Baada ya kujenga, kijiji kizima sasa kinafikia kwangu

jean phillipe beyun

Senior Member
May 18, 2015
142
167
Wadau nawasalimu,

Wakati nikiwa kwenye nyumba ya kupanga chumba na sebule sikua nikipata wageni kabisa, ilipita miezi kabla ya kupata mgeni, wageni ninaowazungumzia ni wa kutoka kijijini kwetu na mikoani

Mwaka jana nilihamia kwenye nyumba yangu baada ya ujenzi wa muda mrefu, sasa nimeshangazwa sana na trend ya wageni kutoka mkoani wanaokuja kwangu, january pekee walipishana ndugu waliokua wakileta watoto wao boarding wakati shule zinafunguliwa hadi nilichanganyikiwa, haikushia hapo hali imeendelea hivyo hadi sasa, wapo wanaokuja kwenye biashara hawataki kulala gesti, na kadhalika

Yote tisa, kumi, yupo mmoja mjomba wangu, yy tangu january yupo hapa, watu wanakuja na kuondoka yy yupo, kilichomleta dar hakieleweki, anashinda hapo anapika asubuhi hadi jioni pamoja na utu uzima alionao, maana sijaoa na maid sina, anadai kaja kutafuta sarafu za wajeremani hadi azipate ndipo arudi

Sasa wadau nifanyeje hawa wageni wasije kwangu? Nataka warudi huko walikokua wanafikia zamani, au nirudi kupanga chumba na sebule, then nyumba niipangishe?

Na huyu mjomba nimtoeje hapa kwangu, maana gharama zimekua kubwa, kila mara anaomba nauli kwenda na wenzie kutafuta sarafu za wajeremani mapangoni kisarawe, na juzi nimemsikia kwenye simu akiita mkewe nae aje dar kuwa yy atachelewa kurudi kijini

Any ideas?
 
Wacha kuwa na roho ya ubinafsi hizo ndiyo baraka zenyewe watu wanatafuta wewe unazikimbia....Kama wagEni wanakuja na unaweza kuwa-afford kuna shida gani maana hujasema unashindwa kwa ajili ya budget ya chakula ila unalalamika tu hataki watu kwako...Na amini hao ndugu zako wanakuwa proud sana na wewe kuweza kuwahifadhi kumbe wewe roho inakuuma...
 
Gharama ya maisha dar ipo juu, ukiendekeza watu hufiki kokote
 
Wadau nawasalimu,

Wakati nikiwa kwenye nyumba ya kupanga chumba na sebule sikua nikipata wageni kabisa, ilipita miezi kabla ya kupata mgeni, wageni ninaowazungumzia ni wa kutoka kijijini kwetu na mikoani

Mwaka jana nilihamia kwenye nyumba yangu baada ya ujenzi wa muda mrefu, sasa nimeshangazwa sana na trend ya wageni kutoka mkoani wanaokuja kwangu, january pekee walipishana ndugu waliokua wakileta watoto wao boarding wakati shule zinafunguliwa hadi nilichanganyikiwa, haikushia hapo hali imeendelea hivyo hadi sasa, wapo wanaokuja kwenye biashara hawataki kulala gesti, na kadhalika

Yote tisa, kumi, yupo mmoja mjomba wangu, yy tangu january yupo hapa, watu wanakuja na kuondoka yy yupo, kilichomleta dar hakieleweki, anashinda hapo anapika asubuhi hadi jioni pamoja na utu uzima alionao, maana sijaoa na maid sina, anadai kaja kutafuta sarafu za wajeremani hadi azipate ndipo arudi

Sasa wadau nifanyeje hawa wageni wasije kwangu? Nataka warudi huko walikokua wanafikia zamani, au nirudi kupanga chumba na sebule, then nyumba niipangishe?

Na huyu mjomba nimtoeje hapa kwangu, maana gharama zimekua kubwa, kila mara anaomba nauli kwenda na wenzie kutafuta sarafu za wajeremani mapangoni kisarawe, na juzi nimemsikia kwenye simu akiita mkewe nae aje dar kuwa yy atachelewa kurudi kijini

Any ideas?
sio bure uliwaendekeza tangu mwanzo
 
Back
Top Bottom