Baada ya kusikia mama anampa Benzi mzee nimeukumbuka wimbo wa Mjomba

Juzi hapa Magufuli kampa Mzee Mwinyi Hekalu

Leo Samia anampa Benzi

Nani kakwambia Mzee Mwinyi hana uwezo wa kujinunulia gari kwa fedha zake?

Kama Samia ameguswa sana na hali ya Mzee Mwinyi, basi akope gari kwa mshahara wake binafsi ampe zawadi lakini siyo kuchukua mali ya wananchi na kugawa kama pipi.

Kuwa rais haimaanishi mali ya serikali ni yako na unaweza kuigawa utakavyo!

Hili litukumbushe Umuhimu wa Katiba mpya, Katiba hii inamfanya rais afikiri nchi ni mali yake binafsi!
 
Hii ni kukosa uelewa. Rais Mstaafu, na viongozi wengine wa juu, wakiwemo majenerali wa Jeshi, wanapewa gari la kutembelea la serikali. Likichoka linabadlishwa. Linaweza kubadilisjwa mapema kwa mahitaji maalum kama haya ya Mwinyi. Nahisi hilo ndilo lilizungumzwa na Samia. Fanyeni uhakiki wa taarifa kabla ya kutoa lawama
 
Hivi hili gari angepewa Hayati Nyerere mngeongea? Tuache unafki! Tuache udini! Tuache ubaguzi wenye misingi yeyote!
 
Benzi LA nini jamani wakati tayari ana nagari ya serikali yabayomhudumia? Sasa Benzi kwa mzee WA miaka 96 la kwenda nalo wapi?
Ila wabongo tuna nongwa sana, mbona mama kasema sababu ya kumpa gari la chini? Mwinyi miaka imeenda sana, 96 hebu tuweni waungwana japo kidogo
 
Hii ni kukosa uelewa. Rais Mstaafu, na viongozi wengine wa juu, wakiwemo majenerali wa Jeshi, wanapewa gari la kutembelea la serikali. Likichoka linabadlishwa. Linaweza kubadilisjwa mapema kwa mahitaji maalum kama haya ya Mwinyi. Nahisi hilo ndilo lilizungumzwa na Samia. Fanyeni uhakiki wa taarifa kabla ya kutoa lawama
Nafikiri Mama karibu kueleza sababu yenye mashiko pia,iliyomsukuma kumzawadia gari hilo la chini...Sioni ubaya kivile na iwe ajabu kama wakurugenzi tu, mmeridhia wajimwaye na maV8/VX ya Bei, sasa hiyo zawadi ya Mzee wetu Mwinyi naye naona tumwache azeeke 'graciously' na wajukuu zake.
 
Hii ni kukosa uelewa. Rais Mstaafu, na viongozi wengine wa juu, wakiwemo majenerali wa Jeshi, wanapewa gari la kutembelea la serikali. Likichoka linabadlishwa. Linaweza kubadilisjwa mapema kwa mahitaji maalum kama haya ya Mwinyi. Nahisi hilo ndilo lilizungumzwa na Samia. Fanyeni uhakiki wa taarifa kabla ya kutoa lawama
Kukanusha taarifa ya mwenzio bila kutuonyesha nukuu ya hiyo sheria inayo tetea hoja yako tunakuona km chawa wa huyo unaemtetea.
 
Hivi hili gari angepewa Hayati Nyerere mngeongea? Tuache unafki! Tuache udini! Tuache ubaguzi wenye misingi yeyote!
We ndo unaleta udini. Kwa taarifa yako hakuna Rais mstaafu anayependwa na Watanzania kwa sasa km Mzee Mwinyi. Mzee ni mstaarabu na hana nongwa na mtu.

Watu wanahoji ni wapi Katiba imeagiza Rais mstaafu apewe Benz? Tukifumbia macho haya ipo siku atatokea Rais kichaa akampatia mwenzake eneo la mkoa.Na km katiba imeagiza alafu hakupewa siku zote toka astaafu basi huo utakuwa ni uzembe wa hali ya juu.
 
Kukanusha taarifa ya mwenzio bila kutuonyesha nukuu ya hiyo sheria inayo tetea hoja yako tunakuona km chawa wa huyo unaemtetea.
Kwa hiyo unataka mzee wa watu wakati wa kupanda V8 suruali ichanike?
Mama kosa ni kutangaza lakini wastaafu wanapewa usafiri na serikali.
 
Hii ni kukosa uelewa. Rais Mstaafu, na viongozi wengine wa juu, wakiwemo majenerali wa Jeshi, wanapewa gari la kutembelea la serikali. Likichoka linabadlishwa. Linaweza kubadilisjwa mapema kwa mahitaji maalum kama haya ya Mwinyi. Nahisi hilo ndilo lilizungumzwa na Samia. Fanyeni uhakiki wa taarifa kabla ya kutoa lawama
Angesema " NAAGIZA GARI YA MZEE MWINYI IBADILISHWE"
 
Tunaanza kulinganisha wanachopata majenerali, mara Nyerere mara wakurugenzi na V8s n.k

Hoja ni kwamba, Raisi wa JMT ametoa zawadi kwakuwa Mzee Mwinyi, kwa umri wake, inampa shida kudandia migari ya juu(SUVs).

Lini hawa viongozi wamebadilishiwa magari yao ili tujue ni katika huo utaratibu au hii ni huruma ya raisi kwa raisi mstaafu tu!

Mzee Mwinyi anao wajibu wa kujiangalia mwenyewe na kujua mahitaji yake, kwasababu ya madhira ya uzee, mke wake anaweza kusaidia hilo, wote wakiwa ukurasa mmoja, huyu Mzee ana watoto wangapi? Hawajui madhira ya uzee wa wazazi wao? Na hapa si tu kwa Mzee Mwinyi, bali wale wooote waliojiweka kwenye mstari wa kuneemeka na nguvu za watanzania isivyo halali.

Mkurugenzi anatembelea V8 akiwa kwenye utumishi, ni sawa. Akistaafu je? Anapewa hiyo 80% ya mshahara wa aliyepo kazini?

Eti ni wazee wetu, waenziwe, kwa lipi sasa? Watanzania tulifanya maombi na dua kuomba fulani awe raisi? Hawakuenda kuchukua fomu tena kwa kulipia kuuomba huo urahisi? Pengine kurogana, kuuana, kuhonga n.k ili waupate huo uraisi. Unadhani kwaninj walifanya yote hayo? Ili kujitolea?

Daktari akitibu mtu, ndio jukumu lake, askari akimkabili jambazi, ndio jukumu lake, zima moto wakifanya uokozi kwenye moto, ndio jukumu haswa, rubani akirusha na kushusha ndege salama, haitaji sifa yoyote n.k Ila hawa wote, wakienda kimya kimya kwa wasiojiweza, yatima pengine na wazee, wakawapa misaada ya hali na mali, wanastahili WOW kwasababu sio jukumu lao la kimkataba.

Miaka 10 ya kufaidi nchi, kutokulipa kodi na kinga kedekede za maovu kisha bado tu utuumize? Na yule mwalimu anayepambana miaka 36 kule Nanjilinji, anayekatwa kodi na kuchangia mafao yake kisha akistaafu umzungushe miaka nenda rudi KISA hao mabwanyenye yenye kila privilege, watoto wao kunufaika na kuendelea kujiweka kwa nguvu ya jina!

Kazi iendelee
 
Umeandika kwa hisia sana.

Watu wanataka tuwalipe wastaafu kwa kutimiza wajibu wao ambao tulishawalipa walipokuwa kazini anyway!, tena hadi kodi tuliwaondolea!

Yazni wanataka Watanzania tufanye double payment kwa huduma tuliyopewa!
 
Back
Top Bottom