavyoaminishwa kwa nguvu kila kona basi angekuwa ameshaozea jela! Nilishagundua kuwa hizo zote kwa Lowassa ni chuki tuu! Nilikuwa na tatizo moja kuhusu Lowassa kulimiliki jukwaa ila kuna kitu nimejifunza na nitakuja kuelezea huko mbeleni! Kwasasa kura yangu ni kwa Lowassa! Sitothubutu kubadilisha maamuzi yangu haya!
Kwa sasa nimeachana kabisa na siasa za Slaa na sitokaa nitoe tena kitu kutoka kwake! Sitokaa tena nijifunze siasa zake! Chama kilichokulea na kukufanya ufike hapo ilipo huwezi kukisemea kama alivyofanya Slaa! Alitaka chama kibomoke eti kwa kuwa sasa hana tena maslahi nacho? Amesahau haraka hivyo alipotoka? Huu ni zaidi ya usaliti!
Niishie kwa kusema kuwa kwa sasa Slaa sitokaa nimuite tena dokta!

Last edited by a moderator: