Kamgomoli
JF-Expert Member
- May 3, 2018
- 1,865
- 3,810
Binafsi sikuwahi kuwaamini viongozi na wanasheria wa Yanga kwenye suala zima la mgogoro wa kimkataba na Feisal Salum kwa wasababu ya historia mbovu ya mikataba na wachezaji ambayo Yanga wamekuwa nayo.
Lakini baada ya kumsikiliza mama yake Feisal nimejiridhisha kuwa kuna watu kwa makusudi na mslahi yao binafsi walitumia mwanya wa uelewa mdogo wa mambo ya kisheria kuwaaminisha kuwa Feitoto anadhulumiwa na Yanga.
Ukimsikiliza mama anarudia rudia tu kusema eti mwanae(Feisal) kadhulumiwa sana na Yanga, sheria itende haki inakuaje mwanae alipwe milioni 4? Anasema Feitoto ana majukumu mengi ya kusomesha ndugu zake n.k. Najiuliza wakati Feisal anasaini mkataba mpya kutoka mil1.6 hadi 4.7 mama alikuwa wapi kumpambania mwanae ili asaini dili nono litakaloendana na thamani wanayodhani anastahili? Leo inakuaje aone hizo mil.4 ni ndogo na mwanae anadhulumiwa? Je kuna pesa yoyote ambayo Feitoto alistahili kulipwa na mwajiri wake na hakulipwa? Hata mimi ambae si mwanasheria sioni hoja yoyote ya msingi.
Ndio maana watu wengi wanaomtakia mema mchezaji wameshauri mara kadhaa familia na mchezaji mwenyewe warudi wakae mezani wazungumze na uongozi wa Yanga ili wayamalize kifamilia na kiundugu kuliko hiki kinachoendelea. Feitoto na Familia nzima wanapaswa kujua sheria haitambui huruma, ila huruma inaweza kupatikana kupitia vikao suruhishi endapo watakaa na kuzungumza km familia.
Narudia tena Familia imerubuniwa.