Mgambilwa ni mntu
JF-Expert Member
- May 30, 2017
- 2,869
- 3,188
Muonekano wa Gati mpya Na. 1
Baada ya kukamilika kwa Gati Na. 1 kati ya 7 yanayojengwa katika Bandari ya Dar es Salaam kwa gharama ya bilioni 33.7; ufunguzi unatarajiwa kufanyika wiki ijayo ha kuhudhuriwa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe.
Kulingana na Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Deusdedith Kakoko, upanuzi huo wa gati lenye urefu wa mita 192 umeiongezea uwezo wa kubeba meli mbili kubwa za tani 45,000 - 60,000 kwa wakati mmoja, kutokana na kuongezwa kitako cha upana wa mita 11.5 kinachobebwa na nguzo imara za zege zilizochimbiwa mita 70 chini ya bahari.
Kukamilika kwa gati hilo kutaiwezesha Bandari kupokea magari 10,000 kwa siku, kiwango ambacho ni mara nne ya kiwango cha sasa cha magari 2,500 kwa siku na kwamba kwa mwaka kitakua cha magari 200,000 kutoka magari 90,000.
Kakoko alieleza kuwa: "Kukamilika kwa gati hili kutaleta mapinduzi makubwa kwani tunaweza kupokea meli ya magari 3,000 hadi 5,000 na ikapakuliwa kwa siku moja pekee."
Mkurugenzi huyo alieleza kuwa, upanuzi wa gati utakwenda sambamba na upanuzi wa lango la Bandari kwa kuongeza kina kutoka mita 10 hadi mita 16. "Nia yetu ni hadi kufikia Disemba mwakani tuwe na gati kuanzia sifuri hadi namba tatu na upanuzi wa lango uwe umekamilika ili tuweze kupokea meli za kimataifa zenye kina cha mita 15 na uwezo wa kubeba hadi makasha 6,000 kutoka meli za sasa zinazoweza kubeba makasha 2,500 tu."