Watanzania kwa kupenda kuongelea watu na si kuongelea maendeleo, haki kabisa mna laana. Msijifanye nyinyi ni malaika msiokuwa na makosa au nyinyi ni miungu wa kutolea hukumu maandiko ya magazeti ya udaku?
Hili suala sio kuongelea watu, bali ni kuongea ukweli ili liwe fundisho kwa watu wenye tabia kama hizo na wewe ukiwemo. Hivi sio kweli kwamba huyo Mhe. alitenda hilo jambo pale Habour View a.k.a J' Mall ? Kulikuwa na sababu gani kuongea na simu ndani ya chumba cha ATM halafu alipoambiwa kama anaongea na simu apishe wengine akauliza Mlinzi kama hamfahamu yeye ni nani !!!! Ina maana huyu Mhe. aliongea na simu na kuchelewesha wengine makusudi bila kujali kuwa labda kuna mtu anataka kuchukua pesa na kumwahisha mgonjwa hospitali !!! Je, ufisadi lazima uwe wa pesa tu ??? Hata kukiuka
utaratibu nao ni ufisadi. Kiongozi yeyote akifika sehemu kama hiyo akasalimia watu, wakishamwona watamwabia atangule tu. Tatizo ni pale anapofika
Big Headed moja kwa moja hadi Counter !!!! Nimeshahudia wawili, tena wote Wamama (
mmoja Waziri na mwingine NW); mmoja (Waziri) aliiingia NMB Bank House akakuta watu kwenye foleni akawasalimia kwa kusema ....Jamani hamjambo ??? Watu wote walipogeuka na kumwona ni yeye kila mmoja alimwambia Mhe. tangulia na alipofika counter; Teller alimhudumiwa maana alishaona watu wakimruhusu kutangulia. Sasa siku nyingine nikapata bahati ya kumwona
Big Headed (NW); asiye fahamu kuwa uongozi ni utumishi wa watu na sio lazima ukiwa Kiongozi kila mtanzania anakufahamu !!!! alipofika hata hakusalimia mtu, akanyoosha moja kwa moja counter akipita katikakti ya mistari, ule wa withraw na ule wa Deposit si mnafahamu mambo ya bank house siku nyingine kunakuwa na nyomi !!!! Basi Bi. Dada mmoja akamvuta NW ili asiende mbele, kama kawaida NW akamwuliza hujui kuwa mimi ni NW wa ..................Bi. dada kama kapinda vile kamwabia huko huko ofisini kwako na UNW wako. Hata hivyo, NW aliweza kupenya na kufika kwa Teller ambaye aligoma kutoa ndururu mpaka taratibu zilipofuatwa.