Baada ya kuondolewa Uwaziri, Ngeleja akamuombe Msamaha mlinzi wa benki aliye mfukuzisha kazi

hataomba radhi maana kile huitwa kiburi cha uzima.mnakumbuka yule mheshimiwa aliyegaragazwa huko Mwanza akaondoa furniture kwenye ofisi ya Mbunge?Hawa shuleni walienda na vishahada walipata lakini ushamba na maisha ya ngumi mkononi yalibaki pale pale-Nachelea kutoa rai kuwa hawakuelimika!.Wewe Waziri gani anaenda kwa ATM halafu anapiga simu isiyoisha akijua wateja wengine wanasubiri na hakuna VIP status kwenye ATM?
Mheshimiwa Ngeleja sasa ni wakati wako wa kuokoka na kumpokea Yesu kuwa BWANA wa maisha yako,ukamtafute yule mlinzi umwombe radhi na pengine MUNGU ataghairi ili unusurike jimboni 2015,vinginevyo imekula kwako,laana iko juu yako Mheshimiwa!

Mambo ya ujana tena-kama kweli mlinzi wa watu alitimuliwa KAZI na mwajili wake basi mimi nataka kumpa Mh.Ngeleja usahuri wa bure - afanye juu chini amtafute mlizi huyo na amuombe msamaha wa kweli, na asihishie hapo ajaribu kumtafutia kibarua popote pale. Mimi nilipo sikia kwamba alikuwa anamfokea mlizi mbele za kadamunasi nilimshangaa sana, angekuwa kiongozi makini kitu ambacho angefanya ni kumpogeza mlizi kwamba anatimiza wajibu wake balabala na kumwambia politely kwamba samahani mimi ni waziri, nilijisahau nikazungumza kwenye simu muda mrefu na kusababisha foleni kwenye ATM, basi yakaishia hapo.

Ndugu Ngeleja huyu mlizi alipo timuliwa kazi ina maana uliathili familia yake, ndugu zake wanao mtegemea na wazazi wake, sasa unaona msululu wa watu walio athilika kutokana kutotafakali mambo, wewe unaweza kufikili hili lilikuwa tatizo dogo kwako, usijidanganye ndugu yangu, hii inaweza kuku-haunt maisha yako yote; so take it seriously nenda kamuone na umuombe msamaha.
 
Great thinker unawaza hayo!Hakuna uhusiano kati ya matukio hayo mawili!Ngeleja kafutwa kazi kwa kutowajibika,si kwa kumpiga huyo mlinzi!Tuache tabia ya kuhusisha matukio yanayofuatana kwamba la pili limetokana na kwanza!

Mkuu usituchekeshe! Kwani ujawahi kusikia laana - wewe unafikili laana lazima zitoke kwa wazazi, hata mtu mnyonge akifanyiwa dhuluma wakati anatimiza wajibu wake Mungu huwa anamsikiliza na kutoa fundisho.
 
Hiki kisa kinafanana sana kingine kiliwahi kutokea Moshi nadhani ilikuwa around 2009. Kuna Mayor wa Moshi alikuwa akiitwa Kaaya alimtandika makofi Security guard wa pale ofisini kwake,kisa yule askari alimkataza yule Mayor asipaki gali lake kwenye car park ya mayor ambayo ilikuwa wazi kwa wakati ule. Kumbe yule binti (Security guard) alikuwa mgeni pale hakuwaki kumfahamu yule Mayor. Lakini hata hivyo isingekuwa rahisi kumfahamu kwani yule Boss alikuja ofisini na gari yake binafsi ndipo aka park kwenye maegesho ya mayor so mlinzi hakuweza kumtambua. Akawa anakazana kumwambia atoe gari yake kwani pale ni kwa Mheshimiwa,not knowing she was talking to the man himself. Aliishia kuchezea kichapo kikali. Ila alienda kushtaki police sijuwi kesi iliishia vipi... Hao ndo viongozi wetu badala ya ku complement a good job unaishia kudhalilishwa eti kosa kutomjua Mayor!!! Mungu atusaidie tuweze kuitambua...
 
wapo wengi waliokuwa wakila kwa mgongo wake! Si wote waliao msibani wanamlilia marehemu! Kuna kila dalili ulikuwa ukinufaika na matunda ya nafasi yake........................ Utaisoma.

Huna ulijuwalo unabaki na dhanna tu, hakuna awezae kuishi kwa mgongo wa binaadam mwenzake yeyote. Rizki zetu anaetowa ni mmoja tu.
 

Similar Discussions

5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom