Baada ya Gawio la Bilioni 3 toka TTCL, nimejifunza mambo kadhaa kutoka kwa Rais Magufuli

Jeff Kabwinde

Member
May 29, 2019
11
22
Na Jeff Kabwinde,

Awali ya yote nitoe pongezi za dhati kwa viongozi walioapishwa leo, hakika wanastahili, hivyo wakamuwakilishe vyema Mhe. Rais Magufuli kwenye utendaji wao.

Kimsingi Tanzania chini ya Rais Magufuli ni Tanzania yenye matumaini chanya kwa wananchi wake kama ilivyokuwa ikisubiriwa na watanzania wengi kwa muda mrefu.

Na hii imejidhihirisha katika hotuba yake ya leo wakati akiwaapisha viongozi wapya wa Serikali walioteuliwa ili kuongeza nguvu na hali katika utendaji wa serikali ya awamu ya tano.

Baada ya gawio la Bilioni 3 kutoka Bharti Airtel International wakiunga mkono juhudi za Mhe. Rais Magufuli, hakika imejidhihirisha wazi kuwa yeye ni mzalendo wa kweli wa nchi hii, na tukichunguza kwenye historia barani Afrika ni mzalendo wa pili akitoka Gaddafi kwa kuwa na mapenzi ya dhati kwa wananchi wake. Mwenyezi Mungu atupe uhai ili tupate kunufaika zaidi uko tuendapo.
Kwa mwendo huu tukimaliza Kuweka sawa miundombinu huenda uko pembeni ataweza kugawa kwa vijana pesa kwaajili ya posa hasa kwa mabarakala waliofikia umri wa kuoa.

Mhe. Rais ameweza kupigania nchi yetu na kuhakikisha kwenye mikataba ya kibiashara hasa ya kimataifa nchi yetu inanufaika kwa kiasi kikubwa, ndio maana kwa kupitia tume huru aliyoiunda iliweza kufanya ushawishi (lobbying) kwa kampuni ya Bharti Airtel International na kupata umiliki wa hisa zisizopungua 49 ambapo ni faida kubwa kwa nchi yetu kiuchumi.

Mzalendo Magufuli ni mkombozi kwa Taifa letu na anawazia yaliyomema siku hadi siku ndio maana hutafuta viongozi wachapakazi na waadilifu kila kukicha, wenye misimamo chanya na wanaojua kusimamia misimamo yao kwa faida ya Taifa letu.
Viongozi makini na wazalendo walioteuliwa na Rais Magufuli wameweza kusababisha kufutwa kwa Bilioni 459.13 ambazo tulipaswa kulipa sisi kama Taifa. Hakika hakuna kama Rais Magufuli.

Rais Magufuli sio mchoyo kwa wawekezaji hivyo huwahakikishia mazingira rafiki kwa kila atakayevutiwa kuwekeza nchini kwetu. Sambamba na ilo kwa kila atakayewekeza nchini kwetu atapata fursa ya masoko kutoka nchi wanachama wa umoja wetu wa Afrika ya Mashariki vilevile ataweza kuuza bidhaa kwa nchi wanachama wa jumuiya ya SADC vya masharti nafuu. Kwa kudhihirisha hilo Rais Magufuli ameweza kusimamia uundwaji wa Bodi ya menejimenti ya Airtel ambayo itasimamia kampuni hiyo vilevile itasimamia makubaliano yote yaliyoingiwa kati ya serikali na mwekezaji huyo. Sambamba na ilo itatoa wasaa na kuwa kivutio kwa wawekezaji wengine kutoka India waweze kuja kuwekeza nchini kwetu hasa kwenye zao la Korosho.

Mh. Rais ameonyesha wazi nia yake ya kutaka kuboresha maisha ya watu wa hali ya chini pale alipochukua uamuzi wa kulitoa gawio la Bharti Airtel ambalo kwa mahesabu makini na ya haraka hizo pesa zinaweza kujenga vituo bora vya afya zaidi 150 ambavyo kwa kiasi kikubwa vitaokoa maisha ya watoto, wakina mama na wazee waliopo mijini na vijijini.
Ila pia hakuishia hapo ameweza kutoa pesa kwa ajili ya Ujenzi wa hospitali ya Uhuru iliyopo Dodoma. Kitu ambacho ni kigumu kwa viongozi na marais wasio na uzalendo kukifanya.

Mh.Rais kwa upendo wake mkubwa na maono ya mbali anaendelea kuongeza Imani yake kwa Vijana wazalendo wa kitanzania wenye mitizamo chanya kwa Taifa na wenye kujitoa kupigania nchi yao kwa faida ya Taifa kwa ujumla. Hivyo vijana msibaki kutumika na mabeberu kulalamika, kupinga, kukejeli na kudhihaki mazuri yanayofanywa na serikali ya awamu ya tano bali mjitahidi kutumia akili na ujuzi wenu kujenga Tanzania iliyo bora zaidi chini ya Rais wetu mpenda JPM

Hakika watanzania tumekua tukichezewa kwa muda mrefu ila chini ya Serikali ya Rais Magufuli imekuwa tofauti kwani amekua mzalendo wa kuhamasisha ulipaji wa kodi unaongezeka na kupelekea ongezeko la ukusanyaji wa mapato ya ndani ili kuwezesha utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kimaendeleo.

Shime watanzania wote huu ni muda wa kuungana kwa pamoja kuiombea nchi yetu na Rais wetu JPM ili safari hii tuliyoianza yenye kuleta tija na Maendeleo tuweze kuifanikisha kwa kiasi kikubwa zaidi.
Vilevile sisi kama wazawa yatupasa kuendelea kumpa Ushirikiano wa kutosha Mh Rais Magufuli na serikali yake kwa kujitahidi kulinda amani tuliyonayo, kufanya kazi kwa bidii na kudumisha uzalendo ili kuendeleza ukuaji wa uchumi nchini kwetu.

Bharti Airtel International wanaunga mkono Juhudi za Rais Magufuli, wewe ni nani upinge?.
Screenshot_20190611-032632.jpeg
 
Bharti Airtel International wanaunga mkono Juhudi za Rais Magufuli, wewe ni nani upinge?.View attachment 1124197
watu kama nyinyi ndio mnamfanya Magufuli avulunde kila kitu. kwani badala ya kumwambia ukweli mnaishia kusifia kila kitu. mnashindwa kutambuwa kuwa raisi sio mungu bali ni mtu wa kawaida sana kama mimi na wewe ili afanikiwe anahitaji watu wa kumushauri kiutaalama kitaluma zaidi nasio watu wa kumwimbia pambio kama hii.
 
Unajua taasisi ya rais sasa watalaamu hao kwako hawatoshi ? Labda sijakuelewa nini shida yako
 
June 11, 2019

Dar-es-Salaam, Tanzania

Bharti Airtel will pay Tanzania to Settle ownership row

The company will pay to the government 1 billion shillings every month for sixty months starting April 2019, Chairman Sunil Mittal said at a briefing in Tanzania's commercial hub, Dar es Salaam

Bloomberg | Dar es Salaam

Bharti Airtel will pay the Tanzanian government 60 billion shillings ($26.2 million) over a period of five years to settle an ownership dispute.

The company will pay to the government 1 billion shillings every month for sixty months starting April 2019, Chairman Sunil Mittal said at a briefing in Tanzania’s commercial hub, Dar es Salaam.
The company will also pay the government a special divided at end of this year, Mittal said without mentioning the amount.

Mittal said that three of the seven members of the company’s board, will be Tanzanian.

Airtel will also give the East African country $1 million to support development projects, President John Magufuli’s communications director, Gerson Msigwa, said earlier Monday in an emailed statement.

The payments are part of a January deal in which Bharti agreed to reduce its stake in Airtel Tanzania to
51 per cent from 60 per cent, boosting the state’s Airtel Tanzania ownership of the company to 49 per cent. A government inquiry ruled in 2018 that the privatization of Tanzania Telecommunications Corp. in 2005, in which Kuwait’s Mobile Telecommunications acquired a 60 per cent stake, was illegal. Airtel acquired the stake in 2010 and said the purchase was in full compliance with Tanzanian law.

Other terms of the agreement include the company writing off debt of $407 million that Tanzania owed it, and that the state will appoint the entity’s chairman, a government official said.

Source: https://www.business-standard.com/a...n-to-settle-ownership-row-119061100058_1.html
 
Yaani maana yake unaruka hatua mbili mbele na kurudi kumi nyuma kisha unajipongeza.
Kwaiyo unataka kusemaje tusichukue hizo 3 billions kutoka Airtel kisa korosho inatupatia pesa nyingi zaidi?
 
Unajua taasisi ya rais sasa watalaamu hao kwako hawatoshi ? Labda sijakuelewa nini shida yako
kwahiyo watalaam ndio walio mshauli kuwa biashara ya korosho inaweza kwenda vizuri kwa kutumia jeshi kubanguwa korosho na meno ? au watalaam wake ndio walio mshauli kuwa matajiri wakiishi kama mshatani wanyonge wataishi kama bilionere ? kama huo ndio ushauri wao basi hana washauri bora awe anakuja jami forum kuchota ushauri wa bure
 
Dec 20 , 2017

Waziri Kindamba: Tunao ushahidi wa kutosha kuwa Airtel ni mali ya TTCL kwa 100% na tupo tayari kuthibitisha

Source:
Kampuni ya simu (TTCL) imetaka kurudishiwa mara moja kampuni ya Airtel kwa kuwa umiliki wake si halali.

Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL, Omar Nundu na Ofisa Mtendaji Mkuu,Waziri Kindamba wameiomba serikali kuingilia kati katika suala hilo.
 
Kwa siku hizi Mungu amekusaidia kumwelewa rais mwanzoni ulipata shida sana nilikuwa naona arguments zako huyu rais atatuacha mbali sana ilifaa baada ya Nyerere awe magufuli
Kama ni Pasco ninayemjua anakeji hayuko serious kama unavyodhani,

Gawio linapelekwa hazina siyo ikulu
 
Back
Top Bottom