Baada ya kuondolewa Uwaziri, Ngeleja akamuombe Msamaha mlinzi wa benki aliye mfukuzisha kazi

Jamani kumbukeni hawa ni wezi na wameshajiwezesha vilivyo !labda lifuatie zoezi la kurudisha iliyo haki yetu!
 
Bw. Ngeleja akiwa waziri alitamani na aliamini kila mtu ni lazima amtambuwe kuwa yeye ndiye Waziri hata pale anapokiuka taratibu za kazi kwa tasisi zingine. Kumbukeni alivyosababisha kumfukuzisha kazi mlizi wa benki moja aliyemwambia hairuhusiwi kuongea na simu kwenye ATM.

duh hii nilikua sijawahi kuisikia... safi sana mungu hamtupi mja wake...
 
He kweli yeye ndiye aliyekuwa kwenye lile sakata!!! Nani kama Mungu wetu? Hakuna wa kumfananisha na anatoa adhabu hapahapa duniani. Watu wasijidanganye kuwa adhabu ni ahera. Mifano mingi tunaiona.
Mheshimiwa kumbuka ni wapi ulipoanguka ukatubu. Tatizo kubwa ni kiburi kumbuka ulipoyang'oa mabango ya kanisa kwa kiburi. Mheshimiwa wenye kiburi hushushwa na hupata aibu. Ndugu yangu YESU anakupenda.
 
watanzania kwa kupenda kuongelea watu na si kuongelea maendeleo, haki kabisa mna laana. Msijifanye nyinyi ni malaika msiokuwa na makosa au nyinyi ni miungu wa kutolea hukumu maandiko ya magazeti ya udaku?

wapo wengi waliokuwa wakila kwa mgongo wake! Si wote waliao msibani wanamlilia marehemu! Kuna kila dalili ulikuwa ukinufaika na matunda ya nafasi yake........................ Utaisoma.
 
As far aa I am concerned kilichomfikisha hapo Njeleja ni hilo sakata. Chozi la myonge bana ni sala yenye nguvu mno na Mwenyezi Mungu hawezi katu kuifumbia macho.

hakika uu ni ukweli mtupu mkuuu....jamaa alkuwa namajibu ya ovyo na kiburi kilichotukuka... as if he was alfa and omega...
 
Yan huyu baba cjui ataend kuficha wap uso wake mana hata watoto wa miaka 5 wanamjua kama mzee wa megawatt full giza ukiuliza majibu yote yanatolew na mzee wa megawatt et kuna mipango ya kujenga mitambo mipya ya kuzalisha umeme, mpaka anaondoka (7yrs) hakuna mpango hata mmoja umeshaanza
what a shamefully scandle!!!!!!!
 
Watanzania kwa kupenda kuongelea watu na si kuongelea maendeleo, haki kabisa mna laana. Msijifanye nyinyi ni malaika msiokuwa na makosa au nyinyi ni miungu wa kutolea hukumu maandiko ya magazeti ya udaku?

Hili suala sio kuongelea watu, bali ni kuongea ukweli ili liwe fundisho kwa watu wenye tabia kama hizo na wewe ukiwemo. Hivi sio kweli kwamba huyo Mhe. alitenda hilo jambo pale Habour View a.k.a J' Mall ? Kulikuwa na sababu gani kuongea na simu ndani ya chumba cha ATM halafu alipoambiwa kama anaongea na simu apishe wengine akauliza Mlinzi kama hamfahamu yeye ni nani !!!! Ina maana huyu Mhe. aliongea na simu na kuchelewesha wengine makusudi bila kujali kuwa labda kuna mtu anataka kuchukua pesa na kumwahisha mgonjwa hospitali !!! Je, ufisadi lazima uwe wa pesa tu ??? Hata kukiuka utaratibu nao ni ufisadi. Kiongozi yeyote akifika sehemu kama hiyo akasalimia watu, wakishamwona watamwabia atangule tu. Tatizo ni pale anapofika Big Headed moja kwa moja hadi Counter !!!! Nimeshahudia wawili, tena wote Wamama (mmoja Waziri na mwingine NW); mmoja (Waziri) aliiingia NMB Bank House akakuta watu kwenye foleni akawasalimia kwa kusema ....Jamani hamjambo ??? Watu wote walipogeuka na kumwona ni yeye kila mmoja alimwambia Mhe. tangulia na alipofika counter; Teller alimhudumiwa maana alishaona watu wakimruhusu kutangulia. Sasa siku nyingine nikapata bahati ya kumwona Big Headed (NW); asiye fahamu kuwa uongozi ni utumishi wa watu na sio lazima ukiwa Kiongozi kila mtanzania anakufahamu !!!! alipofika hata hakusalimia mtu, akanyoosha moja kwa moja counter akipita katikakti ya mistari, ule wa withraw na ule wa Deposit si mnafahamu mambo ya bank house siku nyingine kunakuwa na nyomi !!!! Basi Bi. Dada mmoja akamvuta NW ili asiende mbele, kama kawaida NW akamwuliza hujui kuwa mimi ni NW wa ..................Bi. dada kama kapinda vile kamwabia huko huko ofisini kwako na UNW wako. Hata hivyo, NW aliweza kupenya na kufika kwa Teller ambaye aligoma kutoa ndururu mpaka taratibu zilipofuatwa.
 
Watanzania kwa kupenda kuongelea watu na si kuongelea maendeleo, haki kabisa mna laana. Msijifanye nyinyi ni malaika msiokuwa na makosa au nyinyi ni miungu wa kutolea hukumu maandiko ya magazeti ya udaku?

Hivi wewe kwa nini unapenda tetea maovu ya wana ccm. Kazi huko ofisini zimeisha za kupanga kuibia wa TZ?
 
wapo wengi waliokuwa wakila kwa mgongo wake! Si wote waliao msibani wanamlilia marehemu! Kuna kila dalili ulikuwa ukinufaika na matunda ya nafasi yake........................ Utaisoma.

Hahahaha roho inamuuma haswa
 
Bw. Ngeleja akiwa waziri alitamani na aliamini kila mtu ni lazima amtambuwe kuwa yeye ndiye Waziri hata pale anapokiuka taratibu za kazi kwa tasisi zingine. Kumbukeni alivyosababisha kumfukuzisha kazi mlizi wa benki moja aliyemwambia hairuhusiwi kuongea na simu kwenye ATM.

Yule kamanda alikuwa anaitwa Mnali nadhani
 
Ngeleja anamatatizo na watu wengi maana hata kaka yake mkubwa aliemsomesha hawaelewani kwa sababu wanamuomba msaada
 
Bw. Ngeleja akiwa waziri alitamani na aliamini kila mtu ni lazima amtambuwe kuwa yeye ndiye Waziri hata pale anapokiuka taratibu za kazi kwa tasisi zingine. Kumbukeni alivyosababisha kumfukuzisha kazi mlizi wa benki moja aliyemwambia hairuhusiwi kuongea na simu kwenye ATM.

Ngeleja.jpg
WAZIRI wa Nishati na Madini, William Ngeleja(pichani), juzi alizua tafrani kwenye mashine ya kuchukulia fedha (ATM) ya benki ya Standard Chartered, jijini Dar es Salaam baada ya kutaka kumchapa makonde mlinzi wa mashine hiyo, Pascal Mnaku.

Habari zilizolifikia gazeti hili jana na kuthibitishwa na mlinzi huyo wa kampuni ya Ultimate Security, zimeeleza kuwa tukio hilo lilitokea juzi saa 3:00 asubuhi kwenye jengo la Habour View, maarufu kama JMall. Mnaku aliliambia gazeti hili kuwa alinusurika kupigwa na waziri huyo kijana aliyekuwa akizungumza na simu ndani ya kibanda hicho, baada ya kumtaka atoke kuwapisha wateja wengine kupata huduma hiyo. Mnaku alisema waziri huyo alikuwa anatumia muda mwingi kuzungumza na simu ndani ya mashine hiyo badala ya kuchukua fedha wakati msururu mrefu wa watu ukiwa unamsubiri atoke.

(Source:
http://www.bongocelebrity.com/2010/01/07/alichokifanya-waziri-william-ngeleja-ni-sahihi/#axzz1uBcdx5sr)

Bw. Ngeleja akiwa waziri alitamani na aliamini kila mtu ni lazima amtambuwe kuwa yeye ndiye Waziri hata pale anapokiuka taratibu za kazi kwa tasisi zingine. Kumbukeni alivyosababisha kumfukuzisha kazi mlizi wa benki moja aliyemwambia hairuhusiwi kuongea na simu kwenye ATM.

Great thinker unawaza hayo!Hakuna uhusiano kati ya matukio hayo mawili!Ngeleja kafutwa kazi kwa kutowajibika,si kwa kumpiga huyo mlinzi!Tuache tabia ya kuhusisha matukio yanayofuatana kwamba la pili limetokana na kwanza!
 
Hivi Bishop Kakobe nae bado hajatoa 'ushuhuda' juu ya hili?

Kakobe hana shughuli na mtu kama Ngeleja,ila naionavyo mimi Ngeleja ameuona mkono wa Mungu wa
Kakobe,maana toka alivyomdhihaki huyu Mungu Ngeleja hajapata amani zaidi ya kibano kila kukicha,
mpaka mwisho wa yote ni huu wa kutimuliwa uwaziri uliokuwa unampa kiburi cha uzima.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom