JembePoli
JF-Expert Member
- Jul 14, 2015
- 1,324
- 995
Habari wana bodi,
Ni miaka mingi imepita tukiwa kwenye mahusiano lakini tulikuja potezana 2012-2013.Jana nikiwa katika mihangaiko yangu ya kila siku(nimejiajili) alikuja Mteja oficen kwangu bahati nzuri nilimkumbuka ni bro (kipindi nasoma alikuwa akinisaidia) ndio maana nilikuwa namwita bro isitoshe alikuwa mbele yetu mwaka mmoja.
Katika stori mbili tatu akaniambia yeye ameajiriwa katika moja ya hii mifuko ya hifadhi za jamii na ameoa ila bado hawajabahatika kupata mtoto.Na kwa vile pale ni sehemu ya kazi akaniambia si vema kupiga stori ila jioni baada ya kazi niende sehemu fulani ili tupige stori za muda wote tuliopotezana.
Nilifika sehemu ya tukio saa 2:08 usiku nilimkuta mwenyeji wangu akiwa ameshafika na yupo na mwanamke mzuri/mrembo niligundua ni mkewe (eneo lilikuwa na Giza kiasi) sikuweza kumtambua vizuri, bia zikashuka tukapiga michemsho pale lakini nilikuja kugundua mke hakuwa na furaha, pale mara kwa mara mmewe alipokuwa anamsii kama "vipi uko sawa? Mbona kama umepoa ghafla? Unaumwa? Mkewe mara zote alikuwa akimjibu anatusikiliza/napenda stori zenu.
Baadae jamaa alienda Toilet na ndio yule mwanamke/mkewe jamaa aliponiuliza unanikumbuka? Nikajibu hapana akanitajia jina kidogo nizimie ndio mpenzi wangu niliepotezana na hakutaka kusikia malalamiko yoyote alichonambia yeye sasa ni mke wa mtu na hayo ndio maamuzi yake (kumbuka hatukuwahi kugombana) ila aliniambia mdogo wake ananipenda sana amekuwa akiniulizia na kama nitahitaji msaada yupo tayari kunisaidia (sio mbaya nimekuwa nikiona picha zake Insta)
Japo mara nyingi nimekuwa nikituma DM kuuliza kuhusu dada yake lakini hazikuwa na majibu.Sina namna tena kwani hata sikukaa sana niliaga na kuondoka ila sikuonyesha utofauti kwa bro (unaempenda kamwe huwezi kumualibia)
Leo nimeamua nianze kumpa somo mdogo wake ili niamishie majeshi huko kwani hata post zake za instagram nyingi zinamuonyesha akiwa anatoka church/ama post za nukuu za bible.Sidhani kama atakuwa na tabia mbaya.
Naombeni mnishauri, wazo langu niko sawa au nipotezee.