Baada ya kuokoka mama akiri kumloga mumewe

Baada ya kuokoka mama akiri kumloga mumewe

Mfamaji

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2007
Posts
6,629
Reaction score
1,951
Hii imetoka kwa jamaa ambaye aliachana na mkewe baada ya mke kuokoka na akitaka mume aache pombe na sigara aokoke. Mama huyu alirubuniwa na mama wa jirani na kumpeleka kanisani kwao ambako aliokoka. Baada ya muda mama akahamishia maskani kanisani toka asubuhi hadi jioni yuko kanisani kwao tu, huku akimlalmikia mumewe kuwa ana pepo la pombe na sigara. Mume akasomeshwa ulokole akagoma, na kilichofuata ni mke kufungasha virago na kuhamia sehemu nyingine huku akiacha nyumba tupu. Baada ya mwaka mmoja mama maisha yakamshinda , ndipo alipotuma walokole wenzake wakomwombee mshamaha kwa mumewe. Walokole wakafanya hivyo na hadi mchungaji wao akawa mstari wa mbele kumsihi jamaa akubali mshamaha huo. Mume akaomba mke aitwe na alipofika akaanza kuuliza maswali yakilenga maisha yao ya ndoa na tafrani zao za kila mara. Mume akamuuliza mke, Je unajua miezi kama 6 hivi kila nikijaribu kufanya mapenzi na wewe uume ulikuwa ukianguka ghafla hadi nikapa tatizo la msongo wa mawazo? Mama akajibu; "hiyo ni kweli mume wangu ila naomba mchungaji uniombee dhambi hii iniishe". Akauliza dhambi gani? Akajibu, nilijua baada ya rafiki yangu kunitonya kuwa mume wangu akiwa kwenye pombe zake anakuwa na mwanamke mwingine. Hivyo ili kumkomesha tabia hiyo nitafute dawa. Alinipeleka kwa mganga aliyefikia guest......... (jina kapuni) akanipa dawa baada ya kumpelekea leso iliyokuwa na shahawa zake. Ila toka wakati huo mambo yakaanza kuharibika. Nilipoona hali imekuwa mbaya nikamweleza rafiki yangu nae akanishauri tena kwamba kama hawezi kufanya mapenzi,ina maana kaongeza mwanamke mwingine. Ndipo aliponishauri tena kwamba , kama mganga kashindwa anipeleke kanisani kwao ambako kila ombi linasikizwa na matokeo yanaonekana mara moja. Ndipo jamaa akaja juu na kuwatimua wote. Jamaa akihadithia anasema ilibidi awe anajaribu kwa wadada wengine na mambo yanakuwa shwari, ila akienda kwa mke jogoo nakuwa kama kapigwa sindano ya ganzi. MY TAKE. Kuna uwezekano mkubwa kwamba matatizo ya nguvu za kiume kwa wababa wengi ni matokeo ya kibilogia lakini asilimia kubwa kwa bongo ni ushikirikina wa wake zao. Asilimia kubwa ya wanawake wa Kitanzania wanaamini nguvu za giza au miujiza hivyo kufanya mambo yenye athari kwao bila kujua. Wengi wanaenda kwenye makongamano ya kilokole na wakitoka huko wanaelekea kwa waganga. Wanaume kuweni makini, kama mambo yenyewe ni kama haya,hali ni mbaya . Nimeiweka kama hadithi kwa maneno yangu, lakini ni true story na ni refu , nimefupisha.
 
protection hapa ni kutokuoa tu kuzalisha must!!
 
Back
Top Bottom