Lizaboni
JF-Expert Member
- Feb 21, 2013
- 33,894
- 20,375
Wadau, amani iwe kwenu.
Kuna madai kwamba Rais John Pombe Magufuli ni rafiki wa karibu na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ambaye ameng'olewa kutokana na kosa la kuingia Bungeni akiwa amelewa, Charles Kitwanga. Tena baadhi ya wabunge wa Upinzani wakiongozwa na Godbless Lema walisikika wakisema kuwa Rais Magufuli hawezi kumchukulia hatua Waziri huyo kwa kitendo chake cha kufanya biashara na Wizara anayoiongoza, kwa vile tu ni "MSHKAJI" wake.
Kabla hata mate yao hayajakauka, Rais Magufuli kafanya maamuzi ya kumng'oa Waziri huyo tena kwa kashfa kubwa ya kuingia Bungeni akiwa amelewa. Rais Magufuli angeamua kumuondoa tu kwenye baraza la mawaziri Charles Kitwanga bila ya kutoa sababu ama angeweza kufanya mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri kwa kumuondoa Kitwanga na wengine ambao wameonekana wana Mapungufu kama Januari Makamba na Mwigulu Nchemba. Hata hivyo, Rais Magufuli hakutaka kuwa mnafiki. Akaamua kuchukua hatua kwa wakati.
Ninaamini kuwa hata wale wanaojiita watetezi wa haki za binadamu ambao wanapinga utumbuaji majipu hawatadiriki kupanua vinywa vyao kupinga uamuzi wa Rais. Ninaamini pia hata viongozi wa upinzani wakiongozwa na Freeman Mbowe na Tundu Lissu ambao siku zote wamekuwa wakidai kuwa Rais Magufuli hafuati katiba na Sheria wakati wa kutumbua Majipu kwa kutotoa nafasi kwa watumbuliwa kujieleza hawatadiriki kusema chochote.
Rais Magufuli yupo sahihi siku zote na kwa hili la Kitwanga hakika amedhihirisha kuwa Serikali yake haina mambo ya Kishkaji.