Baada ya kushinda Urais, Je Lowasa angeweza kufanya haya??

Mwasita Moja

JF-Expert Member
Dec 31, 2015
2,903
2,580
Wote tumeona kasi ya Rais Magufuli ndani ya mwaka mmoja wa utawala wake.

1. Kufukuza majizi yote ndani ya serikali na kukimbilia chadema.

2. Kufukuza majizi yote bandarini na kufunga kamera kila sehemu

3. Elimu bure

4. Makusanyo ya kodi kuongezeka

5. Flyovers kila mahali

6. Heshima ya Tanzania kurudi kimataifa

7. Kufutwa kwa safari za nje

8. Kufutwa kwa mgawo wa umeme nchini.

Kama angeshinda Lowasa angeiweza hii kasi ya Magufuli? Kama sasa hivi chama chake kiko bize kutetea wakwepa kodi na mafisadi, je kama angeshinda angeweza kupambana nao??
 
Utakuwa mbibi / mbabu mpaka umepoteza kumbukumbu;

- Lowassa ndiye aliyepigania shule za kata,elimu bure na bora mpaka chuo kikuu.
- Lowassa alipokuwa waziri mkuu alipigania uwajibikaji na uwazi bila kudumaza na kuupinga utajiri kwa wivu wakijinga.
- Lowassa alipigania maji safi na salama toka ziwa victoria bila kuogopa maarabu koko.
- Lowassa alipambana kuhakikisha nchi haiingii gizani lkn akapotoshwa na rahisi zaif wawakati ule.
- Lowassa alifuta nakufurusha kampuni la maji city water ya uingereza bila kigugumizi.

Unapotaja watu mahiri Tanzania huwezi mwacha huyu mpambanaji mcha Mungu licha ya ajali ya kisiasa aliyotengenezewa...wengine tulitaka Ccm ianguke siyo yeye kutolewa chambo.

UMENISHANGAZA NA. 5, HIVI KUMBE KUNA FLYOVERS KILA MAHALI?? KWA UONGO HUU HATA SHETANI ATACHUKIA KHAA! SIFIA KIASI ASEE.
 
Lowassa ana HEKIMA na BUSARA, hawezi kukurupuka hovyo na kufanya maamuzi bila kuchanganua mambo kwanza.
 
Lowassa ana HEKIMA na BUSARA, hawezi kukurupuka hovyo na kufanya maamuzi bila kuchanganua mambo kwanza.
Nyoosha maelezo vema kamanda, sema kwamba luwassa yuko smart kwenye dili na ndio maana hadi leo taifa bado linagugumia kwa ufisadi wake wa richmond!
 
Nyoosha maelezo vema kamanda, sema kwamba luwassa yuko smart kwenye dili na ndio maana hadi leo taifa bado linagugumia kwa ufisadi wake wa richmond!
Luwassa ndio nani?

Yupo smart kwenye Dili kuliko MZEE WA CCM, YULE WA VIJISENTI?

Je Mzee wa Bil 75 za ESCROW?
 
sidhani kama lowasa angeruhusu mkuu wa mkoa avamie clouds tv kisha aachwe tu. pia lowasa asingelinda wakuu wa mikoa wanaofoji vyeti.pia lowasa asingechezea elimu yetu kwa kuruhusu walimu wa sekondari kwenda kufundisha shule za misingi kuliko kuajiri walimu wapya wa msingi waliojaa mtaani. lowasa angefanya mengi mazuri kuliko magu.
 
Ongeza 10. Kuongeza wakuu wa Mikoa wafoji vyeti na majina bandia(mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam - Paul christiani Makonda (jina bandia) badala ya Daudi Albert Bashite (jina halisi). Hii haijawahi kutokea isipokuwa awamu ya tano tu!

11. Kuongeza kasi ya ugumu wa Maisha kwa raia wasio na hatia ( mdororo wa uchumi- economic recession)

12. Kuongeza kasi ya kuivunja katiba ya nchi- kupiga marufuku mikutano ya kisiasa

13. Kuongeza kasi ya kuminywa kwa Uhuru wa vyombo vya habari- matangazo ya moja kwa moja ya BUNGE

14. Kasi ya kuendesha nchi bila weledi- Raisi mwinyi aliwahi kusema nchi inaendeshwa kama gari bovu)
 
Back
Top Bottom