Baada Ya Kikwete Kutoka Ikulu Juzi, Leo Mkapa Naye Ndani

Kibo10

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
11,277
8,850
Ule mwendelezo wa marais wastaafu Mkapa na Kikwete kwenda kwenda Ikulu leo umeendelea tena. Baada ya Kikwete kutoka Magogoni juzi leo Mkapa kamtembelea Rais Magufuli Ikulu tena.

Najiuliza hivi, Ni la Zanzibar linawapeleka? Mbona Rais Alishaliwekea msimamo wake juu ya Zanzibar?

Wakati wa Mkapa na Kikwete mbona watangulizi wao hawakwenda mara kwa mara?
1.jpg

2.jpg
 
Zanzibar si alisema Twende mahakamani.... sijui kwa kutumia sheria ipi?
 
Nikiunganisha Yale maneno ya Mwenyekiti wa CCM " sio Mimi niliesababisha kufutwa uchaguzi " na hivi vikumbo vya ikulu hapa kuna jambo limeibuka. Ni zito zaidi ya uwezo wa Magu.
 
Hahahaahahaha....Mhe Mkapa anatembea na Mzee wa Msoga Jino kwa Jino hili kumnusuru Magufuri Majipu kufundishwa dili za 10%
 
Wanaenda kuwaombea vibarua vijana wao, wanahaha kuhakikisha watu wa jk na mkapa wnakuwepo kwenye safu za ukuu wa wilaya na mkoa Kuna vijana wengi bado wanalilia nafasi zao na wanapitia migongo ya hao wapambe wanaoenda ikulu
 
Mkapa anaenda kumwambia Dr Magufuli asimsikilize kikwete na aachane na mambo ambayo kikwete ameenda kumwambua maana atachemka.

Ule mwendelezo wa marais wastaafu Mkapa na Kikwete kwenda kwenda Ikulu leo umeendelea tena. Baada ya Kikwete kutoka Magogoni juzi leo Mkapa kamtembelea Rais Magufuli Ikulu tena.

Najiuliza hivi, Ni la Zanzibar linawapeleka? Mbona Rais Alishaliwekea msimamo wake juu ya Zanzibar?

Wakati wa Mkapa na Kikwete mbona watangulizi wao hawakwenda mara kwa mara?
 
..isije ikawa kazi imemshinda Raisi Magufuli kila kitu inabidi apewe majibu na miongozo na hao waliomtangulia.

..mbona Dr.Bilali na Dr.Shein hawaendi ofisini kwa mama Samia Suluhu?

..mbona Mizengo Pinda haendi ofisini kwa Kassim Majaliwa.

..mbona mawaziri wa awamu ya nne hawaendi maofisini kwa mawaziri tulio nao sasa?

The Boss, Nyani Ngabu
 
Huuu Utawala wa Tano ni Mchanganyiko wa Serikali 3
Yaani Serikali ya JK, Mkapa na JPM.
Kila mmoja anataka lake lifanyike....
Mimi ndio nimekuweka hapo fanya hivi
Mimi ndio nilikupa uwaziri mara ya Kwanza fanya hivi..
 
Back
Top Bottom