Baada ya kumfunga Lissu, unamshauri nini Samia?

Father of All

JF-Expert Member
Joined
May 30, 2026
Posts
475
Reaction score
863

Rasmi, Tundu Lissu ni mfungwa. Je, hii imelenga kumzuia kugombea tena urais? Hivi, Samia anafaidikaje na ukatili na uvunjaji sheria huu ulioandamana na ukiukwaji wa sheria na haki za binadamu.

Kwa wale wenye mawazo kama yangu kuwa haki haikutendeka, mnaweza au mnataka kumshauri nini rais Samia? Nini afanye kuondoa huu upuuzi na uvunjaji wa haki za binadamu na upindishaji sheria kwa kutumia kwa upendeleo wa kisiasa?

Kwa namna Samia alivyojionyesha na kujifanya kumjali mbali na kumhaidi Lissu wangeyamaliza, amejionesha kuwa ni kigeugeu asiyepaswa kuaminika? Je, Lissu amefungwa kwa ajili ya Samia kutaka mwaka 2030 kutuletea kibaraka chawa wake? Je, nini kifanyike kuzuia hii hujuma dhidi ya taifa? Maswali ni mengi kuliko majibu ila Watanzania, naamini, mna majibu yake sahihi.
 
Afùatiè Kihongosi na Kaŵida
 
Amtoe kwa msamaha wa wafungwa kwenye sherehe za miaka 65 ya Uhuru.

Kwasababu hata kama Tundu Lisu akata rufaa sasa hivi, upo uwezekano wa kupiga tarehe za kutosha ili kupoteza muda.

Hivyo njia pekee iliyopo mbele yake ni kumwachia kupitia msamaha wa raisi, ili kila upande utulie na Lisu aachwe aendelee na shughuli za kisiasa.
 
Rais hahusiki na kifungo cha Lissu. Labda ungesema tuishauri mahakama imwongezee miaka ya kutosha kwenye hiyo rufaa kwa sababu ndo hitaji kubwa la wazalendo wengi kwa sasa.
 
Rais hahusiki na kifungo cha Lissu. Labda ungesema tuishauri mahakama imwongezee miaka ya kutosha kwenye hiyo rufaa kwa sababu ndo hitaji kubwa la wazalendo wengi kwa sasa.
Si kwamba ahusika ila atapopelekewa majina ya kuyafikiria huo ndo utakuwa mwanya wa kumwachia Tundu Lissu.

Tambua kuwa hadi mida hii weye waona sawa lakini kwenye macho ya Dunia Tanzania yaonekana ni kituko kwa kilotokea.
 
Rais hahusiki na kifungo cha Lissu. Labda ungesema tuishauri mahakama imwongezee miaka ya kutosha kwenye hiyo rufaa kwa sababu ndo hitaji kubwa la wazalendo wengi kwa sasa.
Wewe mwanamke ni katili na maamuma wa kiwango cha juu kabisa. Halafu uache mara moja tabia yako ya kujifanya ni dume humu jukwaani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…