Sunbae
JF-Expert Member
- Sep 14, 2015
- 254
- 176
Kampuni ya Mawasiliano nchini Vodacom Tanzania imeingia ushirikiano wa kibiashara na mtangazaji Millard Ayo. Millard na Vodacom wameingia makubaliano hayo mapema mwezi Juni mwaka huu na jana tarehe 2.7.2016 ushirikiano huo ulitangazwa rasmi.
Haijaeleweka ni kiasi gani atakuwa analipwa Millard Ayo na kandarasi hiyo ni ya myda gani lakini inasemekana ni mzigo wa maana, kwa lugha rahisi ni kwamba Millard amepewa hela ili awe anafanya matangazo ya Vodacom pekee, hivyo hatofanya matangazo ya kampuni nyingine yoyote ya mawasiliano nchini.
"Nimempata mtu wangu wa nguvu ambaye nimekuwa nikimtafuta kwa muda mrefu sasa. Pamoja tutafika nae mbali sana na leo nafuraha kukujulisha kuwa Vodacom Tanzania ndio mtu wangu wa nguvu kabisa. Na hakuna shaka maisha ni murua tukiwa pamoja. #BetterTogether"
Hii hapa chini ni video ambayo Millard kaipandisha jana kwenye ukurasa wake.