Baada ya kuhudumia mtoto nimegundua sio damu yangu. Nimuoe huyu mwanamke nilee mtoto asiye wangu au nimuache?

Huyo mtoto ni wako na kwa kuwa ana jina la mama yako basi teyari ni wako
Marekani ukikubali kutengeneza tu birth certificate na ukasaini basi mtoto ni wako
Ila mie natambua sio lazima kuchangamana damu kuwa familia
Mtunze sana huyo mtoto atakuja kuwa msaada mkubwa sana kwako
Hata akikua usije mlea kama mtoto wa nje, atakuletea baraka nyingi sana kwenye maisha yako. .

Anaweza kuja kuwa mtoto wa pekee kwako, unaweza ukatembea tu gari ikakanyaga jiwe na tairi na jiwe likarushwa likagonga pumbu; ndo basi tena hapo. Usimwache mtoto laana zipo na mwisho wa ubaya aibu. .
 
"Nina miaka 25 nipo Kigoma. Nilikuwa na mahusiano na mdada mmoja hivi, tangu mwezi wa tisa mwaka 2016 kipindi hicho yeye alikua mwanafunzi so sikutaka kuharibu malengo yake sikuwahi kumuuliza wala kumtaka kimwili mpaka akamaliza shule ndio tukakutana 2017.

Kuanzia hapo tulipendana sana mpaka tukatambulishana home yaani mahusiano yetu mpaka wazazi walikua wanafahamu. Ilikuwa furaha kwakweli.

Matokeo ya kidato cha nne yalipotoka akaenda chuo Tabora na mimi nikabaki Kigoma nikiendelea na mishe mishe za utafutaji huku tukiwasiliana kwenye simu kila siku.

Kiukweli nilimjali sana, nilimtumia hela ya matumizi kila mwezi, kila kiti kilichokuwa ndani ya uwezo wangu, nilimpa.

Sikutaka akose chochote, hata wazazi wake walipopungukiwa kwenye ada, mimi niliongezea pale wazee walipopungukiwa.

Hiyo ikafanya kwao wanipende mno. Nilitoa msaada kwao na mtoto pia.

Shida ilikuja 2020, alipata ujauzito. Kiukweli hakutaka kwao wafahamu. Tuliweka siri mpaka akajifungua ndio tukafikisha taarifa nyumbani.

Kwa bahati nzuri alijifungua mwezi wa kwanza baada ya kuhitimu chuo. Kwao walikua wakali ila badae walielewa wakatulia.

Nikampa mtoto jina la mama yangu. Maisha yakaendelea na kwao waliamini nitamuoa.

Kwa bahati mbaya miezi miwili badae Mama yangu alifaliki so mambo yakazidi kuwa magumu kwangu. Nikajikuta naahilisha suala la ndoa na yule binti ili nikae sawa. Tukakubaliana tusogoze mbele suala la ndoa Ili tujipange vizuri.

Badae wakati mimi ndio nakamilisha mambo yangu taratibu akaanza kubadilika akawa ananifanyia visa ilimradi tuachene tu. Suala la ndoa akawa halitaki tena.

Kiukweli mara kadhaa niliwahusisha ndugu zake ila wakawa wananipa tu moyo wakasema mimi ndio mkwe wao hakuna mwingine. Mtoto akatimiza mwaka. Yule mwanamke akiwa bado hataki kufunga ndoa na mimi.

Mwanaume niliendelea kumhudumia mtoto, nilimpenda sana mwanangu. Atake nini nisimpe? jina lake lilinikumbusha marehemu mama yangu.

Sasa ikawa tunasumbua sana kwenye masuala ya hela, yaani kila mwezi nilikuwa natuma pesa ya matumizi na siku za sikukuu mwanangu hakosi nguo mpya.

Ilikua natuma pesa mpaka muda mwingine nilihisi ananikomoa. Ila sikutaka kujali sana maana nilijua natuma kwa ajili ya mtoto wangu.

Sasa kimbembe kimekuja hivi majuzi, kuna jamaa nilikuta amepost picha za mwanangu huku akijisifu amekuza. Nilishangaa, kiukweli nilihisi kama naota.

Ikabidi nimfuatilie jamaa mpaka nikapata namba yake, nikampigia akaniambia ukweli kwamba yeye yupo Tabora na alikutana na huyu mdada huko chuo na kumbe walikua wana mahusiano tangu 2020 na ndio alimpa mimba.

Ilinibidi nimuulize mhusika mwenyewe (mama wa mtoto) akakiri ni kweli akaniambia na mtoto sio wangu ni wa huyu jamaa wa Tabora yaani hapo nilitamani hata kufa kwani nilipoteza muda na gharama nyingi kwa ajili ya mtoto.

Niliwaambia wazazi wake, kumbe mama yake alikuwa anajua ila aliogopa kuniambia. Baba yake tu ndo alifichwa.

Sasa baba yake yeye hataki mwanamke aolewe kwingine anataka mimi ndio nimuoe. Hata mahali hataki, yaani ameniambia nikachukue mke bureee.

Sasa mimi nachoomba unifikishie kwa wadau wanipe ushauri , nikaoe huyu mwanamke nilee mtoto asie wangu au niachane nae niendelee na maisha yangu?

Please usiache kufikisha ujumbe huu". Anonymous, Kigoma.
#C&P From WatuNiStory
Kumbe ni copy and paste story?
 
Nadhani hakuna haja ya kuendekea na huyo mwanamke hapo ulikuwa hupendwi ila umepotezewa muda wako bure, huyo sio mwanamke wa kulazimisha kuwa nae kama imetokea hivyo achana nae angalia mbele zaidi japo inauma lkn hauna jinsi hawa viumbe ni hatari sana aisee huwa sio wa kweli.
 
Mkuu pole sana kwa magumu unayopitia ila jipe moyo na uamini kwamba yote Ni mapito tu ipo siku kila kitu kitakuwa shwari.

Huyu dada akae akijua KARMA inamsubiri mbeleni.
 
Nikitoaga mtoto bichwa kama langu, yani hata ukipanga kumpa mtu mwingine dogo haendi!
 
Siwez kukushaur mengi
ila nakuomba ujue uyo mwanamke hakufai kwa ndoa, vinginevyo wanawake wameisha.

1. Kafanya kosa la kwanza la kukucheat na kulalwa na Mwanaume wa nje.
NB: Mwanamke anacheat kwa hisia, kamwe hawezi kulalwa na asiyempenda.
Maana ake we we hupendwi.

2. Kafanya kosa la pili la kubeba mimba kabisa uko kwenye uzinzi wake.
NB: angekua anakupenda, Iyo mimba angeitoa kuepusha tafrani.

3. Kafanya kosa la tatu la kukuomba matumizi ya kulea mimba, Na anajua kusudi iyo mimba siyo yako.
Huu Ni unafiki wa Hali ya juu Sana.

4. Kafanya kosa la 4 la kukuomba matunzo ya kulea mtoto, anaejua kabisa sio wako. Wkt anajua kabisa baba yake yupo.
Huu Ni unafiki, uchonganish na roho mbaya.

5. Kafanya kosa la 5 la kuitunza Siri miaka yote, uku akijua anakula Mara mbili, kwa wanaume wawili tofauti.
Maana ake alijiamini kwa alichokifanya.

Kwa kifupi,
Mwanamke wako ana roho ngumu Sana,
Ana roho ya kikatili sana kuweza kufanya yote hayo. Hafai kua mkeo.
 
"Nina miaka 25 nipo Kigoma. Nilikuwa na mahusiano na mdada mmoja hivi, tangu mwezi wa tisa mwaka 2016 kipindi hicho yeye alikua mwanafunzi so sikutaka kuharibu malengo yake sikuwahi kumuuliza wala kumtaka kimwili mpaka akamaliza shule ndio tukakutana 2017.

Kuanzia hapo tulipendana sana mpaka tukatambulishana home yaani mahusiano yetu mpaka wazazi walikua wanafahamu. Ilikuwa furaha kwakweli.

Matokeo ya kidato cha nne yalipotoka akaenda chuo Tabora na mimi nikabaki Kigoma nikiendelea na mishe mishe za utafutaji huku tukiwasiliana kwenye simu kila siku.

Kiukweli nilimjali sana, nilimtumia hela ya matumizi kila mwezi, kila kiti kilichokuwa ndani ya uwezo wangu, nilimpa.

Sikutaka akose chochote, hata wazazi wake walipopungukiwa kwenye ada, mimi niliongezea pale wazee walipopungukiwa.

Hiyo ikafanya kwao wanipende mno. Nilitoa msaada kwao na mtoto pia.

Shida ilikuja 2020, alipata ujauzito. Kiukweli hakutaka kwao wafahamu. Tuliweka siri mpaka akajifungua ndio tukafikisha taarifa nyumbani.

Kwa bahati nzuri alijifungua mwezi wa kwanza baada ya kuhitimu chuo. Kwao walikua wakali ila badae walielewa wakatulia.

Nikampa mtoto jina la mama yangu. Maisha yakaendelea na kwao waliamini nitamuoa.

Kwa bahati mbaya miezi miwili badae Mama yangu alifaliki so mambo yakazidi kuwa magumu kwangu. Nikajikuta naahilisha suala la ndoa na yule binti ili nikae sawa. Tukakubaliana tusogoze mbele suala la ndoa Ili tujipange vizuri.

Badae wakati mimi ndio nakamilisha mambo yangu taratibu akaanza kubadilika akawa ananifanyia visa ilimradi tuachene tu. Suala la ndoa akawa halitaki tena.

Kiukweli mara kadhaa niliwahusisha ndugu zake ila wakawa wananipa tu moyo wakasema mimi ndio mkwe wao hakuna mwingine. Mtoto akatimiza mwaka. Yule mwanamke akiwa bado hataki kufunga ndoa na mimi.

Mwanaume niliendelea kumhudumia mtoto, nilimpenda sana mwanangu. Atake nini nisimpe? jina lake lilinikumbusha marehemu mama yangu.

Sasa ikawa tunasumbua sana kwenye masuala ya hela, yaani kila mwezi nilikuwa natuma pesa ya matumizi na siku za sikukuu mwanangu hakosi nguo mpya.

Ilikua natuma pesa mpaka muda mwingine nilihisi ananikomoa. Ila sikutaka kujali sana maana nilijua natuma kwa ajili ya mtoto wangu.

Sasa kimbembe kimekuja hivi majuzi, kuna jamaa nilikuta amepost picha za mwanangu huku akijisifu amekuza. Nilishangaa, kiukweli nilihisi kama naota.

Ikabidi nimfuatilie jamaa mpaka nikapata namba yake, nikampigia akaniambia ukweli kwamba yeye yupo Tabora na alikutana na huyu mdada huko chuo na kumbe walikua wana mahusiano tangu 2020 na ndio alimpa mimba.

Ilinibidi nimuulize mhusika mwenyewe (mama wa mtoto) akakiri ni kweli akaniambia na mtoto sio wangu ni wa huyu jamaa wa Tabora yaani hapo nilitamani hata kufa kwani nilipoteza muda na gharama nyingi kwa ajili ya mtoto.

Niliwaambia wazazi wake, kumbe mama yake alikuwa anajua ila aliogopa kuniambia. Baba yake tu ndo alifichwa.

Sasa baba yake yeye hataki mwanamke aolewe kwingine anataka mimi ndio nimuoe. Hata mahali hataki, yaani ameniambia nikachukue mke bureee.

Sasa mimi nachoomba unifikishie kwa wadau wanipe ushauri , nikaoe huyu mwanamke nilee mtoto asie wangu au niachane nae niendelee na maisha yangu?

Please usiache kufikisha ujumbe huu". Anonymous, Kigoma.
#C&P From WatuNiStory
Tafuta msichana mwingine oa achana na hizo mambo bwana mdogo.

Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
 
Pole sanaa usimuoe we kula mbususu pia mjali tu mtoto kwa hali ya kibinadamu ,ukishapata wako sasa utahamishia majukumu uko, uo mwanamke ni shritwani ukioa utakufa muda sio wako 35 utotoboa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom