Baada ya kumsikiliza mama wa Feitoto, ni dhahiri Fei na familia nzima wamerubuniwa

Kamgomoli

JF-Expert Member
May 3, 2018
1,865
3,805
Binafsi sikuwahi kuwaamini viongozi na wanasheria wa Yanga kwenye suala zima la mgogoro wa kimkataba na Feisal Salum kwa wasababu ya historia mbovu ya mikataba na wachezaji ambayo Yanga wamekuwa nayo.

Lakini baada ya kumsikiliza mama yake Feisal nimejiridhisha kuwa kuna watu kwa makusudi na mslahi yao binafsi walitumia mwanya wa uelewa mdogo wa mambo ya kisheria kuwaaminisha kuwa Feitoto anadhulumiwa na Yanga.

Ukimsikiliza mama anarudia rudia tu kusema eti mwanae(Feisal) kadhulumiwa sana na Yanga, sheria itende haki inakuaje mwanae alipwe milioni 4? Anasema Feitoto ana majukumu mengi ya kusomesha ndugu zake n.k. Najiuliza wakati Feisal anasaini mkataba mpya kutoka mil1.6 hadi 4.7 mama alikuwa wapi kumpambania mwanae ili asaini dili nono litakaloendana na thamani wanayodhani anastahili? Leo inakuaje aone hizo mil.4 ni ndogo na mwanae anadhulumiwa? Je kuna pesa yoyote ambayo Feitoto alistahili kulipwa na mwajiri wake na hakulipwa? Hata mimi ambae si mwanasheria sioni hoja yoyote ya msingi.

Ndio maana watu wengi wanaomtakia mema mchezaji wameshauri mara kadhaa familia na mchezaji mwenyewe warudi wakae mezani wazungumze na uongozi wa Yanga ili wayamalize kifamilia na kiundugu kuliko hiki kinachoendelea. Feitoto na Familia nzima wanapaswa kujua sheria haitambui huruma, ila huruma inaweza kupatikana kupitia vikao suruhishi endapo watakaa na kuzungumza km familia.

Narudia tena Familia imerubuniwa.
 
Kuna watu hawapo serious! Yaani mshahara wa milioni 4 anaona ni mdogo! na wakati

Imagine timu nzima ya Majimani Fc ilikosa milioni 1 tu ya kuwawezesha kusafiri kutoka Dar, kwenda Songea!! Hadi wakapata msaada kutoka kwa Erasto Nyoni mwenye asili ya huko!!

Mama amekosa kabisa hekima kwa kushindwa kumshauri mtoto wake kuto kuchezea kazi inayomuweka mjini, kwa kurubuniwa na matapeli.
 
Katika watu wajinga Fei na wanaomzunguka ni wajinga.

Ukirudi nyuma fei alitaka kutoka kimaisha haraka na mpaka anaingia yanga amekubari yote ili kufanikiwa haraka.

Sasa wanamlaumu nani ?
Wametaka wenyewe kununua kiwanjwa mchana ufukwe wa bahari kabla usiku ujaingia maji kujaa.
 
Kuna watu hawapo serious! Yaani mshahara wa milioni anaona ni mdogo! na wakati

Imagine timu nzima ya Majimani Fc ilikosa milioni 1 tu ya kuwawezesha kusafiri kutoka Dar, kwenda Songea!! Hadi wakapata msaada kutoka kwa Erasto Nyoni mwenye asili ya huko!!

Mama amekosa kabisa hekima kwa kushindwa kumshauri mtoto wake kuto kuchezea kazi inayomuweka mjini, kwa kurubuniwa na matapeli.
Pengine kaona Kuna kwingine ambapo anaweza PATA zaidi ya hiyo
 
Poor reasoning

Mwambie Azizi Ki kuanzia leo awe ana chukua 4M kwasababu kuna timu ya majimaji ilikosa pesa ya nauli
 
Pengine kaona Kuna kwingine ambapo anaweza PATA zaidi ya hiyo
Lakini angetumia njia ya kiungwana. Na siyo ile aliyoitumia yeye. Maana ilijaa dhrarau, uhuni, na utoto mwingi.

Binafsi ningetamani kumuona dogo akicheza kwa miwango cha juu! Halafu angevumilia mpaka mwakani. Viongozi wangekaa naye mezani, ndiyo anvetikisa sasa kibiriti ili wapande dau, na kama invetokea wameshindwa; angeenda zake kwingine.

Sasa maamuzi aliyochukua, yamekuwa na madhara pande zote! Hakuna mnufaika katika huu mgogoro. Zaidi tu ya upande mmoja kushika kwenye mpini, na upande mwinvine kushika kwenye makali.
 
Lakini angetumia njia ya kiungwana. Na siyo ile aliyoitumia yeye. Maana ilijaa dhrarau, uhuni, na utoto mwingi.
Inawezekana ila usihitimishe, Fei hawezi kuongea against Yanga sababu bado ni mchezaji, si salama kwa carrier yake. Huenda alitumia hizo njia na ikashindikana, viongozi wa Yanga si malaika kuwa hapawezi tokea mnyonyaji au mdhulumu haki. Lolote linawezekana. Siku akizungumza ndo utaweza kuhitimisha.
 
Poor reasoning

Mwambie Azizi Ki awe ana chuka 4M kwasababu kuna timu ya majimaji ilikosa pesa ya nauli
Wajuaji kama nyinyi, huwa ninawapuuzia tu. Mchezaji amesaini mwenyewe mkataba, halafu mnaleta porojo za Aziz Kii.

Kwanza usikute hata mishahara ya wachezaji wa timu yako tu chini ya mwekezaji wenu janja janja, hata huijui! Ila ya wale wa Yanga, unaijua yote! Na hili ndilo tatizo lenu kubwa; kujitoa ufahamu.
 
Kuna watu hawapo serious! Yaani mshahara wa milioni anaona ni mdogo! na wakati

Imagine timu nzima ya Majimani Fc ilikosa milioni 1 tu ya kuwawezesha kusafiri kutoka Dar, kwenda Songea!! Hadi wakapata msaada kutoka kwa Erasto Nyoni mwenye asili ya huko!!

Mama amekosa kabisa hekima kwa kushindwa kumshauri mtoto wake kuto kuchezea kazi inayomuweka mjini, kwa kurubuniwa na matapeli.
Et milion 4 ndogo , huyu mama anachekesha aisee 😁 anyway wacha apambane apate hyo million 15 per month
 
Acheni maneno mengi..mlipeni vizuri kwishaa
Kwani Yanga wamemlipa kinyume na mkataba aliousaini mwenyewe ?

Je kama akilipwa vizuri kwa madai kiwango chake kinaruhusu je akishuka kiwango baada ya mkataba mpya kama ilivyokuwa kwa Nondo na baadhi hata ya wachezaji ulaya ,je klabu nayo ina haki ya kudai fedha na mchezaji kupunguziwa au Kukata mshahara kisa ameshuka kiwango ?
 
Ila jamani twende mbele na kurudi nyuma huo mshahara sio mdogo sema angeomba aongezewe tuu maslahi kwa taratibu nzuri..ila kuja public na kusema mshahara mdogo wkt kuna watu wanalipwa laki 5 na maisha yanaenda sidhani kama ni kitu sahihi..
Sema angeomba mkataba upitiwe aongezewe maslahi yake kulinga na kazi yake na umuhimu wake pia...
 
Watu gani? Hao wanao staafu wakiwa na miaka 60, mchezaji akifikisha miaka 30 tayari anaambiwa ni mzee, wakati kada nyingine ndio kwanza kijana anaanza kazi, lazima mchezaji alinge pesa ndefu maana thamani yake inapungua na umri
 
Haya hapo alipo analipwa au anapoteza muda? Mimi naonea huruma kipaji chake...any way kupanga ni kuchagua
 
Back
Top Bottom